Namna ya kutufu, na masharti ya mwenye kutufu

3.

Namna ya kutufu, na masharti ya mwenye kutufu

3. Tawaf



Kutufu ni kitendo cha kuizunguka Ka'aba mara saba kuanzia kwenye Jiwe Jeusi (Hajaratil-aswad). Wakati wa kuzunguka Ka'aba inakuwa upande wa kushoto, yaani mzunguko ni kinyume na ule wa saa (anti-clockwise). Kutufu ndio Ibadah ya kwanza anayoifanya mwenye kuhiji au kufanya 'Umra mara tu baada ya kuizuru Ka'aba na kubusu Jiwe Jeusi.



Masharti ya Tawaf



Mwenye kutufu hana budi kuwa twahara. Yaani awe ameepukana na najisi na aina zote za hadath - asiwe na janaba, hedhi wala nifasi na awe na udhu.
Kwa wanawake wenye hedhi wanaruhusiwa kuingia katika Ihram na kufanya vitendo vyote vya Hija isipokuwa kutufu kama tunavyofahamishwa katika hadith ifuatavyo:
Amesimulia Aisha (r.a): Nilikuwa katika hedhi nilipoingia Makka, kwa hiyo sikuweza kutufu wala kusali. Kisha nilimfahamisha Mtume wa Allah, akaniambia, 'fanya vitendo vyote vya Hija kama wengine lakini usitufu mpaka uwe twahara.: (Bukhari).



Namna ya Kutufu



Kama kawaida ya kila ibada, mwenye kutufu atatia nia ya kutufu na ataanza tawafu kwa kulibusu Jiwe Jeusi kisha atasema: 'Bismillaah Allaahu Akbar'. Kama, kutokana na msongamano wa watu haitawezekana kulibusu 'Jiwe Jeusi', basi inatosha kwa kuligusa kwa mkono au kwa fimbo kisha kuubusu mkono au fimbo na kusema: 'Bismillaah Allahu Akbar'. Kama vile vile itashindikana kuligusa jiwe jeusi kwa mkono au kwa fimbo, basi itatosha kuashiria kwa mbali kwa mkono au fimbo bila kubusu mkono au fimbo hiyo, kisha utasema: 'Bismillaah Allaahu Akbar'. Hivi sasa kuna alama ya mstari mweupe uliochorwa ili kuwawezesha wale wanaozunguka mbali na Jiwe Jeusi kujua kuwa wamefika usawa na Jiwe Jeusi ili waashirie (Angalia kielelezo A na B uk. 297-8).



Wakati wa kuzunguka Ka'aba itakuwa upande wa kushoto na kuzunguka karibu na kuta za Ka'aba ni bora zaidi iwapo kuna uwezekano. Pembe nne za Ka'aba zimepewa majina. Pembe ya Mashariki ni hii yenye 'Jiwe Jeusi' inaitwa Ar-Ruknul-aswad, ambapo mzunguko huanza baada ya kulibusu Jiwe Jeusi. Pembe inayofuatia wakati wa kuzunguka huitwa Ruknul-Iraaq, hii ni pembe ya Kaskazini, inayofuatia hii ni Ruknu-Sham, hii ni pembe ya Magharibi na inayofuatia ni Ruknul-Yaman, hii ni pembe


Ibn Abbas (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: 'Kutufu katika Nyumba (Tukufu) ni kama mtu aliyeko kwenye swala isipokuwa mtu anaweza kuongea wakati wa kutufu. Kwa hiyo yeyote atakayeongea katika Tawaf hana budi kuongea maneno mazuri.' (Tirmidh, Nisai, Darimi).



