Ni ipi hukumu ya kutoa talaka hali ya kuwa umelazimishwa au ukiwa umerukwa na akili
Endapo mtu atamuacha mke pasi na ridhaa yake yaani amelazimishwa ama amemuwacha wakati amerukwa na akili. Je ni ipo hukumu yake.
Talaka ya Aliyerukwa na akili na aliyetenzwa nguvu
Talaka si jambo Ia kulifanyia maskhara Muislamu anatakiwa awe hadhiri wakati wa kutoa talaka. Ahakikishe kuwa wakati anaamua kutoa talaka akili yake iko katika hali ya utulivu. Talaka ya aliyerukwa na akili haiswihi kama tunavyojifunza katika Hadith:
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: "Kila talaka ni halali isipokuwa talaka ya punguani na mwenye kurukwa na akili". (Tirmidh).
Pia mtu akilazimishwa kutoa talaka pasina sababu za kisheria au mume na mke wakitalakishwa kwa nguvu huku bado wanapendana katika mipaka ya Allah (s.w), talaka hiyo haitaswihi kama tunavyojifunza katika Hadithi:
Aysha (r.a) ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allah akisema: "Hakuna talaka wala hakuna kumwacha huru mtumwa kwa nguvu ". (Tirmidh).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 ai web app 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Hili ndio lengo la kufunga.
Ni kwa nini Allah ametutaka tugunge. Je kuna lengo gani hasa katika kufunga.
Soma Zaidi...Ndoa ya mke zaidi ya mmoja katika uislamu na taratibu zake, faida zake na namna ya kuitekeleza
- Je, Ukeweza, (ndoa ya mke zaidi ya mmoja) humdhalilisha mwanamke?
Soma Zaidi...benki za kiislamu na njia zake za kuingiza kipato
Benki za KiislamuBenki za Kiislamu ambazo hutoa huduma kama benki nyingine zinaendeshwa katika msingi wa biashara na sio ule wa riba.
Soma Zaidi...