Umuhimu, Ubora na Fadhila za kufunga

Umuhimu, Ubora na Fadhila za kufunga

Umuhimu wa Funga ya Ramadhani katika Uislamu



Funga ya Ramadhani ni miongoni mwa nguzo za Uislamu na ni faradh kwa Waislamu kama inavyobainika katika aya ifuatayo:


Enyi Mlioamini! Mmelazimishwa kufunga (swaum) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu. (2:183).
Kama ilivyo katika nguzo nyingine za Uislamu, mtu atakapoivunja makusudi nguzo hii hatabakia kuwa Muislamu japo atajiita Muislamu na watu wakaendelea kumuita hivyo. Katika Hadhith iliyopokelewa na Ibn Abbas (r.a), Mtume (s.a.w) amesema:



โ€œKuna viungo vitatu vinavyomuunganisha Muislamu na dini ya Uislamu na yeyote yule atakayevunja kiungo kimoja katika hivi atakuwa amekana Uislamu na kuuawa kwake ni halali.Viungo hivi ni: Kushuhudia kuwa Hapana Mola ila Allah, kusimamisha Sw ala Tano na Kufunga Mwezi w a Ram adhani.โ€



Katika Hadith nyingine Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa mtume (s.a.w) amesema:
โ€œYeyote yule atakayeacha makusudi kufunga siku moja ya Mwezi wa Ramadhani, hawezi kuifidia siku hiyo hata akifunga kila siku katika umri wake wote (uliobakia)โ€ (Abu-Daud).


Funga ni ibada maalum iliyo muhimu sana katika kumuandaa mja kuwa mcha Mungu kwa kule kukata kwake matamanio ya kimwili. Kwa hivyo Allah (s.w) kwa ukarimu wake ameahidi malipo makubwa kwa wenye kutekeleza ibada hii, ili iwe motisha wa kuwawezesha kuitekeleza ibada hii kwa hima kubwa na kwa ukamilifu unaotakikana.
Ahadi ya Allah (s.w) ya malipo makubwa kwa wenye kufunga Ramadhani tunaipata katika Hadith kama ifuatavyo:



Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuw a Mtume w a Allah amesema: Mw enye kufunga Ramadhani akiwa na imani na akawa na matumaini ya kupata malipo kutoka kwa Allah dhambi zake zote zilizopita husamehewa; na mwenye kusimama kw a sw ala (Tarawehe) katika mw ezi w a Ramadhani akiwa na imani na matumaini ya kupata malipo (kutoka kwa Allah), dhambi zake zote zilizopita zitasamehew a. (Bukhari na Muslim).



Pia Abu-Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume w a Allah amesema:
Kila amali njema anayoifanya mwanaadam italipwa mara kumi (Al-Qurโ€™an 6:160) mpaka kufikia mara mia saba (Al-Qurโ€™an 2:261). Allah (s.w) amesema: โ€œIla kufunga kwa sababu funga ni kwa ajili Yangu, na ni Mimi mwenyew e nitakayelipa. Mwenye kufunga anakata matamanio yake ya kimwili na anaacha chakula kwa ajili Yangu. Kwa mwenye kufunga kuna furaha mbili, furaha moja anaipata wakati wa kufuturu na nyingine wakati atakapokutana na Mola wake. Na hakika harufu ya mdomo wa mwenye kufunga ni bora mbele ya Allah (s.w) kuliko harufu ya miski. Na funga ni ngao. Kwa hiyo atakayefunga miongoni mwenu hataongea maneno ya upuuzi wala hatagombana. Kama itatokea achokozwe na yeyote, au mtu ataka kupigana naye, na aseme: โ€œNimefunga โ€. (Bukhari na Muslim).



Abdullah bin Amr (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: โ€œFunga na Qurโ€™an vitamwombea mtu shufaa. Saum itasema: Ee Bwana (Rabb) nilimwachisha chakula na kujamii wakati wa mchana, kwahiyo nifanye niw e muombezi wake. Na Qur-an itasema: Nilimwachisha usingizi wakati wa usiku, kwa hiyo nifanye niwe muombezi wake. Kwa hiyo vyote vitamuombea shufaa. โ€ (Baihaqi).



