Mgogoro wa kuandama kwa mwezi, Je mwezi wa Kimataifa ama kila Mji na mwezi wake?

Mwezi ukionekana sehemu moja, Waislamu wote ulimwenguni watalazimika kufunga?

Mgogoro wa kuandama kwa mwezi, Je mwezi wa Kimataifa ama kila Mji na mwezi wake?

Mwezi ukionekana sehemu moja, Waislamu wote ulimwenguni watalazimika kufunga?



Waislamu wote wanakubaliana kutokana na hadithi tulizozinukuu hapo juu, kuwa mtu mmoja au watu wachache wakishuhudia kuandama mwezi wa Ramadhani, Waislamu watalazimika kufunga. Pia waislamu wote wanakubaliana kuwa watu wa wili au zaidi wakishuhudia kuandama kwa mwezi wa Shawwal, Waislamu watalazimika kufuturu na kuswali Id dil-Fitr.



Hitilafu kati ya Waislamu juu ya swala la watu wachache kushuhudia kuandama mwezi wa Ramadhani au wa Shawwal ipo kwenye umbali, kwamba ni watu wa wapi wafunge watakaposikia habari za kuandama mwezi kutoka wapi? Juu ya suala hili Waislamu wamegawanyika katika makundi mawili yafu atayo:



Kundi la kwanza ni la wale wanaosema kuwa mwezi ukionekana katika mji mmoja au sehemu moja, basi Waislamu wengine popote walipo ulimwenguni watalazimika kufunga au kufungua. Haya pia ni maoni ya Imamu Hambali, Malik na Abu Hanifa. Hawa wamejiegemeza katika hadithi tulizozinukuu hapo juu.



Kundi la pili ni la wale wanaojiegemeza katika Hadithi ifuatayo: Kurayb (r.a) ameeleza kuwa Umm Fadhl, binti wa Harith alimtuma (mtoto wake) Fadhl Syria (Sham) kwa Muawiya. Fadhl aliwasili Syria na akatekeleza yale aliyotumwa na mama yake. Alipokuwa pale Syria mwezi wa Ramadhani ulianza. (Amesema Fadhl): Niliuona mwezi wa Ramadhani ulipoandama siku ya Ijumaa. Kisha nilirudi Madina mwishoni mwa mwezi. 'Abdullah bin Abbas (r.a) aliniuliza juu ya kuandama kwa mwezi wa Ramadhani na akasema: Mliuona lini? Nikajibu: Tuliuona usiku wa Ijumaa. Akaniuliza; Uliona wewe mwenyewe? Nikajibu; Ndio na watu pia waliuona na walifunga na Muawiya pia alifunga, ndipo akasema; lakini sisi tuliuona usiku wa Jumamosi. Kwa hiyo tutaendelea kufunga mpaka tukamilishe 30 au tuuone mwezi Shawwal baada ya 29 Ramadhani) Nikauliza; (Fadhili): kuonekana kwa Mwezi wa Muawiya hakukutosha? Akajibu; Hapana hivi ndivyo Mtume wa Allah (s.w) alivyotuamrisha '. (Muslim).



Kutokana na hadithi hii kama kuna masafa marefu kati ya mji ulipoonekana mwezi na mji watu walipopata taarifa juu ya kuonekana kwake haitajuzu kwao kufuata mwandamo huo, lakini endapo mji huo utakuwa umekaribiana basi watu waliopata taarifa ya kuandama mwezi kutoka mji wa karibu watawajibika kufunga au kufungua, mwanachuoni mashuhuri anayeshikilia rai hii ni Imamu Shafii.



Kutokana na hitilafu hizi, imetokea kuwa waislamu wote ulimwenguni hawaanzi kufunga Ramadhani siku moja na kuswali Iddil-Fitr na Iddil Hajj siku moja. Wale wanaoshikilia raia ya kwanza, wanaona kuwa si vyema umma mmoja wa Kiislamu kutofautiana katika matukio haya muhimu ambayo ni alama ya dini. Isitoshe kutokana na maendeleo ya sayansi, mawasiliano ulimwenguni hivi leo yamerahisika mno. Ulimwengu mzima unaweza kupata habari kwa muda wa dakika chache juu ya mwandamo wa mwezi katika mji mmoja.



