1.
1. Twahara
Maana ya Twahara:
“Twahara” ni neno la Kiarabu lenye maana ya usafi wa nje ulioambatana na usafi wa ndani ya mtu. Usafi wa nje unahusiana na usafi wa mwili na nguo na usafi wa ndani unahusiana na utakaso wa nafsi. Mwili na nguo hutwaharika kwa kusafisha kwa kufuata maelekezo
ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Ama nafsi hutwaharika kwa kumtii Allah na Mtume wake kwa kufuata maamrisho yao na kuacha maovu na machafu waliyotukataza. Watu waliotwaharika kwa mtazamo huu hupendeza mbele ya Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
“...Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu na huwapenda wanaojitakasa (wanaojitwaharisha)” (2:222)
“...Humo wamo watu wanaopenda kujitakasa. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wajitakasao”. (9:108)
Kwa ujumla tunaweza kusema twahara kwa mtazamo wa Qur-an ni usafi wa nguo zetu, miili yetu, hisia zetu, mawazo yetu na mwenendo na tabia zetu kwa mujibu wa maelekezo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Pamoja na maana hii ya ujumla, Muislamu aliyetwaharika na kuwa tayari kusimama kwenye swala ni yule aliyeepukana na Najisi na Hadathi. Hivyo tunapojitwaharisha kwa ajili ya swala tunajishughulisha na kuondoa Najisi na Hadath.
Umeionaje Makala hii.. ?
Nguzo za uislamu: Shahada (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Talaka zimegawanyika katika makundi mengi. Katika somo hili utakwenda kukifunza aina kuu za talaka katika uislamu.
Soma Zaidi...Kabla ya kuhubiriwa uislamu watu wa Maka walikuwa na tarayibu zenye dhuluma ndani yake katika ugawaji wa mirathi.
Soma Zaidi...Endapo mke na mume wameachana na hali ya kuwa mke ana watoto wachanga. Je uislamu unasemaje kuhusu taratibu za malezi?
Soma Zaidi...Haya ni maandalizi ya kumuandaa maiti baada ya kufariki.
Soma Zaidi...Lugha ya Swala Lugha ya swala,kuanzia kwenye Takbira ya kuhirimia Swala mpaka kumalizia swala kwa Salaam, ni Kiarabu.
Soma Zaidi...