Kuepuka Maongezi yasiyo na Maana
12.
12. Kuepuka Maongezi yasiyo na Maana
Maongezi au mazungumzo yasiyo na maana ni yale yasiyoleta manufaa au kheri yoyote ila hasara tu. Mazungumzo haya yapo katika kupiga soga, kupiga porojo, kupiga hadithi za pauka pakawa, kutaniana, kubishana, na mengine ya namna hiyo. Mara zote mazungumzo ya aina hii huwapelekea watu kusengenya, kusema uwongo, kufitinisha, kugombana na kupoteza muda. Aidha mazungumzo ya aina hii huwasahaulisha watu kumkumbuka Allah (s.w).
Muumini hana budi kujiepusha na tabia hii ya kujiingiza kwenye mazungumzo ya upuuzi. Miongoni mwa sifa za waumini ni pamoja na kujiepusha na mambo ya upuuzi kama tunavyojifunza katika Quran:
“Hakika wamefuzu Waumini. Ambao katika Sw ala zao ni wanyenyekevu. Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi”. (23:1-3).
Waja wema mbele ya Allah ni pamoja:
“Na wale ambao hawashuhudii uwongo na wanapopita penye upuuzi hupita kwa heshima (zao). (25:72).
Muislamu anashauriwa daima abaki kimya kama hana la maana la kuzungumza. Mtume (s.a.w) ametuusia:
“Kuwa kimya. Hii ni njia ya kumfukuza shetani na kuimarisha dini yako” (Ahm ad).
“Anayekuwa kimya (anayenyamaza wakati hana la maana la kuzungumza) atakuw a salama ”. (Ahmad, tirmidh).
“Ni jambo bora mno kwa Muumini kuacha yasiyomhusu” (Ma lik, Ahm ad, Tirm idh).
“Ni katika ubora wa Imani ya mtu kwa kuacha kujihusisha na mambo ya upuuzi”. (Tirm idh).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 kitabu cha Simulizi 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 ai web app
Post zinazofanana:
Uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba
Nini kilichangia ongezeko la uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba.
Soma Zaidi...Dua za kuomba riziki
Dua na adhkar hizi hutumika kuomba allah akujaalie riziki kwa wepesi na iliyo halali.
Soma Zaidi...Mzazi na msafiri na mwenye kudhulumiwa dua zao hujibiwa kwa haraka
Wapo watu kadhaa ambao waliomba dua hazirudi. Hapa nitakueleza wawili ambao ni mzazi na msafiri.
Soma Zaidi...kuwa mwenye hikma au hekima na faida zake
Elimu, pamoja na ubora wake, hainufaishi bila ya kutumiwa kwa hekima.
Soma Zaidi...