Maana ya Hija na ’UmraKatika lugha ya Kiarabu neno “Hajj” lina maana ya kuzuru au kutembelea mahali kwa lengo maalum. Katika Sharia ya Kiislamu, “Kuhiji” ni kuizuru Ka’aba - Nyumba takatifu ya Allah (s.w) - katika mwezi na siku maalum, kwa kuzingatia masharti na kutekeleza matendo yote yanayo ikamilisha ibada ya Hija kama ilivyoelekezwa katika Qur’an na Sunnah. Hija ni faradh kwa kila Muislamu ‘Mukallaf’ mwenye uwezo wa kiafya na mali mara moja katika umri wake.Neno “Umrah” lina maana ya kutembelea. Katika sharia ya Kiislamu, kufanya `Umrah” ni kutembelea nyumba takatifu ya Ka’abah katika mwezi wowote na siku yoyote katika mwaka, kwa kuzingatia masharti na kutekeleza kwa ukamilifu matendo ya `Umrah ambayo ni Kutia nia katika vituo maalum (Miqat), kuwa katika Ihram, kutufu, kusa’i na kupunguza au kunyoa nywele. Ibada ya ‘Umrah ina matendo machache zaidi kuliko ibada ya Hijja hivyo imeitwa “Hijja ndogo”. Ibadah ya ‘Umrah ni Sunnah iliyokokotezwa.Umuhimu na nafasi ya Ibada ya Hija katika UislamuHija ni nguzo ya tano ya Uislamu iliyofaradhishwa kwa waumini kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:


“... Na Mwenyezi Mungu amewawajibishia watu wafanye Hija katika Nyumba hiyo (Al-Ka’aba), yule awezaye kufunga safari kwenda huko. Na atakayekanusha (asiende na hali ya kuwa ana uwezo) basi Mwenyezi Mungu si muhitaji anayewahitajia walimwengu ”(3:9 7).Pia katika Hadith iliyosimuliwa na Abu Hurairah (r.a), Mtume (s.a.w) alitoa khutuba akasema:
“Enyi watu! Hija imeamrishwa kwenu, basi Hijini”. Mtu mmoja akauliza: “Ee Mtume wa Allah! ni kila mwaka? Mtume (s.a.w) alinyamaza mpaka


yule mtu akarudia kuuliza swali hilo mara tatu. Kisha Mtume akasem a: “kam a ningalisem a ‘ndio’, ingalikuw a faradhi kuhiji kila mw aka na pangalikuw a hakuna hiari ” (Muslim).Hija imefaradhishwa kwa Waislamu wenye uwezo wa kusafiri na kugharimia safari na masurufu, mara moja katika maisha yao. Mwenye uwezo wa kuhiji, akaacha makusudi kuhiji si Muislamu japo ataendelea kujiita Muislamu na watu wataendelea kumuita hivyo, kwani Allah (s.w) an a s em a


“...Na atakayekanusha (asiende na hali ana uw ezo) basi Mw enyezi Mungu si muhitaji, kuwahitajia w alimwengu ” (3:97).
Maneno haya ya Allah (s.w) ni makemeo makubwa sana kwa wanaopuuzia Ibada hii. Allah (s.w) hana haja na Uislamu wao, na matendo yao mema waliyofanya yataruka patupu kwani Allah (s.w) hana haja nayo. Katika kuonyesha ubaya wa kukanusha amri hii ya Hija, Mtume (s.a.w) anasema katika Hadith iliyosimuliwa na Ali (r.a) kuwa:
Yeyote atakayekuwa na uw ezo w a kuhiji katika Nyumba ya Allah, lakini asifanye hivyo akifa atakuwa hana tofauti na Myahudi au Mkristo na hiyo ni kwa sababu Allah (s.w) amesema:


“... Na Mwenyezi Mungu amewaamrisha watu wafanye Hija katika Nyumba hiyo, yule awezaye kufunga safari kwenda huko ...” (3:97) (Tirm idh).
Ni katika msingi huu Mtume (s.a.w) ameamuru katika Hadith aliyosimulia Ibn Abbas(r.a):
“Yeyote anayehusika kuhiji, na aharakishe”. (Abu Daud, Darimi).Hivyo basi mtu akifikia baleghe na akawa na afya njema na uwezo wa kugharimia safari ya Hija, Ibada hiyo itakuwa faradhi kwake na kama hataitekeleza wakati huo na ikawa uwezo huo umemuishia baada ya Hija hiyo, basi afahamu vyema kuwa atahesabiwa kuwa kavunja faradhi ya Hija. Kwa hivyo kila Muislamu anapopata uwezo wa kuhiji, hana budi kuhiji wakati huo huo.Hija na Umrah ni Ibada za hali ya juu zenye kuahidiwa malipo makubwa mbele ya Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika hadith zifuatazo:
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Atakayefunga safari ya Hija kwa ajili ya Allah bila kuongea maneno maovu na kufanya vitendo viovu, atarudi (akiwa huru na dhambi) kama siku ile aliyozaliwa na mama yake. ” (Bukhari na Muslim).Abu Hurairah (r.a) amesimulia tena kuwa Mtume wa Allah kasema: “Umra moja ni kifutio cha dhambi zilizofanywa katika kipindi kati ya Umra hii na Umra inayofuatia na Haji iliyokamilika haina malipo mengine isipokuwa Pepo. ” (Bukhari na Muslim)