Nini maana ya Kibri, madhara yake na kujiepusha na kibri

17.

Nini maana ya Kibri, madhara yake na kujiepusha na kibri

17. Kuepuka kujisifu na kujitukuza


Waislamu tumekatazwa kujisifu sisi wenyewe na pia tumekatazwa kuwasifu wengine kupita kiasi.Mtume (saw) amekataza jambo hili katika Hadith zifuatazo:
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume (saw) amependekeza kwetu kuwa tumtupie mchanga (vumbi) usoni yule anayejihusisha na kuw asifus ifu w atu kupita kiw ango kinachos tahili. (Tirim idh).


Abu Bakar (ra) amesimulia kuwa mtu mmoja alimsifu mtu mwingine mbele ya Mtume (saw). Mtume (saw) alisema mara tatu. 'Ole wako umekata kichwa cha ndugu yako!' (Kisha anasema Mtume); Yeyote miongoni mwenu ambaye ataona hapana budi kumsifu mwingine na aseme; Nafikiri fulani yuko hivi na hivi ( ana sifa hizi na hizi) na Allah (sw) atamuhesabu hivyo kama kweli mbele yake anastahiki sifa hizo. Lakini asithubutu mtu kumpachika yeyote sifa ya Ucha-Mungu(wema) juu ya Allah.' (Bukhari na Muslim)
Aidha Allah (sw) ametukataza kujisifu sifu katika aya ifuatayo:

'Yeye (Allah) ndiye anayekujueni sana tangu alipokuumbeni katika ardhi na mlipokuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msizitakase nafsi zenu; Yeye (Allah) anamjua sana aliyetakasika '. (53:32)


Kuwasifu sana watu kupita kiasi huwapelekea wale wenye kusifiwa kuvimba vichwa na kujihisi kuwa wao ni watukufu na bora zaidi kuliko wengine katika jamii. Tunayaona madhara makubwa yaliyojitokeza katika jamii ya waislamu kutokana na sifa za kupita kiasi tulizowapachika masheikhe zetu na watu wengine tuliowapachika usharifu, uwalii, ucha-mungu,n.k. Mgawanyiko wa waislamu tunaoushuhudia hivi leo kwenye madh-habu, twarika na matapo mengine mbali mbali, unatokana na dhambi hii ya kuwasifu viongozi wa hayo makundi kupita kiasi.


Pia tunajifunza katika historia kuwa chanzo cha Mitume wa Allah (sw) na watu wema kushirikishwa na Allah (s.w) ni kuwasifu kupita

kiasi. Katika Qur'an (9:30) tunafahamishwa kuwa kuwaiga washirikina waliowatangulia katika kuwasifu kupita kiasi viongozi wao, Mayahudi walimfaya Uzair (Mtu mwema) mwana wa Mungu na wakristo wakamfanya Isa Bin Maryam mwana wa Mungu. Kwa kuchelea watu wa Ummah nao wasijetumbukia kwenye shirki hii ya sifa, Mtume (saw) anatuasa katika Hadith ifuatayo:


' Imepokelewa kutoka kwa Umar(r.a) kuwa amesema Mtume wa Allah (saw) Msizidishe kwenye kunisifu kama walivyozidisha wakristo ( manasara) katika kums ifu mwana wa Maryam. Mimi ni mja wa Allah tu; kwa hiyo niiteni ;'Mja wa Allah na Mtume wake '. (Bukhari)
Hivyo muumini wa mkweli hanabudi kujiepusha na kujisifu sifu au kuwasifusifu watu. Na ikiwa hapana budi kumsifu mtu tuzingatie mipaka na tuseme kama alivyotuelekeza Mtume (saw) katika Hadith tuliyoirejea hapa juu. Tabia ya kujisifusifu au kuwasifusifu watu ni tabia ya uwongo, unafiki na ushirikina.



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 271

Post zifazofanana:-

MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO
MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO Matibabu ya vidonda vya tumbo inategemea sababu. Soma Zaidi...

CHEMSHABONGO NA BONGOCLASS
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

DARASA LA AFYA NA AFYA YA UZAZI
Jifunze mengi kuhusu Afya, kuwa nasi kwenye makala hii hadi mwisho. Soma Zaidi...

Kazi na wajibu wa khalifa katika dola ya kiislamu
Kazi na Wajibu wa KhalifaKhalifa katika Serikali ya Kiislamu ndiye mtendaji mkuu wa Serikali kama alivyokuwa Mtume(s. Soma Zaidi...

English tenses test 002
Soma Zaidi...

DARSA ZA DINI YA KIISLAMU KAMA QURAN, FIQH, SIRA, AFYA, TAJWID NA TAFSIR ZA QURAN
Soma Zaidi...

Kujiepusha na Kibri na Majivuno
Soma Zaidi...

DUA 85 - 93
SWALA YA MTUME 85. Soma Zaidi...

Homa ya Dengue, dalili za homa ya dengue na Njia ya kujikinga nayo
HOMA YA DENGUEHoma ya dengue ni miongoni mwa maradhi hatari ambayo husambazwa na mbu. Soma Zaidi...

Ni watu gani wanaopewa Zaka
Soma Zaidi...

Nataka nijue siku ya kubeba mimba mwanamke
Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KATIKA HARAKATI ZA KULINGANIA DINI
Soma Zaidi...