lengo la kuswali za faradhi na suna

lengo la kuswali za faradhi na suna

lengo la kuswali za faradhi na suna

Lengo la Kusimamisha Swala



Bila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya Uislamu kutokana na lengo lake. Lengo la swala limebainishwa katika Qur-an kama ifuatavyo


“Soma uliyoletewa wahyi katika kitabu (Qur-an) na usimamishe swala. Bila shaka swala (ikiswaliwa vilivyo) humzuilia (mwenye kuswali na) mambo machafu na maovu, na kw a yakini kumbuko la Mw enyezi Mungu (lililomo ndani ya swala ni jambo) kubwa kabisa (la kumzuilia mtu na mabaya). Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyatenda.” (29:45).



Kutokana na aya hii tunajifunza kuwa lengo la kusimamisha swala ni kumtakasa mja na mambo machafu na maovu. Kwa maana nyingine, tunajifunza kuwa swala ikisimamishwa vilivyo, humfanya msimamishaji awe mtu mwema mwenye kutakasika na mambo machafu na maovu na mwenye kuendea kila kipengele chake cha maisha kwa kumtii Allah (s.w). Labda tujiulize swali: “Ni nguvu gani au ni msukumo gani uliomo katika swala unaomfanya mwenye kuswali atakasike na maovu na awe na tabia njema anayoridhia Allah (s.w)” Linaloleta mabadiliko haya makubwa katika tabia na utendaji wa Muumini, ni lile kumbuko la Allah (s.w) lililomo ndani ya swala. Kwa hiyo lengo hili la swala litapatikana tu pale mwenye kuswali atakapokuwa na mazingatio na kumkumbuka Allah (s.w) katika kila hatua ya swala.




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views: 1734

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 ai web app     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 web hosting     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Dua za Mitume na Manabii     👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Nini maana ya ndoa katia uislamu na ni upi umuhimu wake

Hapa utajifunza maana ya ndoa kulingana na uislamu na umuhimu wake katika jamiii

Soma Zaidi...
NI KWA NINI TUNASWALI?, NI UPI UMUHIMU WA KUSWALI NA NI ZIPI FADHILA ZA KUSWALI

Umuhimu wa KusimamishaSwala Kwa mujibu wa Hadith ya Ibn Umar (r.

Soma Zaidi...