Zijuwe Faida za Kuwa na Istiqama (Msimamo Thabiti)

38.

Zijuwe Faida za Kuwa na Istiqama (Msimamo Thabiti)

38. Kuwa na Istiqama (Msimamo Thabiti)



Muumini wa kweli anayemtegemea Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kila hali hana budi kuwa na msimamo thabiti katika kuusimamisha na kuufuata Uislamu. Si muumini wa kweli yule anayeyumba yumba (mudhabidhabina) kwa kuchanganya haki na batili au utii na uasi katika kuendesha maisha yake ya kila siku. Mwenyezi Mungu (s.w) ametuamrisha wale tutoao shahada ya kweli tuuingie Uislamu wote au tuwe Waislamu katika kila kipengele na kila hatua ya maisha yetu na wala tusiuingie nusu nusu. Anatuamrisha:


Enyi mlioamini! ingieni katika Uislamu wote, wala msifuate nyayo za shetani, kwa hakika yeye kwenu ni adui dhahiri. (2:208)
Hivyo, kutamka tu shahada au kusema: 'Tunakiri kuwa hapana Mola ila Mwenyezi Mungu na Muhammad (s.a.w) ni Mtume wake' haitoshi kutufanya kuwa Waislamu wale walioahidiwa malipo makubwa huko akhera; bali tutakuwa wa kweli katika shahada zetu iwapo tutaendesha


maisha yetu yote kama alivyotutaka tuishi Mwenyezi Mungu (s.w) na kama alivyotuelekeza Mtume wake (s.a.w). Waislamu watakaokuwa imara katika kuutekeleza Uislamu katika maisha yao ya kila siku, ndio walioahidiwa malipo makubwa ya Peponi katika maisha ya Akhera. Hebu turejee aya chache zifuatazo:


'Wale waliosema: Mola wetu ni Mwenyezi Mungu kisha wakabakia imara (wakawa na msimamo), hao huwateremkia Malaika (wakawaambia), 'Msiogope wala msihuzunike, na furahini kwa Pepo mliyokuwa mkiahidiwa. Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata vitu vinavyopendwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyovitaka '. (41:30-31).


Hakika wale waliosema: 'Mola wetu ni Mwenyezi Mungu', kisha wakatengenea (wakawa na msimamo) hawatakuwa na khofu (siku ya kufa kwao wala baadaye) wala hawatahuzunika. Hao ndio watu wa Peponi, watakaa humo (milele); ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyatenda. (46:13-1 4).
Hebu pia tuone jinsi Mtume (s.a.w) alivyotuwaidhi juu ya kuwa na msimamo katika Uislamu wetu:
Sufyaan bin Abdullah (r.a) amesimulia kuwa alisema: Ee! Mtume wa Allah niambie neno juu ya Uislamu ambalo sitakuwa tena na haja ya


kumuuliza mtu mwingine baada ya hapa. Alisema Mtume(s.a.w); 'Sema: Ninamuamini Mwenyezi Mungu kisha ubakie katika msimamo huo'. (Muslim)
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: Fuata barabara njia sahihi ya imani na kuwa na msimamo huo, na ujue kwamba hapana yeyote atakayeokoka kutokana na amali yake (nzuri). Mmoja akauliza: Hata wewe Mtume wa Allah? Akajibu (Mtume) hata mimi, ila mpaka Allah anikunjulie Rehema zake na Fadhila zake. (Muslim)


Enyi mlioamini! Kwanini mnasema msiyoyatenda. Ni chukizo kubwa mbele ya Allah kusema msiyoyatenda.
(61:2-3)




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 166

Post zifazofanana:-

NYANJA ZA AFYA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

NJIA ZA KUKABILIANA NA MINYOO: kuosha mikono, kuwa msafi, kuvaa viatu, maji safi, kuivisha nyama vyema
NJIA ZA KUKABILIANA NA MINYOO Kwa kuwa tumekwisha kuona namna ambavyo minyoo huenezwa, hivyo basi ni rahisi sasa kutaja namna ya kubambana na minyoo. Soma Zaidi...

Geography in our real life
Geography in our real life. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Spinachi
Soma Zaidi...

familia
Soma Zaidi...

TIBA ASILI ZITOKANAZO NA VYAKULA
Soma Zaidi...

Kufunga Mwezi wa ramadhani kisheria
Soma Zaidi...

Dhana ya uzazi wa mpango na historia yake duniani
Soma Zaidi...

Kumkafini maiti namna ya kushona sanda ya maiti na utaratibu wa kumvisha sanda maiti
2. Soma Zaidi...

Sifa za uchumi wa kiislamu na njia halali za uchumi na umiliki mali katika uislamu
Soma Zaidi...

.Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu
3. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula kabichi
Soma Zaidi...