Nguzo za Funga
Nguzo za funga ni mbili: Kutia Nia na kujizuilia na kila chenye kufunguza tangu mwanzo wa alfajiri mpaka kuingia magharibi.Nia ni dhamira anayokuwa nayo mtu moyoni mwake kuwa atafunga. Nia ya funga ya faradhi inatakiwa iletwe kabla ya Alfajir, kwa mnasaba wa Hadith ifu atayo:
Bibi Hafsah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: ambaye hakunuia kufunga kabla ya alfajir, hana funga. (Tirmidh, Abu Daud, Nis a i).
Ama nia ya funga za sunnah, inaweza kuletwa mchana iwapo mtu hajala chochote tangu alfajir kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Aisha, Mama w a Waumini (r.a) ameeleza: Mtume (s.a.w) alikuja kwangu siku moja akaniuliza: Una chochote (cha kula)? Nilijibu: Hakuna. Kisha akasema: βBasi nitafunga.β Siku nyingine alikuja tena kwetu tukamuambia: Mtume wa Allah, tumeletewa zawadi ya Hais (aina ya chakula cha mchanganyiko wa Tende na Siagi). Kisha akasema: βNionyeshe, nilifunga tangu asubuhi. Kisha alikula chakula kile.β (Muslim).
Katika Hadith hii tunajifunza mambo mawili. Kwanza tunajifunza kuwa mtu anaweza kunuia funga ya sunnah mchana kabla ya adhuhuri, iwapo atakuwa hajala chochote tangu alfajiri.
Pili, tunajifunza vile vile kutokana na Hadith hii kuwa mtu anaruhusiwa kuvunja funga ya sunnah pasi na sababu ya kisharia.
Umeionaje Makala hii.. ?
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mirathi katika jamii za kijahiliKatika jamii nyingi za kijahili kama vile jamii ya Waarabu kabla ya Mtume Muhammad (s.
Soma Zaidi...Katika post hii utajifunza maana ya twahara kiligha na kishria. Pia utajifunza umuhimu wake
Soma Zaidi...Hapabutajifunza endapp mwanamke anahitaji kuachwa ni nini anatakiwa afanye.
Soma Zaidi...Ni kwa nini Allah ametutaka tugunge. Je kuna lengo gani hasa katika kufunga.
Soma Zaidi...