4. Kusa’iKusai ni kitendo cha kutembea mara saba baina ya vilima viwili - Saffaa na Marwa vilivyo karibu na Ka’aba. Mtume (s.a.w) alipoukaribia mlima wa Saffaa, alisoma:
“Hakika Safaa na Marwa ni katika alama za (kuwepo) Allah (s.w) ....” (2:158).Kisha Mtume (s.a.w) alipanda kilima cha Saffaa kiasi cha kuweza kuiona Ka’aba, akiwa ameielekea Ka’aba (Qibla) na akiwa ameinua mikono yake juu akasema:
Hapana mola ila Allah. Allah ni Mkubwa.
Kisha Mtume (s.a.w) alisoma mara tatu:


“Hapana mola ila Allah. Allah ni mmoja asiye na mshirika. Yeye ndiye Mm ilik i (Mfa lm e) w a k ila kitu, sifa zote amestahiki Yeye na ni Muweza wa juu ya kila kitu. Hapana mola ila Allah pekee ambaye ni Mtekelezaji wa Ahadi Yake, ambaye aliwanusuru waja wake na kuwatoa maadui wake”. (Abu Daud).


Kisha baada ya kusoma hivi mara tatu Mtume (s.a.w) alishuka mlimani na kuelekea kilima cha pili - Marwa. Alipofika bondeni alikimbia matiti mpaka alipoanza kupandisha kilima cha Marwa ndio akatembea kama kawaida. Alipofika juu ya kilima cha Marwa kiasi cha kuweza kuiona Ka’aba alielekea huko na kurudia kusoma na kuleta dua kama ile aliyoileta katika kilima cha Saffa. Mtume (s.a.w) alikwenda baina ya Saffa na Marwa mara saba, akirudia Dhikiri au maneno hayo hapo juu kila alipofika katika kila kilima. Alimalizia safari yake ya saba katika kilima cha Marwa.Wale wanaofanya aina ya Hijja ya “at-Tamattu” au walionuia kufanya Umra tu, wakimaliza safari ya saba hupunguza nywele (au kuchopoa nywele kidogo) na kuvua Ihram au huwa huru na masharti ya Ihram. Ama wale walionuia Hijja tu (Al-Ifraad) au Hijja na Umra (al-Qiran) wataendelea kubakia na Ihram zao na kuendelea na Talbiya mpaka mwezi 10 Dhul Hija baada ya kutupa mawe kwenye mnara mkubwa.Na hapa ndipo unapoonekana urahisi wa Hija ya aina ya at-Tamattu.Mtume (s.a.w) aliwaamuru wale wote ambao hawakuja na wanyama wavue Ihram mpaka mwezi 8 Dhul-Hija wakati ibada ya Hija itakapoanza rasmi, ndio wavae tena Ihram na kuanza talbiya. Katika hadith ifuatayo t u n a fa ham is h wa:Mtume (s.a.w) alipofika al-Marwa kwa mara ya mwisho, alitangaza: “Kama ningelijua kabla, kama nilivyo kuja jua baadaye kuhusu dini yangu, nisingalikuja na wanyama wa muhanga (Haady) na nikafanya Umra tu. Kwa hiyo yeyote yule miongoni mwenu ambaye hakuja na mnyama anaweza kuvua Ihram na kuifanya hii Umra (Ambayo hu is ha baada ya Sai.)” Suraqa bin Jushum (r.a) aliinuka na akauliza: “Ee Mtume wa Allah, hii ni kwa mwaka huu tu au ni kwa nyakati zote”? Mtume wa Allah alifumbanisha vidole vyake na akasema: “Umra imeoanishwa na Hija daima (muda wote) mpaka siku ya mwisho (Muslim).
Baada ya Sai,Haji au Hajjat atakaa Makka mpaka siku ya Tarwiya - mwezi 8 Dhul-Hija.