Ni ipi maana ya Imani katika Uislamu, na ni zipi sifa za muumini.

Katika Uislamu imani inanguzo kuu 6.Pia muumini anatakiwa ajipambe na sifa za waumini. Posti hii itakufundisha kuhusu imani katika Uislamu.

Maana ya imani

Imani: ni neno la Kiarabu lenye maana ya kuwa na yakini au kuwa na uhakika moyoni juu ya kuwepo kitu au jambo fulani lisiloonekana machoni lakini kuna dalili za kuthibisha kuwepo kwake

 

. Hivyo ili mtu awe na imani juu ya jambo lolote lile asiloweza kuliona, hanabudi kuwa na ujuzi wa kina utakaompa hoja au dalili za kutosha zitakazomkinaisha moyoni juu ya kuwepo jambo hilo.

 


Nani Muumini?
Imani ni kitu cha moyoni kisichoonekana lakini dalili za Muumini huonekana kwenye matendo. Katika Uislamu mtu hatakuwa Muumini kwa kudai tu bali uumini wake utaonekana katika matendo yake.

 

Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa:

“Na katika watu wako wasemao, ‘tumemuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na hali ya kuwa wao si wenye kuamini.”(2:8).
Si wenye kuamini kwa sababu hawajaingiza imani yao katika matendo bali wamebakia kwenye kudai tu kuwa wao ni waumini pengine kwa kujiita majina au kuchagua kufanya vitendo fulani fulani tu.

 

Muumini wa kweli ni yule atakayethibitisha imani yake katika mwenendo na matendo yake ya kila siku.

 

“Hakika wanaoamini kweli ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa hofu, na wanaposomewa aya zake huwazidishia imani na wanamtegemea Mola wao tu basi.(8:2).

 

Ambao husimamisha swala na wanatoa katika yale tu liy ow apa. (8:3).

 

Hao ndio wanaoamini kweli kweli, wao wana vyeo (vikubwa) kwa Mola wao, na msamaha na riziki bora kabisa”. (8:4).

 

“Wenye kuamini kweli kweli ni wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake kisha wakawa si wenye shaka na wanaopigania dini ya Allah kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio wenye kuamini kw eli kweli” (49:15)

 

Sifa za waumini

 1. KUMCHA ALLAH

 2. IMANI HUONGEZEKA

 3. KUMTEGMA ALLAH

 4. KUSWALI

 5. KUSAIDIANA

 6. KUFANYA BIASHARA NA ALAAH

 7. KUWA NA KHUSHUI

 8. KUHIFADHI SWALA

 9. ZINGATIO

 10. KUEPUKA LAGHAWI

 11. KUTOA

 12. KUEPUK UZINIFU

 13. KUWA MUAMINIFU

 14. KUCHUNGA AHADI

 15. KUTENDA WEMA

 16. KUEPUKA UGOMVIJe! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/14/Wednesday - 06:26:08 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 869


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-