Kwa nini Funga imefaradhishwa Mwezi wa Ramadhani
Japo tumefahamishwa katika Qur-an kuwa, faradhi ya funga ni kwa umma zote hatufahamu umma zilizotangulia zilifaradhishiwa kufunga miezi gani au wakati gani wa mwaka. Umma huu umefaradhishiwa kufunga katika mwezi wa Ramadhani kwa sababu ndio mwezi ilipoanza kushuka Qur-an kama tunavyofahamishwa katika aya ifu atayo:
β(Mw ezi huo mliofaradhishw a kufunga) ni mw ezi w a Ramadhani ambao ndani yake imeshuka hii Qur-an ili iwe uongozi kwa watu na hoja zilizowazi
za uongozi na upambanuzi. Atakayeshuhudia mwezi huu miongoni mwenu na afunge ....β (2:185).
Hivyo, Waislamu wameamrishwa kufunga katika mwezi wa Ramadhani ili pamoja na kutekeleza amri hii wafikie lengo lililoku su diwa, vile vle iwe ni kumbukumbu ya kushuka Qur-an, Mwongozo wa Allah (s.w) wa mwisho kwa wanaadamu. Ni kwa msingi huu kusoma Qur-an kwa wingi katika mwezi huu kumesisitizwa zaidi. Qur-an ilianza kumshukia Mtume (.s.a.w) alipokuwa Jabal-Hira, usiku wa manane katika usiku mmoja wa Mwezi wa Ramadhani. Usiku huo mtakatifu ni βLailatulβqadriβ (Usiku Wenye Cheo) kama tunavyojifunza katika Suratul-Qadr.
Hakika Tumeiteremsha (Qurβan) katika usiku w a Laylatul Qadri. Na jambo gani litakalokujulisha ni nini huo usiku wa Laylatul Qadri? Huo usiku wa heshima ni bora kuliko miezi elfu. Huteremka Malaika na roho katika (usiku) huo kwa idhini ya Mola wao kwa kila jambo. Ni amani (usiku) huo mpaka mapambazuko ya alfajiri(97:1-5)
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza kuhusu taratibu za ibada ya itiqaf yaani kukaa msikitini kwa ajili ya ibada.
Soma Zaidi...Haya ni mamno muhimu yanayozingatiwa kabla ya kuanza zoezi la kugawa mirathi ya marehemu.
Soma Zaidi...Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Milki ya RasilimaliIli kujipatia maendeleo ya kiuchumi katika zama zote mwanaadamu anahitaji rasilimali za kumwezesha kufikia azma hiyo.
Soma Zaidi...Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...