Wale wanaoshikilia rai ya pili wanaoona kuwa si vyema kufunga au kufungua Ramadhani kwa kufuata habari ya kuandama kwa mwezi kutoka popote pale bila ya kujali masafa au machweo (matlai) kati ya mji huo na pale habari ya kuandamana mwezi ilipopokelewa. Kwani kijiografia sehemu mbali mbali za ulimwengu zinatofautiana sana. Kutokana na uchunguzi wa anga umepatikana ushahidi kuwa kuna kutofautiana katika kuona mwezi ambako katika mji mmoja kuna uwezekano mkubwa kabisa wa kuona mwezi endapo hapatakuwa na mawingu, katika mji mwingine ulio masafa ya mbali na matlai mengine, mwezi hauandami kabisa siku hiyo hata kama hapata kuwa na mawingu. Kwa hiyo hawa wenye mtazamo wa pili, pia kutokana na maendeleo hayo hayo ya kisayansi, wanaona kuwa hadithi zilizowaamrisha watu kufunga au kufungua kwa kupata habari ya kuandama mwezi kutoka kwa mtu mmoja au watu wachache, hazionyeshi kuwa wale walioleta habari za kuandama mwezi walitoka masafa marefu na pale alipokuwa Mtume (s.a.w).



Kutokana na rai hizi mbili, ni vema Waislamu wasigombane kwa jambo hili. Kila mtu ana uhuru wa kufuata hoja iliyomtua zaidi. Hata hivyo, lingelikuwa jambo zuri kama wanachuoni wa kila jimbo lenye uhusiano mwema kama vile Afrika ya Mashariki, wangelijadiliana na kukubaliana juu ya msimamo mmoja.




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2269

Post zifazofanana:-

JINSI YA KUDOWNLOAD VIDEO YOUTUBE
NJIA RAHISI YA KUDOWNLOAD VIDEO YOUTUBE Teknolojia ya mawasiliano ni muhimu katika kuhakikisha kuwa ulimwengu unafikika kama kijiji kimoja na hapa ndipo unapata maana halisi ya neno UTANDAWAZA yaani kwa lugha ya kimombo ni globalization. Soma Zaidi...

Sifa za waumini katika quran
Soma Zaidi...

VYNZO VYA MINYOO: nyama isiyowiva, maji machafu, kinyesi, uchafu wa mazingira, udongo
VYNZO VYA MINYOO Kama tulivyoona hapo mwanzo kuusu aina za minyoo, pia tumeona vyanzo vya minyoo hao kulingana na aina zao. Soma Zaidi...

BAADHI YA DUA ZA KILA SIKU
BAADHI YA DUA ZA KILA SIKU. Soma Zaidi...

quran na sayansi
QURANI KATIKA ZAMA ZA SAYANSI NA TEKNOLOJIAAsalaalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula viazi vitamu
Soma Zaidi...

Twahara
FIQH 1. Soma Zaidi...

HADITHI YA BINTI MWENYE KUFICHWA MTOTO WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA BINTI MWENYEKUFICHWA, MTOTO WA MFALME. Soma Zaidi...

Sababu za mdomo kuwa mchungu
Hapa utajifunza sababu zinzopelekea mdomo kubadilika ladha na kuwa mchungu, ama mchachu. Soma Zaidi...

Dawa ya fangasi uumeni
kama unasumbuliwa na fangasi uumeni, nitakujuza dawa yake, sababu za fangasi uumeni, matibabu yake na njia za kuwaepuka Soma Zaidi...

ENGLISH FOR PRIMARY SCHOOL, STANDARD FOUR
Soma Zaidi...

Kujiepusha na maringo na majivuno
Maringo, majivuno, majigambo, dharau ni vipengele vya kibri. Soma Zaidi...