Namna ya kujitwaharisha Najisi ndogo
Kujitwaharisha Kutokana na Najisi
Kutokana na uzito wa kujitwaharisha tutazigawanya najisi katika makundi matatu
(a)Najisi ndogo.
(b)Najisi kubwa na
(c)Najisi hafifu
(a)Najisi Ndogo.
Najisi Ndogo
Inahusu najisi zote isipokuwa najisi ya mbwa na nguruwe. Namna ya kujitwaharisha kutokana na najisi ndogo ni kuosha paliponajisika kwa maji safi mpaka iondoke rangi na harufu ya najisi.
Kama tunatumia maji machache ambayo huharibika mara tu yatakapoingiwa na japo najisi ndogo, hatuna budi kutumia kata au chombo kingine cha kuchotea maji na kujitwaharisha pembeni kwa kujimiminia maji kupitia sehemu ile yenye najisi mpaka najisi hiyo iondoke.
Katika hali ya kawaida, maji safi hutumika kwa kustanjia. Tunazitwaharisha sehemu zetu za siri kwa mkono wa kushoto mpaka tuhakikishe kuwa najisi imeondoka. Katika hali ya dharura ya kukosa maji au ugonjwa usioruhusu kutumia maji, tunaruhusiwa kustanji kwa kutumia vitu vikavu kama vile karatasi laini (toilet paper), mawe, n.k. Tukistanji kwa vitu vikavu, kama vile mawe makavu tutapangusa sehemu zetu za siri kwa mawe matatu. Kama najisi ingalipo, tutaongeza mawe mawili mawili mpaka turidhike kuwa najisi imeondoka.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉2 Bongolite - Game zone - Play free game 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Jukumu la serikali katika kuzuia dhuluma
Serikali ina nafasi kubwa katika kuzuia dhulma na kufanya uchumibuwe huru kuyokana na dhulma.
Soma Zaidi...Jinsi ya kiswali swala ya haja
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya haja na jisi ya kuiswali.
Soma Zaidi...