picha

Epuka kuwa muoga na yajue madhara ya uwoga

36.

Epuka kuwa muoga na yajue madhara ya uwoga

36. Kuepukana na Woga



Kinapokosekana kipengele hiki cha “kumtegemea Mwenyezi Mungu katika kila hali” katika tabia au mwendo wa mja nafasi yake inajazwa na kipengele cha “woga”. Woga na khofu juu ya matukio mbali mbali ya maisha ya hapa ulimwenguni husababishwa na uhaba wa imani


juu ya Allah (s.w) na sifa zake. Mtu asiyemtegemea Mwenyezi Mungu hudhania kuwa mafanikio yote ya maisha hupatikana kwa uwezo wa mwanaadamu na kuwa ni mwanaadamu pekee mwenye uwezo wa kujikinga na shari zote zinazomkabili.Dhana hii humtia mtu katika wasi wasi na woga atakapohisi kuwa tatizo au dhara fulani linalomkabili litamshinda nguvu kwa kuwa hana uwezo au msaada wa mwanaadamu wa kumuwezesha kupambana nalo.



Muislamu wa kweli hapaswi kuwa mwoga wa chochote kwa sababu hapana chochote kinachoweza kumdhuru, ila awe amekadiria hivyo Mwenyezi Mungu (s.w) na hapana mja awezaye kuepa ajali yake aliyoandikiwa na Mwenyezi Mungu. Muislamu anatakiwa awe imara katika kusimamisha Dini ya Allah katika kila kipengele cha maisha yake, bila ya kuhofu chochote kwani yeye daima yuko chini ya ulinzi na uangalizi wa Mwenyezi Mungu (s.w), na halitamsibu ila lile alilomuandikia Mwenyezi Mungu (s.w).


“Sema; halitatusibu ila alilotuandikia Mwenyezi Mungu, yeye ni Mola wetu. Basi Wa is lamu na wamtegemee Mwenyezi Mungu tu ”(9:51).
Pia Allah (s.w) ametukataza kuwaogopa makafiri:


“ Leo makafiri wamekata tamaa na dini yenu basi msiwaogope, bali
n iogop en i mimi ”(5:3).




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Jifunze Main: Dini File: Download PDF Views 1767

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 web hosting    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Umbwaji wa mwanadamu kutoka Nutfa (tone la mbegu za uzazi), alaqah (tone la damu, mudgha (pande la nyama) na kuwa mtu kamili

عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم ...

Soma Zaidi...
(x)Wenye kuepuka lagh-wi

Waumini wa kweli waliofuzu hujiepusha na Lagh-wi.

Soma Zaidi...
HISTORIA YA UANDISHI WA HADITHI

Historia fupi ya uandishi wa Hadith za Mtume (s.

Soma Zaidi...
Kitabu Cha Darsa za Funga

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...