Yajuwe mandalizi ya Ibada ya hija

Yajuwe mandalizi ya Ibada ya hija

Maandalizi ya Safari ya Hija



Maandalizi ya Hija hayaanzii kwenye miezi ya Hija, bali huanzia mbali katika umri wa mtu. Tunafahamu kuwa utekelezaji wa Ibada ya Hija unahitaji kuwa na uwezo wa kifedha (kimali). Hivyo Muislamu wa kweli katika kuchuma na kutumia mali yake, hana budi kuzingatia suala la nguzo ya Zaka na nguzo ya Hija. Muislamu atakapoweka mbele yake wazo la kutoa Zaka na Kuhiji, daima atachunga mipaka ya Mwenyezi Mungu (s.w) katika kuchuma kwake, kwani anafahamu wazi kuwa mali iliyochumwa kwa njia za haramu haifai kutolea Zaka au Kuhijia. Hebu tuzingatie hadithi ifuatayo:



Ibn Umar amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Swala haikubaliwi bila ya Twahara, wala Sadaqa haikubaliwi kama inatolewa kutokana na mali iliyochumwa kwa njia za haramu. (Muslim).



Halikadhalika, kutokana na hadithi hii, Hija haitasihi endapo mtu atahiji kwa kutumia mali iliyopatikana kwa njia za haramu. Hivyo, fikra ya kuhiji, humzoesha Muumini kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu katika uchumi.



Pia fikra ya Hija humzoesha Muumini kutumia mali yake kwenye mambo muhimu tu ili kumuwezesha kuweka akiba kwa ajili ya Hija. Yaani fikra ya kutekeleza nguzo hii, humuepusha na ubadhirifu au utumiaji bila ya haja na bila ya ratiba.



Mtu anayekusudia kuhiji azidishe kutenda wema. Ajizatiti katika kusimamisha swala tano, kutoa Zaka, kufunga Ramadhani, kuwahurumia wanyonge kwa kuwapa misaada wanayohitajia na kusuhubiana vizuri na watu wote kwa ujumla. Amuombe msamaha kila aliyemkosea na amsamehe kila aliyemkosea. Pia mwenye kunuia Hija anatakiwa ajitahidi kujiepusha na maovu na azidishe kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu (s.w) kwa yote aliyokosea kwa kujua au kutojua na yaliyowazi au yaliyofichikana. Katika Qur-an Mwenyezi Mungu (s.w) anaagiza kwa wanaokusudia kuhiji:


'Na anayekusudia kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu, wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika hiyo Hija. Na kheri yoyote mnayoifanya Mw enyezi Mungu anajua ' (2:197)



Utaona mtu mwenye fikra ya kutekeleza ibada ya Hija daima atakuwa mwangalifu katika mwenendo wake wa kila siku. Atajitahidi kutekeleza maamrisho yote ya Mwenyezi Mungu (s.w) na kujiepusha na makatazo yake yote atajitahidi kuwatendea wema wanaadamu wenzake na kila mara atakuwa mwenye kujiandaa kuitika mwito wa Mola wake (Labbayka), kama vile mtu anayejiandaa kukutana na Mola wake kwa kifo, muda mfupi ujao.






                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 76

Post zifazofanana:-

MAANA NA HUKUMU YA TAJWIDI
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Swala za sunnah na faida zake
Soma Zaidi...

HUKUMU ZA MIIM YENYE SAKINA (MIIM SAKINA)
HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA : Mym sakina ni miym ambayo haina i'rab ( '). Soma Zaidi...

TEKNOLOJIA, HABARI NA MAWASILIANO
Soma Zaidi...

DALILI ZA UGONJWA WA MALARIA, (homa,uchovu, kutapika, kichefuchefu, maumivu ya kichwa n.k)
Soma Zaidi...

COMMON CAUSES OF DIABETES
Diabetes is a disease that occurs when the body fails to produce insulin or body fail to produce sufficient insulin hormone or body failure to use insulin hormone. Soma Zaidi...

nyakati za swala
3. Soma Zaidi...

NECTA FORM YWO GEOGRAPHY PAST PAPERS
Soma Zaidi...

STANDARD FOUR ENGLISH TEST 14
Soma Zaidi...

darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...

DUA 21 - 31
21. Soma Zaidi...

DAWA MBADALA ZA VIDONDA VYA TUMBO
DAWA MBADALA ZA VIDONDA VYA TUMBO Dawa za kukabiliana na zaidi ambazo zina calcium carbonate (Tums, Rolaids), zinaweza kusaidia kutibu vidonda vya tumbo lakini hazipaswi kutumiwa kama matibabu ya msingi. Soma Zaidi...