picha

Maana ya Swaumu na Lengo la kufunga

Maana ya Swaumu na Lengo la kufunga

Maana ya Swaumu (Funga)



Kilugha; neno “Swaum” lina maana ya kujizuilia kufanya jambo lolote la kawaida. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Bibi Maryam baada ya kumzaa nabii Isa (a.s) alijizuilia (alikuwa katika Swaum ya) kutosema na mtu yoyote juu ya mtoto wake.


“... Na kama ukimuona mtu yeyote (akauliza habari za mtoto huyu) sema: `Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa Rehema ya Swaum (kufunga), kwa hiyo leo sitasema na mtu’” (19:2 6).



Katika Sharia ya Kiislamu kufunga (Swaum) ni kujizuilia kula, kunywa, kujamii, kuingiza kitu chochote katika matundu ya mwili na kujizuilia kumuasi Allah (s.w) kuanzia alfajiri ya kweli mpaka kuingia ma gharibi.


Lengo la Swaumu



Lengo la Swaum katika Uislamu ni kumuwezesha mja awe mcha Mungu kwa kufuata maamrisho yote ya Allah (s.w) na kuacha makatazo yake yote. Hivyo, ili lengo hili litimie mfungaji pamoja na kujizuilia kula, kunywa, kujamii, hanabudi pia kujizuilia na kitendo chochote kitakachompelekea kuvunja amri ya Allah (s.w) na Mtume wake (s.a.w). Kwa maana nyingine, ili Swaum ya mfungaji iwe na maana na yenye kufikia lengo, mfungaji hana budi kukizuilia (kukifungisha) kila kiungo chake cha mwili - macho, ulimi, masikio, mikono na miguu pamoja na fikra na hisia zake -na matendo aliyoyakataza Allah (s.w.).


Funga ya macho ni kujizuilia kutazama yale yote aliyoyakataza Allah (s.w), funga ya ulimi ni kujizuilia na mazungumzo yote aliyoyakataza Allah (s.w), kama vile kusengenya, kusema uwongo, kugombana n.k., funga ya masikio ni kujizuilia kusikiliza yale yote aliyoyaharamisha Allah (s.w); funga ya miguu ni kujizuilia kuendea yale yote aliyotukataza Allah (s.w); funga ya fikra na hisia, ni kujizuilia na fikra na dhana mbaya ambazo zinampelekea mja kuvunja amri na makatazo ya Allah (s.w). Ni katika maana hii Mtume (s.a.w) anasema katika Hadith zifuatazo:


“Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Yule ambaye haachi kusema uwongo na haachi kufanya vitendo viovu, Allah hana haja na kuona kuw a anaacha chakula chake na kinyw aji chake - ( Allah (s.w) hana haja na funga yake). (Bukhari).



Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema; Ni wangapi wamefunga lakini hawana funga ila kukaa na kiu tu, ni wangapi wanaoswali usiku ambao hawana swala ila huambulia kupoteza usingizi tu. (Darimi).



Hadith hizi zinatuthibitishia kuwa ufungaji usioambatana na kujizuilia na maovu na machafu, haumpatii mfungaji faida yoyote.




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views 4130

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 web hosting     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Wafundisheni kuswali watoto wenu

Mtume amemfundisha kuwa watoto wafundishwe kuswali wakiwa na miaka saba na waadhibiwe wakiacha wakiwa na miaka 10

Soma Zaidi...
Nguzo za swala.

Kipengele hiki kinaelezea nguzo mbalimbali za kuswali.

Soma Zaidi...
Watu hawa huruhusiwi kuwaoa katika uislamu

Hapa utajifunza watu ambao ni halali kuwaoa na wale ambao ni haramu kuwaoa.

Soma Zaidi...
Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za Kirumi hapo zamani

(b) WarumiJamii ya Warumi nayo ni miongoni mwa jamii zinazohesabika kuwa zilianza kustaarabika mapema katika historia ya ulimwengu.

Soma Zaidi...
Hadhi na Haki za Mwanamke katika jamii mbalimbali hapo zamani

Utangulizi:Uislamu unamuelekeza mwanaadamu namna nzuri ya kuendesha maisha yake katika kila kipengele cha maisha akiwa binafsi, katika familia na katika jamii.

Soma Zaidi...