ijuwe namna ya kufanya ihram na Vazi la ihram
Ihram
Mwenye kunuia Hija au ‘Umra katika Miiqaat anakuwa katika hali ya kuchunga masharti kadhaa mpaka akamilishe matendo kadhaa ya Hija au ‘Umra. Hali hii ya kuchunga masharti hujulikana kwa jina la “Ihram ”.
Wanaume wanapokuwa katika Ihram hulazimika kuvaa vazi rasmi la Ihram.Vazi la Ihram kwa wanaume ni kuvaa shuka mbili nyeupe zisizo shonwa.Shuka moja hufungwa kiunoni na mkanda huweza kutumika ili kuhakikisha isivuke. Shuka la pili huvaliwa lubega kwa kufunika bega la kulia na kuacha wazi bega la kushoto. Katika hali ya Ihram, ni haram kwa mwanamume kuvaa nguo nyingine yoyote, ni haramu kufunika kichwa, ni haram kuvaa soksi au kuvaa viatu vinavyofunika miguu.
Wanawake hawana vazi rasmi la Ihram. Akiwa katika Ihram Hajat analazimika kama kawaida kujifunika mwili wake wote isipokuwa uso na viganja vya mikono na atavalia ushungi. Hijab yaweza kuwa ya rangi yoyote isiyovutia kama kawaida ya vazi la mwanamke wa Kiislamu lakini vazi jeupe ni bora. Mwanamke akiwa katika Ihram ni haramu kufunika uso au kuvaa soksi za mikononi(gloves). Pia wanawake katika Ihram hawaruhusiwi kuvaa soksi wala kuvaa viatu vinavyofunika miguu.
Yaliyoharamishwa kwa Mwenye kuwa katika Ihram
(i)Kujimai (kufanya tendo la ndoa) au kubusu au kukumbatiana au kufanya vitendo vingine vya kimapenzi kati ya mume na mke ambavyo vitawaletea fikra za kufanya ten do la ndoa.
(ii)Kusema maneno maovu na machafu kama vile kusengenya,kugombana, kugombanisha, kusema uwongo, kubishana, n.k. Na anayekusudia kufanya Hija katika (miezi) hiyo basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika hiyo Hija ... (2:197).
(iv) Kunyoa au kung’oa nywele, kukata kucha au kukata au kupunguza sehemu yoyote ya mwili ila kwa matibabu kama vile kuumika, kutolewa damu kwa ajili ya matibabu na mengineyo.
(vi)Kuoa au kufanya mipango ya ndoa au hata kupeleka posa.
(vii)Kujipaka manukato
(viii)Kuvaa nguo ya rangi yenye kuvutia
(ix)Kwa wanaume kuvaa nguo iliyoshonwa, na kufunika kichwa.
(x)Kwa wanawake kufunika uso na kufunika viganja vya mikono kwa kuvaa glovu (gloves).
(xi)Kuvaa viatu vinavyofunika miguu na kuvaa soksi.
(xii)Kuwinda au kusaidia kuwinda angalau kwa kuonyesha mnyama anayewindwa.
(xiii)Kula nyama iliyowindwa au iliyopatikana kwa msaada wa mtu aliyekuwa katika Ihram.
(xiv)Kula mayai ya ndege waliopatikana kwa kuwindwa.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 web hosting 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Nini maana ya protini
Unaijuwa maana ya virutubisho vya protini, na kazi zake mwilini. Soma zaidi hapa
Soma Zaidi...Kazi za tunda la papai katika kurekebisha homoni imbalance
Posti hii inahusu zaidi kazi za tunda la mpapai katika kurekebisha homoni.ni tunda ambalo ufanya kazi yake kwa sababu ya kuwepo kwa virutubisho muhimu ndani ya tunda hili.
Soma Zaidi...Faida za kula uyoga
Kula uyoga kwa faida kubwa, ja unazijuwa faida za kula uyoga kiafya
Soma Zaidi...Athari za kula vitamin C kupitiliza
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu athari za kula vitamini C kupitiliza
Soma Zaidi...