picha

maana ya swala kilugha na kisheria

maana ya swala kilugha na kisheria

Maana ya Swala



(a)Kilugha



Katika lugha ya Kiarabu neno “Swalaat” lina maana ya “ombi” au “dua”. Katika Qur-an tunaamrishwa kumswalia Mtume, yaani kumuombea dua Mtume (s.a.w) katika aya ifuatayo:


“Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamswalia Mtume (w anamtakia Rehema). Basi, enyi mlioamini mswalieni (muombeeni au mtakieni Mtume) Rehema na muombeeni amani”. (33:56)



Vile vile katika Hadith, Mtume (s.a.w) anatuambia:
“Yule atakayealikwa kwenye karamu ya harusi aitikie wito huo, kama hataweza kuitika amswalie (amuombee dua) aliyemkaribisha. ” (Muslimu)



(b)Kisheria



Katika sheria ya Kiislamu, “swalaat” ni maombi maalumu kwa Allah (s.w) yanayofanywa kwa kufuata utaratibu maalumu uliowekwa na Allah (s.w) na kufundishwa kwa matendo na Mtume wake. Katika maombi haya maalumu mwili mzima huhusika katika maombi haya kwa kusimama, kurukuu, kuitidali, kusujudu, kukaa na kuzingatia yale yote anayosema katika kuleta maombi haya.




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: General Main: Post File: Download PDF Views 2953

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉2 Dua za Mitume na Manabii     👉3 web hosting     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zinazofanana:

NGUZO ZA IMAN

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

Soma Zaidi...