picha

kujiepusha na uongo na sifa za uongo

Uwongo ni kinyume cha ukweli.

kujiepusha na uongo na sifa za uongo

  1. Kujiepusha na Uwongo

Uwongo ni kinyume cha ukweli. Uwongo ni giza na ukweli ni nuru. Uwongo ni upotofu na ukweli ni uongofu. Ambapo ukweli ni uhakika wa asili wenye kudumu, uwongo ni uzushi ambao hutoweka mara tu ukweli u nap os im am a.



“Na sema: Ukweli umefika na uwongo (batwili) umetoweka. Hakika uw ongo ndio w enye kutow eka.” (17:81)

Uongo ni uovu wenye kumuangamiza mja hapa duniani na huko akhera. Aidha uwongo ni miongoni mwa maovu makubwa mbele ya Allah (s.w) kama inavyobainika katika Hadith zifuatazo:

Abubakar (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Nikufahamisheni juu ya madhambi makubwa katika madhambi

makubwa? Sikia! Ni kumshirikisha Allah (s.w), kutotii wazazi na kusema uwongo”. (Bukhari na Muslim).

Katika Hadithi nyingine tunafahamishwa:



Abubakar (r.a) anasimulia kuwa Mtume wa Allah aliuliza: “Je, nikufahamisheni madhambi makubwa?” Aliuliza swali hilo mara tatu. Tukamjibu: “Kwa nini usitufahamishe, Ee Mtume wa Allah?” Akaeleza “Ni kumshirikisha yeyote na Allah (s.w). “Na kusema uwongo na kutoa ushahidi wa uwongo. “Aliendelea kurudia hili mpaka tukaanza kujishauri, kuwa ingelikuwa vyema kama tusingelimuuliza. ” (Bukhari)



Mtume (s.a.w) ametukataza kusema uwongo hata katika mazungumzo ya utani. Mtume (s.a.w) alitoa makemeo makali kama ifu atavyo:

Kuna Kifo kw a mtu anayejihusisha na simulizi za uw ongo ili kuchekesha watu na kuna kifo kwake, kuna kuangamia kwake. (Tirmidh).

Katika Hadith nyingine Mtume (s.a.w) amesema:

Muumini hataweza kuikamilisha imani yake mpaka aache kusema uwongo katika utani na katika midahalo hata kama ni mkweli katika mambo yote mengine. (Ahmad)

Pia katika Hadith nyingine Mtume (saw) aliulizwa;

Kuwa Mu is lamu anaweza kuwa mwoga. Akajibu “Ndiyo”. Akauliza tena, “ Je, Mu is lamu anaweza kuwa bakhili?” akajibu, “Ndiyo, anaweza kuwa bakhili. ” Aliuliza tena, “Je, Muumini anaw eza kuw a mw ongo?” Alijibu, “Hapana ”. (Malik)



Ieleweke kuwa si kwamba maovu mengine yaliyotajwa katika Hadith hii yanaruhusika, bali maovu hayo baada ya kuyafanya muislamu anaweza kutanabahi na kurejea kwa mola wake kwa kuleta toba ya kweli na toba ya kweli haipatikani mpaka awe mkweli katika kukiri makosa yake. Kwa mujibu wa Hadith, Mwongo si Muumini bali Mnafiki.

Mtume (saw) pia anatutahadharisha tujiepushe na kuwabembeleza watoto kwa kuwadanganya kuwa tutawapa zawadi fulani. Mtume(saw) anasisitiza kuwa ukimwahidi mtoto zawadi hunabudi kumletea zawadi hiyo. Tukiwadanganya watoto hao kwamba tutawapa kitu na tusiwape, tutakuwa tunawafundisha uwongo.



