ukweli na sifa zake kwenye uislamu na sifa za mtu mkweli

Ukweli ni uhakika wa jambo.

ukweli na sifa zake kwenye uislamu na sifa za mtu mkweli

  1. Kuwa Mkweli

Ukweli ni uhakika wa jambo. Muislamu wa kweli hana budi kuwa mkweli na kusimamia ukweli. Allah (s.w) anatuamrisha tuwe wakweli katika kuendesha shughuli zetu zote.

 

“Enyi mlioamini Mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli.” (9:119).

Msema kweli ni mpenzi wa Allah (s.w) . Naye Allah (s.w) amewaandalia wakweli ujira mzuri kabisa kwa hapa duniani na huko akhera kama tunavyobainishiwa katika Qur-an” kuwa Allah (s.w) atasema katika hiyo siku ya hisabu:-

 

“Hii ndiyo siku ambayo wakweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata bustani zipitazo mbele yake mito. Humo watakaa milele. Allah amewawia radhi nao wanaradhi naye. Huku ndiko kufaulu kukubwa. (5:119)

 

“... Na wanaume wasemao kweli na wanawake wasemao kweli... Allah amewaandalia msamaha na ujira mkubwa”. (33:35).

Msisitizo wa Muislamu kujipamba na tabia ya kuwa mkweli pia tunaupata katika Hadith ifuatayo:

‘Abdullah bin Mas ’ud (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Utaongea ukweli kwa sababu ukweli unaongoza kwenye Ucha-Mungu na Ucha-Mungu unaongoza kw enye Pepo. Mja ataendelea kusema kweli na kubakia katika ukweli mpaka aorodheshwe mbele ya Allah kuwa ni miongoni mwa wakweli wakubwa.Tahadharini na uwongo! Uwongo unaongoza kwenye uasi na uasi unaongoza kwenye Moto.Mja ataendelea kusema uwongo na kubakia katika uwongo mpaka aorodheshwe mbele ya Allah kuwa ni miongoni mwa waongo wakubwa”.

(Bukhari na Muslim).



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 115

Post zifazofanana:-

Faida za kiafya za kula Kisamvu
Soma Zaidi...

Vitamini C ni nini, na vipo kwenye nini?
Hapa utajifunza maana ya Vitamini C, mwaka vilipogunduliwa na aliyegundua vitamini C Soma Zaidi...

darasa la dua
Soma Zaidi...

darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...

USULUHISHWAJI KWA WALODHULUMIWA
Download kitabu Hiki Bofya hapa USULUHISHAJI WA WALODHULUMIWA. Soma Zaidi...

Zingatio:
Swala husimama kwa kuhifadhiwa na kuswaliwa kwa khushui na kudumu na swala katika maisha yote. Soma Zaidi...

What is Geography?
What is geography? Geography is a study of man and his or her environment.. Soma Zaidi...

haki za mwanamke za kisiasa katika uislamu
Haki ya Kushiriki Katika Siasa. Soma Zaidi...

Kuanzishwa kwa vitenge vya ulinza na Usalama, na usalama wa taifa
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Tangawizi
Soma Zaidi...

Nini maana ya twahara katika uislamu, na ni zipi njia za kujitwharisha
1. Soma Zaidi...

Ni yupi mtume wa mwisho? na je ni kwa nini Muhammad ndiye mtume wa mwisho?
Soma Zaidi...