image

Ni kwa nini riba imeharamishwa kwenye Uislamu

Hapa utajifinza uharamu wa riba na sababu za kuharamishwa kwake.

Uharamu wa Riba katika Uislamu

Kwanza, Uislamu umeharamisha riba kwa sababu ni dhulma (unyonyaji).Ukichukua mkopo wa riba uliochukuliwa kwa madhumuni ya kukidhi haja ya matumizi ya lazima ya nyumbani, utozaji wa riba unakiuka lengo la Allah la kuumba (kuleta) mali kwa wanadamu. Utaratibu aliouweka Allah ni kwamba kwa kuwa mali ameileta kwa wanaadamu wote:

 

“Yeye (Allah) Ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi...” (2:29).
Ni lazima matajiri (wenye mali) wawapatie wanyonge na wenye dhiki mahitaji yao muhimu ya maisha.

 


Pili, riba imeharamishwa katika Uislamu kwa sababu inahamisha mali kutoka kwa maskini au wanyonge na kuipeleka kwa tajiri ambayo huzidi kuondoa usawa katika mgawanyo wa mali. Hii ni kinyume na mahitaji ya jamii. Uislamu unataka kila mtu apate mahitaji muhimu ya maisha. Hivyo wale walio na ziada ya mahitaji muhimu ya maisha wanatakiwa wawape wasionacho kabisa au wale waliopungukiwa kwa upendo na udugu. Riba inakanusha kabisa msimamo huu.

 


Tatu, riba imeharamishwa katika Uislamu kwa sababu hufanya kundi la watu katika jamii liishi kivivu bila ya kufanya shughuli yoyote ya uzalishaji, likitegemea kuishi kwa riba kutokana na mali zao walizozikusanya katika mabenki, bima, na vyombo vingine vya riba. Jamii inakosa mchango wa watu hawa katika uzalishaji na si hivyo tu, bali watu hawa wanakuwa mzigo na bughudha katika jamii. Ufasiki (uharibifu) wa aina zote katika ardhi hufanywa na kundi hili.

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 789


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Ni mali ipi inatakiwa kutolewa zaka?
Soma Zaidi...

Kufunga Mwezi wa ramadhani kisheria
Soma Zaidi...

Kujitwaharisha kutokana na najisi
Post hii itakufundisha namna ya kutwaharisha Najisi. Soma Zaidi...

Kutoa vilivyo vizuri
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

MARADHI MENGINE 10 YANAYOTOKANA NA MBU ( matende, ngirimaji, homa ya manjano, n.k
Tofauti na maradhi yaliyotajwa hapo juu pia tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwepo kwa maradhi mengine hatari yanayosambazwa na mbu, kama vile ngirimaji pamoja na matende. Soma Zaidi...

Tofauti kati ya zakat na sadaqat
Nguzo za Imani, tofauti kati ya sadaqat na zakat (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

msimamo wa uislamu juu ya kupanga uzazi na uzazi wa mpango
Msimamo wa Uislamu juu ya kudhibiti uzaziKama tulivyoona, msukumo wa kampeni ya kudhibiti kizazi, umetokana na mfumo mbaya wa kijamii na kiuchumi ulioundwa na wanadamu kutokana na matashi yao ya ubinafsi. Soma Zaidi...

Maana ya shahada kama nguzo ya kwanza ya uislamu
4. Soma Zaidi...

Maana ya Hija na Umuhimu wa kuhiji
Soma Zaidi...

Sifa za stara na mavasi katika uislamu
2. Soma Zaidi...

Mifano na namna ya kurithisha
Ugawaji wa mirathi-Mume ana nusu (1/2) = 1/2 -Mama ana sudusi. Soma Zaidi...

Jinsi ya kushona sanda ya maiti na kumvisha yaani kumkafini
Hapa utajifunza taratibu za kumkafini maiti wa kiislamu. Yaani kushona sanda yake na kumvisha. Soma Zaidi...