Hizi ndio suna za swala kwa swala za faradhi na suna

Hizi ndio suna za swala kwa swala za faradhi na suna

Sunnah za Swala


Vipengele vya sunnah katika swala ni vile ambavyo mwenye kuswali akivitenda husaidia sana kukuza daraja ya swala yake na kuipa nguvu na msukumo mkubwa wa kuiwezesha kufikia lengo lililokusudiwa kwa urahisi zaidi. Ama mwenye kuswali akiacha kipengele chochote katika vipengele vya sunnah, swala yake itakamilika iwapo atatekeleza vipengele vyote vya nguzo. Katika Hadith tumeona kuwa Mtume (s.a.w) katika swala yake pana vipengele vya ziada ya nguzo kama ifuatavyo:


1.Kuinua viganja vya mikono mkabala na mabega, usawa wa vigingi vya masikio wakati wa kuhirimia swala, kwenda kwenye rukuu, baada ya rukuu na baada ya kutoka kwenye Tahiyyatu ya kwanza.
2.Kusoma dua baada ya takbira ya kuhirimia.
3.Kuanza na a 'udhubillaah (kumlaani Shetani) kabla ya kuanza kusoma suratul-Fatiha.
4.Kuitikia 'Aamin'baada ya kumaliza Suratul Fatiha.
5.Kusoma aya za Qur-an baada ya Suratul-Fatiha katika rakaa mbili za mwanzo.
6.Kuleta Tasbih, Tahmid na dua katika rukuu, itidali na s ijda.
7.Kutoa takbira katika kubadilisha kitendo kimoja kuendea kingine isipokuwa tu kutoka kwenye rukuu kwenda kwenye itidali ndipo tunaposema: 'Sami'Allahu liman hamidah - Rabbanaa lakal-hamdu'.
8.Kukaa na kusoma Tahiyyatu kila baada ya rakaa mbili, kwa swala zenye rakaa zaidi ya mbili.
9.Kusoma dua baada ya kumswalia Mtume na kabla ya kutoa S a la am.




                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 189

Post zifazofanana:-

Kumuandaa Maiti kabla ya kufa ama kukata roho
Soma Zaidi...

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA WANAWAKE WATATU NA CHONGO WATATU
Soma Zaidi...

Zaka ni nini? Nini maana ya zaka katika uislamu
Zaka, kilugha ni kukua; kubariki na kuzidi kheri. Soma Zaidi...

ADABU ZA KUSOMA QURAN
Adabu wakati wa kusoma quran 1. Soma Zaidi...

Nini maana ya Kushahadia nguzo ya kwanza ya uislamu
Soma Zaidi...

Je ,mafua yanayojirudia Mara kwa Mara hasa wkati was baridi ,au vumbi likiingia puan chafya haziishi,Hilo nalo ni upungufu wa vitamin c?
Soma Zaidi...

Chemistry in a real life
Application of Chemistry in our real life Soma Zaidi...

Kitabu Cha hadithi ya Chongo
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

KUAMINI MALAIKA
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Utaratibu wa kuzika, hatua kwa hatua, na namna ya kusindikiza jeneza
4. Soma Zaidi...

Ni zipi Nguzo za Udhu au Kutawadha
Soma Zaidi...

Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume
Zijuwe dawa za kuongeza nguvu za kiume, na vyakula salama vya kuongeza nguvu za kiume Soma Zaidi...