picha

Hili ndilo hasa lengo la kuamrishwa kufunga

Hili ndilo hasa lengo la kuamrishwa kufunga

Lengo la Funga



Lengo la funga limebainishwa katika Qur-an pale ilipotolewa amri ya kufunga:


“Enyi mlioamini! Mmeamrishwa kufunga kama walivyoamrishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu ”. (2:183)


Hapa tunabainishwiwa kuwa lengo la kufunga ni kuwafanya Waumini kuwa wacha-Mungu. Neno “Taqwa ” ambalo linatafsiriwa kuwa ni “Uchamungu” lina maana pana zaidi. “Taqwa” ni hali ya kuhofu ghadhabu za Mwenyezi Mungu (s.w) ambayo humfanya mja ajiepushe mbali na yale yote yanayomghadhibisha Mwenyezi Mungu (s.w) na ayaendee mbio kwa unyenyekevu na kwa jitihada kubwa yale yote aliyoamrisha Mwenyezi Mungu (s.w) na yale yote anayoyaridhia. Maana ya ‘Taqwa’ inabainishwa vyema na Hadith ifuatayo:



Siku moja Umar (r.a) alimuuliza Ubbay bin Ka ’b (r.a) amueleweshe maana hasa ya Taqwa. Ubbay (r.a) alijibu: “Amir Muuminin, umewahi kupita njia ya kichaka chenye miba?” Umar (r.a) akajibu: “Naam, nimepita mara nyingi” Kisha Ubbay (r.a) akamuuliza ni hadhari gani uliyoichukua wakati ukipita huko? “Nilishikilia na kukusanya pamoja nguo zangu na kutembea kwa uangalifu katika kupita njia hiyo”, alisema Umar (r.a) ili sehemu yoyote ya nguo zangu isije shikwa na miba hiyo”. Kutokana na jibu hili, Ubbay (r.a) alisema: “Hii hasa ndio maana ya “Taqwa”.



Kutokana na mfano huu mtu mwenye “Taqwa” au Muttaq ni yule mwenye shauku na jitihada kubwa kuepukana na kila aina ya mwiba (uovu) katika kila hatua na kila kipengele cha maisha yake yote na wakati huo huo huwa na shauku na jitihada kubwa ya kuyakimbilia mema katika kila hatua ya maisha yake ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu (s.w). Muttaq ni mtu mwenye cheo na hadhi kubwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) kama tunavyofahamishwa katika Qur-an:


“... Hakika aheshimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule aliye Muttaq (am chaye Mw enyezi Mungu zaidi) katika nyinyi. Kw a yakini Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mw enye khabari ya mambo yote. (49:13).



Hiki ni cheo kikubwa sana ambacho hakina mfano wake katika vyeo vya hapa ulimwenguni. Cheo hiki hakipatikani kwa kuomba kura au kwa hongo, bali kinapatikana kwa kujizatiti kujiepusha na makatazo yote ya Mwenyezi Mungu (s.w) na kujitahidi kutenda mema na kutekeleza maamrisho yote ya Mwenyezi Mungu (s.w) kwa matarajio ya kupata Radhi ya Mwenyezi Mungu (s.w).




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views 1437

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Dua za Mitume na Manabii     👉3 web hosting     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 ai web app    

Post zinazofanana:

Aina za talaka, sharti zake na taratibu za kutaliki katika uislamu

Maana: ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa baina ya mume na mke mbele ya mashahidi wawili kwa kuzingatia sheria ya Kiislamu.

Soma Zaidi...
Mwenendo wa Mtu aliyetoa Shahada

Muislamu aliyetoa shahada ya kweli hanabudi kumfanya Mtume (s.

Soma Zaidi...
Haki ya kumiliki mali na mipaka yake katika uislamu

Je unaijuwa mipaka yako katika kumiliki mali. Ama unajuwa haki zako katika mali inayomiliki. Endelea na somo

Soma Zaidi...
Vipi utapata uchamungu kupitia funga

Vipi lengo la funga litafikiwa na kumfanya mfungaji awe mchamungu.

Soma Zaidi...