nmna ya kufanya Talbiy kwa mwenye kuhiji

2.

nmna ya kufanya Talbiy kwa mwenye kuhiji

2. Talbiya



Talbiya ni maneno ya kuitikia wito wa Allah (s.w) pale alipomuamrisha Nabii Ibrahim (a.s) kuwaita watu kwa Hija:


'Na (tukamw am bia Ibrahim): Utangaze kw a w atu habari za Hija, w atakujia


(wengine) kwa miguu na (wengine) juu ya kila mnyama aliyokonda (kwa uchovu wa safari ndefu). Ili washuhudie manufaa yao na kulitaja jina la Mwenyezi Mungu katika siku zinazojulikana ...' (22:2 7-2 8).



Maneno ya kuitikia wito huu wa Allah, yaani maneno ya Talbiya, kama yalivyo katika hadith iliyosimuliwa na Abdullah bin Umar (r.a) ni haya yafuatayo:


'Labbayka Allaahumma labbayka. Labbayka laashariika laka
labbayka. Innal-hamda wanni-i-mata laka wal-mulku; laashariika laka'.



Tafsiri:
'Naitika wito wako Ee Allah, Naitika. Naitika, Ewe Usiye na mshirika, Naitika. Hakika sifa zote njema na neema zote ni zako na Ufalme ni Wako, Ewe Usiye na mshirika (Bukhari na Muslim).



Wanaume wataitika kwa sauti ya juu na wanawake wataitika kwa sauti ndogo. Kwa wale walionuia kwa Hija tu au Hija na 'Umra, Talbiya huanza mara baada ya kuvaa Ihram na kunuia, mpaka watakapotupa jiwe la kwanza katika mnara mkubwa -'Jamaratul' Aqaba' siku ya mwezi 10 Dhul-Hija.



Talbiya ya 'Umra huanzia kwenye Miiqaat baada ya kuvaa Ihram na kutia nia ya 'Umra mpaka kwenye Nyumba Takatifu ya Ka'aba. Kwa wale walionuia Hija ya 'Tamattu', wataanza Talbiya tena baada ya kuvalia Ihram kwa nia ya Hija siku ya mwezi 8 Dhul-Hija, na wataendelea mpaka wakati watakapoanza kutupa jiwe la kwanza kulenga mnara mkubwa siku ya mwezi 10 Dhul-Hija.



Wakati wa kwenda Makka Talbiya itarudiwa tena na tena. Isomwe kila baada ya swala ya faradh, kila Haji au Hajjat anapopanda na kuteremka katika kipando au chombo anachosafiria, kila akipanda na akiteremka mlima na kila anapokutana na msafara mwingine.Mtume (s.a.w) alifanya hivyo pamoja na maswahaba wake alioongozana nao katika Hija ya kuaga. Kila alipotaka Waislamu wasome talbiya aliwaamrisha kwa kusema 'Takbiir'.Kisha Masahaba wake na yeye mwenyewe walianza kusoma Talbiya kwa nguvu.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 129


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Jinsi Uislamu Ulivyokomesha Biashara ya Utumwa wakati na baada ya Mtume Muhammad (s.a.w)
- Uislamu ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s. Soma Zaidi...

Mapambano ya Mtume Muhammad dhidi ya Wanafiki na hila zao Madina
Soma Zaidi...

UANDISHI WA HADITHI WAKATI WA MASWAHABA
Wakati wa Masahaba wa Mtume (s. Soma Zaidi...

HUU NDIO USIA WA MTUME KWA WAISLAMU
' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '. Soma Zaidi...

Kuhajiri Waislamu wa Makka Kwenda Madinah
Baada ya mikataba miwili ya 'Aqabah na baada ya Waislamu 75 kufika Yathrib salama, Mtume(s. Soma Zaidi...

quran na tajwid
TAJWID Utangulizi wa elimu ya Tajwid YALIYOMO SURA YA 01 . Soma Zaidi...

Uchaguzi wa Abubakari kuwa Khalifa wa kwanza baada ya kufariki Mtume Muhammad (s.a.w)
Soma Zaidi...

Kitabu Cha Quran na sayansi
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Sifa za uchumi wa kiislamu na njia halali za uchumi na umiliki mali katika uislamu
Soma Zaidi...

HISTORIA YA KUPASULIWA KWA KIFUA AU TUMBO CHA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) AKIWA MTOTO KWA BI HALIMA
KUPASULIWA KWA KIFUA MTUMEWAKATI AKIWA MTOTO. Soma Zaidi...

Haki na Wajibu wa mume kwa mkewe na familia
Soma Zaidi...

Quran si njozi za mvurugano alizoota Mtume Muhammad
(ii)Dai kuwa Qur-an ni zao la njozi za Mtume (s. Soma Zaidi...