Kwa wanaume ni sunnah kukimbia matiti (jogging or trotting) katika safari tatu za mwanzo, na kisha kumalizia safari nne zilizobakia kwa kutembea kawaida. Wanawake watatembea kama kawaida kwa mizunguko yote saba.Baada ya mzunguko wa saba, Haji au Hajjat ataendelea mbele mpaka pale aliposimama Nabii Ibrahim (a.s) wakati akiinua kuta za Ka'aba. Sehemu hii inaitwa 'Maqamu Ibrahim' ambapo alama ya unyayo wa Nabii Ibrahim (a.s) huonekana. Katika Qur'an tunakumbushwa juu ya alama hii.



Kwa yakini Nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya watu ni ile iliyoko Makka, yenye baraka na uwongozi kwa ajili ya walimwengu wote. Humo mna is ha ra zilizo wazi (za kuonyesha utukufu wake na ukongwe wake. Miongoni mwa hizo ni) mahali alipokuwa akisimama Ibrahim, ...' (3:96-97).
Haji atakapofika 'Maqamu Ibrahim' ataswali rakaa mbili kwa kutekeleza amri ya Allah (s.w).


'... Na mahali alipokuwa akisimama Ibrahim pafanyeni pawe pa kuswalia ...' (2:125).


Mtume (s.a.w) katika Hija ya kuaga alipofika hapa Maqamu Ibrahim alisoma kipande hiki cha aya kisha aliswali rakaa mbili. Katika rakaa ya kwanza alisoma: Suratul Kaafiruun na katika rakaa ya pili alisoma Suratul Ikhlas.



Kama kutokana na msongamano wa watu hapatakuwa na uwezekano wa kuswali karibu na sehemu hii, basi Hajj au Hajjat ataswalia sehemu yoyote katika usawa wa eneo hili la Maqamu Ibrahim.



Tawaf ya Mgonjwa au Mkongwe



Mgonjwa au mkongwe asiyeweza kutembea mwenyewe anaruhusiwa kutufu juu ya kipando kama vile mnyama au anaweza kubebwa katika machela au juu ya gari la kusukuma. Mtume (s.a.w) aliwahi kutufu juu ya mnyama alipokuwa ameumia mguu kama tunavyofahamishwa katika Hadithi ifuatayo:
Amesimulia Ibn Abbas (r.a) kuwa Mtume wa Allah alitufu akiwa juu ya ngamia (wakati huo Mtume (s.a.w) alikuwa ameumia). Kila alipofika kwenye pembe ya Jiwe Jeusi aliiashiria kwa kitu mkononi mwake na kusema: 'Allaahu Akbar' (Bukhari).



Vile vile katika Hadith ifuatayo tunafahamishwa kuwa mtu anaweza kutufu akiwa amebebwa mgongoni:
Ames imulia Ummu Salama (r.a): 'Nilimfahamisha Mtume w a Allah juu ya maradhi yangu'. Alisema: 'Tufu ukiwa umepanda juu ya migongo ya watu (ukiwa umebebwa) ...' (Bukhari).



Hukumu ya aliyekatisha Tawafu



Je, mtu akitokewa na dharura ikabidi akatishe tawafu kabla ya kumaliza mara zote saba, itabidi akirudi aanze upya? Kwa mfano mtu anaweza kutenguka udhu katikati ya tawafu ikabidi akatishe tawafu ili akatie udhu ndio arejee tena kutufu.Au, panaweza kukimiwa kwa swala ya faradh ikabidi akatishe tawafu ili ajiunge na jamaa kwa swala. Je, itabidi kuanza tawaf upya atakaporudi baada ya kutia udhu au baada ya kumaliza kuswali swala ya jamaa? Jibu la swali hili linajibiwa na Hadith ifu atayo:
'Atta (r.a) amesema: 'Kama mtu anatufu na pakakimiwa kwa ajili ya swala na swala ikaanza au kusukumwa na kutolewa nje ya sehemu' alimokuwa, hana budi kurudi na kuanzia pale alipoachia (na kumalizia safari zilizobakia)'.
Hadithi hii pia imesimuliwa na Ibn Umar (r.a) na Abdur-Rahman bin Abuu Bakr (Bukhari).


