Haya ndio yanayobatilisha Hija
Kubatilika kwa Hija
Hija itabatilika iwapo Haji ataacha kutekeleza moja wapo ya matendo yafuatayo:
(i) Ihram au nia ya Hija na kuwa katika hali ya Ihram ikiwa ni pamoja na vazi lake kwa wanaume na kuchunga masharti ya Ihram. Mtu akivunja masharti ya Ihram Hija haibatiliki lakini analazimika kufidia kwa kuchinja mnyama au kulisha maskini au kufunga. Ila kufanya tendo la ndoa ndani ya Ihram hubatilisha Hija kabisa.
Saβi kati ya Safaa na Marwa.
(ii) Kuhudhuria katika uwanja wa Arafat siku ya mwezi 9 Dhul- Hija kati ya kuchomoza jua la mwezi 9 dhul-Hija na alfajir ya mwezi10 Dhul-Hija.
(iii) Tawaful Ifadha (Tawafu ya Nguzo).
Lengo la Hija
Kama tulivyojifunza katika masomo yaliyopita, lengo la ujumla la kuamrishwa kusimamisha nguzo tano za Uislamu, Shahada, kusimamisha Swala, Kutoa Zaka, Kufunga Ramadhani na Kuhiji Makka - ni kumuandaa mja aweze kuishi kulingana na lengo la kuumbwa kwake na kuletwa hapa duniani. Lengo la kuumbwa mwanaadamu limebainishwa katika Qur-an kuwa ni kumwabudu Allah(s.w.) katika kila kipengele cha maisha yake (Rejea Qurβan 51:56).
Ibada ya Hijja ni kilele au ni Chuo Kikuu cha kukamilisha maandalizi ya kumfikisha Muumini katika lengo la kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w) katika kila kipengele cha maisha na kumuwezesha Muumini kuisimamisha dini ya Mwenyezi Mungu (s.w) kuwa juu ya dini zote.
Namna Hija inavyomuandaa Muumini kuwa Khalifa waAllah katika jamii
Katika sehemu hii tutaangalia falsafa ya kila kitendo cha Ibada ya Hija kuanzia maandalizi ya safari mpaka mwisho wa safari na kuonesha namna ya kila kitendo cha Hijja kinavyomuandaa mja kuwa mcha-Mungu aliyetayari kuipigania Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w) kwa hali na mali.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Simulizi za Hadithi Audio π2 Kitau cha Fiqh π3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π4 Madrasa kiganjani π5 web hosting π6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Ni nini maana ya Talaka katika uislamu
Post hii inakwenda kukufundisha maana ya neno talaka katika uislamu kisheria na kilugha.
Soma Zaidi...Kwa nini waislamu wanaoa mke zaidi ya mmoja
Post hiibitakugundisha hekima ya kuruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja katika sheria za kiislamu.
Soma Zaidi...Wenye ruhusa za kutofunga ramadhan
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Kugungisha ndoa ya kiislamu hatuwa kwa hatuwa
Hapa utajifunza jinsi ya kuozesha hatuwa kwa hatuwa. Pia utajifunza masharti ya kuoa na masharti ya kuolewa.
Soma Zaidi...