Vile vile Mtume (s.a.w.) katika kusisitiza umuhimu wa funga ya Ramadhani alitoa khutuba mwishoni mwa mwezi wa Shaabani kama ilivyonukuliwa katika Hadith ifuatayo:
Salman al-Farisy (r.a) ameeleza: Mtume (s.a.w) alituwaidhi mwisho wa siku ya Shaabani akasema: Enyi watu! Hakika umekujieni mwezi mtukufu, mw ezi uliobarikiw a, mw ezi ambao ndani yake kuna usiku ulio bora zaidi kuliko miezi elfu moja. Allah (s.w) amefaradhisha kufunga katika mwezi huu na kusimama (kwa swala ya tarawehe) katika mausiku yake ni Sunnah.


Atakayetekeleza kitendo kizuri kisicho faradhi atapata ujira wa mtu aliyetekeleza kitendo cha faradhi katika miezi mingine na yule atakayetekeleza kitendo cha faradhi atapata ujira mara 70 wa ujira wa kitendo hicho katika miezi mingine. Na ni mwezi wa subira, na ilivyo, subira malipo yake ni Pepo. Na ni mwezi wa kuhurumiana na mwezi ambao mahitaji (mapato) ya Muumini huongezwa. Atakayetoa futari kwa mwenye kufunga katika mwezi huu kuna kusamehewa dhambi zake na kuwekwa huru na Moto, na atapata malipo sawa na ya yule aliyefunga bila ya yeye kupunguziwa chochote. โ€ Tukauliza: Ee Mtume wa Allah! Hakuna yeyote kati yetu mwenye uwezo wa kumfuturisha mtu aliyefunga. Alijibu Mtume: Allah atamlipa yule mwenye kumfuturisha aliyefunga kwa funda la maziwa, au tende moja au funda la maji. Na yule anayekidhi haja ya mtu Allah atamnywesha kutokana na Birika (Kawthar) langu na hatakuwa na kiu mpaka atakapoingia Peponi.Na (Ramadhani) ni mwezi ambao mwanzo wake kuna kurehemewa, katikati yake kuna kusamehewa na mwisho wake kuna kuachwa huru na Moto. Na yule atakayempunguzia kazi mtumw a (mtumishi) wake, Allah atamsamehe, na atamuacha huru na Moto.



Hadith hizi zinatupa picha juu ya umuhimu wa funga ya Ramadhan kwamba funga ni ngao ya kumzuia Muumini na maovu yanayosababishwa na matashi ya kimwili na itakuwa ni sababu ya Muumini kuingia peponi na kuachwa huru na moto.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1597

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰2 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰3 Kitau cha Fiqh    ๐Ÿ‘‰4 kitabu cha Simulizi    ๐Ÿ‘‰5 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

Kumkafini (kumvisha sanda maiti)

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Warithi wasio na mafungu maalumu katika uislamu

Hapa utajifunza watu wanaorithi bila ya kuwekewa mafungu maalumu au viwango maalumi vya kurithi.

Soma Zaidi...
Mambo yanayobatilisha funga au yanayoharibu swaumu.

Hapa utajifunza mambo ambayo akiyafanya mtu aliyefunga, basi funga yake itaharibika.

Soma Zaidi...
Maana ya shahada

Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Kwa nini waislamu wanaoa mke zaidi ya mmoja

Post hiibitakugundisha hekima ya kuruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja katika sheria za kiislamu.

Soma Zaidi...
Sifa za imamu wa swala ya jamaa

Post hii inakwenda kukupa sifa za imamu wa msikitini anayepasa kuswalisha swala ya jamii.

Soma Zaidi...
HUKUMU YA KUUWA MTU (KUMWAGA DAMU) KWENYE UISLAMU

ุนูŽู†ู’ ุงุจู’ู†ู ู…ูŽุณู’ุนููˆุฏู ุฑูŽุถููŠูŽ ุงู„ู„ู‡ู ุนูŽู†ู’ู‡ู ู‚ูŽุงู„ูŽ: ู‚ูŽุงู„ูŽ ุฑูŽุณููˆู„ู ุงู„ู„ูŽู‘ู‡ู ุตู„ู‰ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆ ุณู„ู… "ู„ูŽุง ูŠูŽุญูู„ูู‘ ุฏูŽู…ู ุงู…ู’ุฑูุฆู ู…ูุณู’ู„ูู…ู [ ูŠุดู‡ุฏ ุฃู† ู„?...

Soma Zaidi...
Mali zinazojuzu kutolewa zaka, nisaab yake na viwango vyake

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Taratibu za eda ya kufiwa katika uislamu

Hapa utajifunza taratibu za kukaa eda kwa mwanamke ambaye amefiwa na mume.

Soma Zaidi...