Aina za Tawaf



(i)Tawaful-Quduum
Tawaf hii ni ile inayofanywa mara tu baada ya kuingia Makka kwa 'Umra au kwa Hija. Katika tawaf hii Haji (mwanamume) atafunika bega lake la kushoto na kuacha wazi bega la kulia. Kitendo hiki kinaitwa 'Iztibaa.' Pia katika tawaf hii wanaume watakwenda matiti katika mizunguko mitatu ya kwanza. Kitendo hiki cha kukimbia matiti kinaitwa 'Ramal'. Mizunguko minne iliyobakia itamaliziwa kwa kutembea kwa hatua fupi za kawaida.



(ii)Tawaful-Ifadha (Tawaf ya Nguzo)
Tawaf hii ni miongoni mwa matendo ya nguzo za Hija na hufanywa siku ya mwezi 10 Dhul-Hija baada ya kukamilisha ibada za Rami (kutupa mawe kwenye mnara mkubwa - Jamaratul-Aqaba), Nahar (kuchinja mnyama) na Halqa (kunyoa kichwa). 'Iztibaa' na 'Ramal' hazipo katika tawaf hii. Tawaf hii wakati mwingine inaitwa 'Tawafuz `Ziyaara.'



(iii)Tawaful-Widaa
Tawaf hii ya kuaga hufanywa wakati Haji akiwa tayari kuondoka Makka kurejea makwao. Hiki ni kitendo cha mwisho cha ibada ya Hija.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 283


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Njia za kudhibiti riba
Ufumbuzi wa tatizo la ribaRiba imeenea na kuzoeleka duniani kwa kiasi ambacho watu wengi wanadhani kuwa bila riba hakuna shughuli yoyote ya uchumi inayowezekana. Soma Zaidi...

(c)Vipawa vya Mwanaadamu
Vipawa vya mwanaadamu ni sababu nyingine inayomfanya mwanaadamu asiweze kuishi bila ya kufuata dini moja au nyingine. Soma Zaidi...

Nini maana ya Kibri, madhara yake na kujiepusha na kibri
17. Soma Zaidi...

Himizo la kuwasamehe waliotukosea
'Na wasiape wale wakarimu na wenye wasaa miongoni mwenu, kujizuia kuwasaidia jamaa zao, maskini na wale waliohama kwa ajili ya Dini ya Allah; na wasamehe na waachilie mbali (wapuuze yaliyopita). Soma Zaidi...

Faida za kuwa na Huruma Kwenye Uislamu
23. Soma Zaidi...

Mitume waliosimuliwa katika Qur-an ni hawa ishirini na tano (25) wafuatao:
Adam (a. Soma Zaidi...

AMRI YA KUMFUATA MTUME (s.a.w9)
Amri ya Kumfuata Mtume (s. Soma Zaidi...

Maana na taratibu za kiuchumi katika uislamu
Soma Zaidi...

Mtume Muhammad hakujuwa kusoma wala kuandika ni hoja na kuna hekima zake
(i)Mtume Muhammad (s. Soma Zaidi...

Lengo la kuletwa mitume
Mitume wameletwa kuwa Waalimu na viongozi wa kuwafundisha watu Uislamu na kuwaelekeza kuusimamisha Uislamu katika jamii kinadharia na kimatendo kama tunavyojifunza katika Qur-an:'Kwa hakika Tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na Tukavitere.. Soma Zaidi...

Historia ya Watoto Wawili wa Nabii Adam
'Na wasomee khabari za watoto wawili wa Adam kwa kweli, walipotoa sadaka, ikakubaliwa ya mmoja wao na ya mwingine haikukubaliwa Akasema (yule asiyekubaliwa sadaka yake): 'Nitakuua'. Soma Zaidi...

Mitihani aliyopewa Nabii Ibrahimu kutoka kwa Allah
Tumeona katika historia yake kuwa Nabii Ibrahiim(a. Soma Zaidi...