Uwongo na Ulaghai katika Biashara

Waislamu wa kweli hawanabudi kuwa wakweli katika kila kipengele



cha maisha yao. Imekuwa kawaida kwa wafanyabiashara waliowengi kutumia udanganyifu na ulaghai katika biashara ili kujipatia faida kubwa. Wafanyabiashara wasio waadilifu mara nyingi huwapunja watu kutokana na kutojua kwao bei halisi za vitu, hasa wanunuzi wanapokuwa wageni wa sehemu ile. Pia baadhi ya wafanyabiashara huchanganya bidhaa mbovu na nzuri au kuficha dosari (upogo) ya bidhaa na kuiuza kwa bei ya bidhaa nzima. Na baadhi ya wafanyabiashara hutumia viapo vya uwongo ili kuwahadaa watu wanunue bidhaa zao. Huu wote ni udanganyifu katika biashara. Biashara ya namna hii ni biashara haramu kama Mtume (saw) anavyotufahamisha :

“ Si halali kwa Mu is lamu kuuza bidhaa yenye dosari, mpaka azioneshe dosari hiyo kw a mnunuzi. ” (Bukhari)

“…Kiapo cha uwongo kitasaidia biashara inunuliwe , lakini inapunguza mapato”.(Ahmad)



Ni wapi uwongo unaporuhusiwa?

Katika maisha ya kila siku kuna sehemu tatu tu ambapo uwongo unaruhusiwa. Ni katika vita, katika kuleta suluhu na katika maongezi ya kusuluhishana kati ya mume na mkewe au mke na mumewe kama tunavyojifunza katika hadith zifuatazo:-



Asma bint Yazid (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah (saw) amesema: Uwongo si halali ila katika mambo matatu; uwongo wa mume kwa mkewe (au wa mke kwa mumewe) ili kumfurahisha; uwongo katika vita na uwongo katika kusuluhisha au kuleta amani kati ya watu”. (Ahmad, Tirm idh).



Ummu Kulthumu bint U’qubah (r.a) amesema, Sikumsikia Mtume wa Allah (saw) akitoa ruhusa ya kusema uwongo juu ya chochote watu wanachosema ila katika mambo matatu:- vita, kurudisha amani kati ya watu (kusuluhisha) na mazungumzo ya mume kwa mkewe au ya mke kwa mumewe”. (Muslim)



Hivyo, Muislamu wa kweli analazimika kuwa mkweli katika mazungumzo, katika mahusiano yake ya wengine na katika utendaji wake wa kila siku katika kila kipengele cha maisha yake. Atakuwa mkweli katika mazungumzo ya kawaida, katika uchumi, siasa , familia, n.k. Pia ukweli kwa muumini ni lazima upatikane katika dhamira, msimamo na utii.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sunnah Main: Dini File: Download PDF Views 1673

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Dua za Mitume na Manabii    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉6 web hosting   

Post zinazofanana:

JINSI YA KUOMBA DUA ILI IKUBALIWE NA ALLAH

Kukubaliwa kwa dua kunategemea mahusiano yako na Allah. hata hivyo kuna baadhi ya mabo ukiyafanya dua yako inaweza kukubaliwa kwa haraka zaidi. Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi ya kuomba dua ikubaliwe.

Soma Zaidi...
Hadithi Ya 32: Kusiwe Na Kudhuriana Wala Kulipiza Dhara

الحديث الثاني والثلاثون "لا ضرر ولا ضرار" عَنْ أَبىِ سَعيدٍ سَعْدِ بْن مَالكِ بْن سِنَانٍ الْخُدريِّ رضي الله عنه  أَنَّ رَسُولَ اللّ?...

Soma Zaidi...
Hadithi ya pili: sifa za muumini wa kweli

Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Faida za swala ya Mtume

Hapa utajifunza fadhila za kumswalia Mtume (s.a.w)

Soma Zaidi...
Ni zipi hadithi sahihi na hadithi Quds

Hapa tutajifunza maana ya hadithi sahihi na hadithi Quds na tofaiti zao.

Soma Zaidi...
SWALA YA MTUME (s.a.w)

SWALA YA MTUME Kumswalia Mtume (s.

Soma Zaidi...
DUA 94 - 114

DUA ZA KUONDOA WASIWASI, SIHIRI NA UCHAWI 94.

Soma Zaidi...
KUINGIA KWA WAGENI

Download kitabu Hiki Bofya hapa KUINGIA KWA WAGENI Amina na Sadie walimuonea huruma wakamuomba Zubeid amruhusu abakie.

Soma Zaidi...