37.
37. Kuepukana na Kukata Tamaa
Pia Muislamu hatakiwi kukata tamaa na Rehema za Mwenyezi Mungu (s.w). Hakuna kinachoshindikana kwa Mwenyezi Mungu. Muislamu hana budi kufanya jitihada katika kufanikisha jambo muhimu la maisha kwa kufuata njia za halali anazoziridhia Mwenyezi Mungu (s.w). Kama jambo hilo lina kheri na yeye, basi Mwenyezi Mungu (s.w) atalifanikisha. Mzee Yaquub (a.s) akiwausia wanawe wasichoke kumtafuta Yusuf na ndugu yake aliwaambia:
โEnyi wanangu! Nendeni mkamtafute Yusuf na nduguye, w ala msikate tamaa na Rehema ya Mwenyezi Mungu. Hawakati tamaa na Rehema ya Mw enyezi Mungu isipokuw a w atu makafiriโ. (12:87).
Pia iwapo baada ya Muislamu kufanya juhudi na kutumia uwezo wake wote, hakupata mafanikio aliyotarajia, asikate tamaa bali aridhike kuwa matokeo hayo ndiyo yenye kheri kwake kwa kuzingatia Qur-an:
โ... Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mugu ndiye anayejua, (lakini) nyinyi hamjuiโ. (2:216).
Umeionaje Makala hii.. ?
Waumini wa kweli waliofuzu hutoa Zakat wakiwa na mali na hutoa misaada na huduma waziwezazo kwa wanaadamu wenziwe kwa kadiri ya haja ilivyojitokeza.
Soma Zaidi...Ni ipi haki ya mwanamke kwenye mirathi endapo atafiwa na mume wake, ilihali yeye ni mke wa pili?
Soma Zaidi...Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...