Masharti ya udhu
        Ili udhu wa mtu ukamilike hapana budi kuchunga na kutekeleza masharti yafuatayo kabla ya kuanza kutawadha:
        (i)Kuwa na “maji safi” ya kutosha kuweza kutitirika (yasiwe ya kupakaza tu) katika viungo vya udhu vinavyooshwa.
        (ii)Kutokuwa na kitu kilichogandamana (kama vile lami, rangi, ulimbo, n.k) kitakachoweza kuzuia maji kufika kwenye ngozi ya viungo vya udhu. Ni lazima mtu aondoe hicho kilichogandamana ndio aanze kutawadha.
(iii)Kutokuwa na uchafu mwingineo au vumbi,la aina yoyote au kitu chochote juu ya viungo vya kutawadhia kitakachobadilisha rangi, harufu au tamu ya maji yatakayotiririka humo. Ni sharti mtu awe msafi kwanza ndipo aanze kutawadha.
        (iv)Kuondoa najisi juu ya viungo vya udhu kabla ya kuanza kutawadha.
        (v)Kukata kucha ndefu zinazozuia maji kufikia kona za vidole, kabla ya kuanza kutawadha.
        Masharti haya haya ndiyo masharti ya kuoga katika kuondoa hadathi ya kati na kati na hadathi kubwa, bali pamoja na hayo,kwa wanawake wenye kusuka, hawana budi kufumua misuko yao isiyoruhusu maji kupenya.
Umeionaje Makala hii.. ?
- Watumwa walikuwa wakikamatwa na kutezwa nguvu bila kujali utu na ubinaadamu wao.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu lengo la kusimamisha swala.
Soma Zaidi...Quran imegawanya mirathi katika haki. Mgawanyo huu ndio unaotakiwa utumike na si vinhinevyo.
Soma Zaidi...Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha hatuwa kwa hatuwa jinsi ya kumuosha maiti wa kiislamu
Soma Zaidi...