Kujitwaharisha najisi kubwa najisi ya mbwa na Nguriwe

Kujitwaharisha najisi kubwa najisi ya mbwa na Nguriwe

Kujitwaharisha najisi kubwa najisi ya mbwa na Nguriwe

(b)Najisi Kubwa:



Najisi hii imeitwa kubwa kutokana na uzito unaochukuliwa katika kujitwah aris ha.
Namna ya kujitwaharisha kutokana na najisi ya mbwa na nguruwe ni kuikosha sehemu hiyo mara saba na mojawapo katika hayo makosho saba iwe kwa kusugua kwa udongo safi. Hivi ndivyo Mtume (s.a.w) alivyotufundisha kama inavyobainika katika Hadithi zifu atazo:



Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Kutw aharisha chombo cha yeyote kati yenu, baada ya kulambwa na mbwa ni kukikosha mara saba, ukitumia udongo katika safari ya kwanza. (Muslim)



Ibn Mughafal amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) aliamuru kuuawa mbwa (wenye ugonjwa au wasio na waangalizi) kisha akaulizwa: β€œVipi juu ya mbwa wengine?” Kisha akaruhusu kufuga mbwa kwa ajili ya kuwindia, kuchungia (na ulinzi kwa ujumla) na akasema: Mbwa atakapolambachombo, kioshe mara saba na kisugue na udongo kwa mara ya nane”. (Muslim)



Hadithi hizi zinatupa msimamo wa Uislamu juu ya mbwa, ufugaji wake na namna ya kujitwaharisha kutokana na naye. Tumejifunza kuwa japo mbwa ni mnyama najisi tunaruhusiwa kumfuga kwa ajili ya kuwindia, na ulinzi wa nyumbani. Kama itabidi tufuge mbwa kwa ajili ya madhumuni haya, tutalazimika kuwafunza na kuwatayarishia makao yao yasiyohusiana na watu kwa malazi, chakula au ukaribu wowote.



Katika utafiti uliofanywa na Daktari mmoja huko Marekani (1978) iligundulika kuwa mbwa (na nguruwe) ni wachukuzi wa vijidudu vya magonjwa mbali mbali. Baadhi ya vijidudu hivyo havifi kwa dawa yoyote isipokuwa udongo




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views: 4011

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰2 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰3 Dua za Mitume na Manabii     πŸ‘‰4 Bongolite - Game zone - Play free game     πŸ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     πŸ‘‰6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Kusimamisha swala za faradh katika nyakati za dharura.

Kipengele hichi tutajifunza namna ya kusimamisha swala ukiwa safarini na vitani na nguzo zake.

Soma Zaidi...
Usawa na uhuru wa kuchuma mali katika uislamu

Uchumi wa uislamu umeweka taratibu mbalimbali katika kuchuma mali.

Soma Zaidi...
Taratibu za kuchaguwa mchumba katika uislamu

Hapa utajifunza hatuwa kwa hatuwa za kuchaguwa mchumba kulingana na sheria za kiislamu.

Soma Zaidi...