Ni ipi hasa siku ambayo nitafute ujauzito

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kutafuta ujauzito

NI IPI HASA SIKU AMBAYO NITAFUTE UJAUZITO?

Kama ulipojifunza hapo juu kuwa zipo siku maalaumu ambazo yai hukomaa. Katika siku hizo mojawapo yai huletwa kwenye mirija ya falopia. Baada ya kukokotoa siku zako hapo juu sasa itakubidi kuongeza siku moja ama mbili nyuma. Hii ni kwa sababu makadirio ya siku hutofautiana. Na si lazima kkutafuta toto katika siku zote hizi. Unaweza kuruka kwa siku moja moja.

 

Jitahidi kufanya tendo la ndoa hasa katika siku hizo nne ulizozipata baada ya kukokotoa. Katika siku hizo jitahidi kufanya tendo siku ambayo itakuwa na sifa zifuatazo:-

 

1.Majimaji ya mwanamke ukeni yatakuwa ni mengi kuliko siku zilizopita. Mwanamke mwenyewe anaweza kujichunguza hali hii na kuigundua ila taabu. Anaweza kutumia kidole ama kitambaa safi kuchunguza uwepo wa majimaji haya katika ukeni kwake. Kumbuka hali hii isiambatane na shida nyingine za afya kama PID. Wakati mwingine inaweza kuwa ngumu kuchunguza hasa kwa wale wanaotumia uzazi wa mpango hasa hasa kwa kutumia vidonge vya homoni.

 

2.Joto la mwanamke litakuwa ni kubwa kuliko siku nyingine. Joto hili sio homa, na lisiambatane na sababu nyingine kama maumivu ya kichwa, ama kutokana na kulala sana, ama misongo ya mawazo. Kikawaida siku ambayo yai hutolewa joto la mwanamke linakuwa kubwa hivyo akishiriki siku hii ujauzito ni rahisi kuingia.

 

3.Siku ambayo mwanamke atakuwa na hamu sana ya kushiriki tendo. Wakato ambapo yai hutolewa kuna homoni huzalishwa kwa wingi. Homoni hizi zinaweza kusababisha mwanamke kutamani sana kushiriki tendo zaidi ya siku nyingine.

 

Pindi mwanamke atakapojigundua kuwa siku hii ameipata basi ni vyema kushiriki tendo ndani ya siku hii ama siku itakayofata haraka iwezekanavyo, maana yai la mwanamke linaweza kufa ndani ya muda mchach masaa 12 mpaka 24.

 

Kuna baadhi ya wanawake wanapata changamoto kutokana na kuwa na shida ya homoni katika mfumo wao wa uzazi. Hawa ni wale ambao siku zao hawazipati katika mpangilio sawa. Ni vyema wakafika kituo cha afya kupata matibabu ya tatizo hilo.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-06     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 998

Post zifazofanana:-

Vyakula vya kuoambana na mafua
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya kuoambana na mafua Soma Zaidi...

Njia za kukabiliana na presha ya kushuka
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kukabiliana na presha ya kushuka Soma Zaidi...

Kuwepo kwa maziwa wakati wa ujauzito.
Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa maziwa kwa akina Mama wakati wa ujauzito ni kawaida kwa sababu ya kuzaliwa kwa homoni ambayo usaidia kutoa maziwa. Soma Zaidi...

Zijue kazi za madini ya chuma mwilini
Posti hii inahusu zaidi kazi za madini ya chuma mwilini,Ni madini ambayo ufanya kazi mbalimbali mwilini na pia utokana na vyakula mbalimbali ambavyo upatikana kwenye wanyama na mimea. Zifuatazo ni kazi za madini ya chuma. Soma Zaidi...

Tofauti kati ya Quran na vitabu vingine vya mwenyezi Mungu
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Namna ya kujikinga na ugonjwa wa madonda ya koo
Post hii inahusu zaidi namna ya kuzuia ugonjwa wa madonda ya koo,ni njia ambazo usaidia katika kujikinga na ugonjwa wa madonda ya koo. Soma Zaidi...

PHP level 1 somo la tisa (9).
Somo la nane mafunzo ya php, katika somo hili utajifunza kuhusu array na jinsi ya kutengeneza array. Soma Zaidi...

Dalili za fangasi Mdomoni.
Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili za fangasi Mdomoni kwa watoto, vijana, watu wazima na mama wanaonyonyeshwa. Soma Zaidi...

Dalilili zinazotokea kwenye mrija wa mkojo
Mrija wa mkojo hutoa mkojo nje ya mwili lakini mrija huu unapoziba hufanya utoaji wa mkojo kutoka kwa shida au maumivu Soma Zaidi...

Hadithi ya binti wa kwanza na mbwa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

TAFSIRI (TARJIMA) YA QURAN KWA LUGHA YA KISWAHILI
Tafsiri ya Quran kwa iswahili iliyotafsiriwa na Sheikh Ali Muhsin Al-BArwani Soma Zaidi...

Dondoo za afya 21-40
Somo Hili linakwenda kukuletea dondoo mbalimbali za afya Soma Zaidi...