(c) Najisi Hafifu:
        Najisi hafifu ni mkojo wa mtoto mdogo wa kiume chini ya miaka miwili ambaye hajaanza kula chakula ila maziwa tu. Uhafifu wa najisi hii hupatikana katika kutwaharisha. Tofauti na najisi ndogo, najisi hafifu hutwaharishwa kwa kumwagia maji tu ile sehemu iliyonajisika bila ya kusugua. Hivi ndivyo alivyofanya Mtume (s.a.w) kama tunavyojifunza katika hadith ifuatayo:
        Aysha (r.a) amesimulia kuw a mtoto mchanga wa kiume aliyekuwa angali ananyonya aliletwa kwa Mtume (s.a.w) aliagiza maji na kuyamiminia juu ya pale palipo kojolewa ”. (Muslim)
        Hadathi Ndogo
        Kuwa katika hadathi ndogo ni kuwa katika hali ya kutokuwa na udhu na huondolewa hadathi hiyo kwa kutia udhu baada ya kuzingatia na kutekeleza kwa ukamilifu masharti na nguzo za udhu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Jifunze namna ya kuswali, zijuwe aina za swala na ujifunze masharti ya swala, kwa nini swala hazijibiwi? nini kifanyike?
Soma Zaidi...Zijuwe fadhila za usiku wenye cheo kuliko nyusiku ya miezi 1000.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Hapa utajifunza kuhusu taratibu za ibada ya itiqaf yaani kukaa msikitini kwa ajili ya ibada.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha kuhusu swala ya maiti, nguzo za swala ya maiti, sharti za swwla ya maiti na jinsi ya kuiswali.
Soma Zaidi...