Ni yapi mambo yanayoharibu Swaumu na Mambo yanayobatilisha funga

Ni yapi mambo yanayoharibu Swaumu na Mambo yanayobatilisha funga

Yanayobatilisha Funga



Mtu aliyefunga analazimika kujizuilia na vitendo mbalimbali ambavyo hubatilisha funga yake. Mfungaji akifanya moja wapo katika yafuatayo swaum yake itabatilika.


(i)Kula na Kunywa
Ukila au ukinywa chochote kile kwa kudhamiria hata ikiwa ni dawa utakuwa umefungulia. Vile vile ukivuta sigara au chochote kile au ukivuta dawa ya mafua kwa pua utakuwa umefungua. Pia kupitisha chochote puani au masikioni kwa kudhamiria, hata ikiwa dawa utakuwa umefu n gu a.



Ikumbukwe kuwa kujifunguza makusudi katika mwezi wa Ramadhani kwa kula na kunywa bila ya udhuru wowote wa kisharia ni kosa kubwa sana mbele ya Allah(s.w) kwa kiasi ambacho hata kama mtu atafunga umri wake wote hataweza kuilipia hiyo siku moja aliyojifunguza makusudi kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:



Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Yule anayefungua siku moja ya Ramadhani bila kuwa mgonjwa au kuwa na udhuru mwingine wa kisheria, hata akifunga maisha yake yote hataweza kuilipia funga hiyo. (Ahmad, Tirmidh, Abu Daud, Ibn Majah, Darimi).



Hadith hii inatuasa tusifanyie mas-khara amri za Allah (s.w). Hivyo mtu akijifunguza makusudi ajue wazi kuwa amefanya kosa kubwa ambalo halitasameheka kwa kuilipia tu siku hiyo bali ni lazima pia arejee kwa Mola wake kwa toba ya kweli.



(ii)Kujitapisha Makusudi
Mtu akijitapisha makusudi funga yake itavunjika kutokana na Hadith ifuatayo:
Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Anayeshindwa kuzuia matapishi halipi. Lakini anayejitapisha makusudi, na alipe. (Tirmidh, Abu Daud, Ib Majah).
Kutokana na Hadith hii kutapika kwa ugonjwa hakufunguzi.



(iii)Kupatwa na Hedhi au Nifasi
Mwanamke akipatwa na hedhi au nifasi hata kama imempata nyakati za mwisho kabla ya jua kuchwa, atakuwa amefungua na atalazimika kuilipia siku hiyo baada ya Ramadhani.



(iv)Kujitoa Manii Makusudi Ukijitoa manii kwa mkono au kwa kubusiana na kukumbatiana mume na mke, au kwa njia nyingine yoyote ile utakuwa umefungua.Kutokwa na manii kwa kuota au kwa njia nyingine isiyokuwa ya makusudi, hakufunguzi.



(v) Kunuia Kula na hali umefunga
Ukinuia kula hata kama hukula swaumu yako itakuwa imebatilika kwa kuwa utakuwa umevunja nguzo moja ya funga - nia.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 3510

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

taratibu na namna ya kutaliki, na mambo ya kuzingatia

Taratibu za Kutaliki KiislamuKama palivyo na taratibu za kuoa Kiislamu ndivyo hivyo pia ilivyo katika kuvunja ndoa.

Soma Zaidi...
Riba na Madhara Yake Katika Jamii

- Riba ni kipato chochote kile cha ziada kutokana na mkopo au mtaji bila kushiriki katika faida au hasara.

Soma Zaidi...
Kutoa vilivyo vizuri

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Swala ya jamaa.

Kipengele hiki tutajifunza kusimamisha swala ya jamaa,swala za ijumaa.

Soma Zaidi...
Uzuri wa Benki za kiislamu

Kwa nini benki za kiislamu ni bora kuliko benki nyingine?

Soma Zaidi...
Jinsi ya kiswali swala ya haja

Post hii itakufundisha kuhusu swala ya haja na jisi ya kuiswali.

Soma Zaidi...