Ni nini maana ya Tajwid, na ni ipi nafasi yake kwenye uislamu
Hapa utajifunza maana ya Tajwid kilugha na kisheria. Pia nitakujuza jukumu ya kusoma tajwid.
Neno ‘Tajwiyd ’
linatoka na neno جَ و د (jawwada) kilugha ina maana ‘ufundi’, yaani kufanya kitu kwa uhodari au ustadi.
Maana yake Kishariy’ah: Kuitamka kila herufi kama inavyotakiwa kutamkwa, kwa kuipa haki yake na swiffah zake huku ukifuata hukmu zote za Tajwiyd.
Katika qurani na sunnah imehimizwa sana kusoma qurani kwa tajwid au tartila. Elimu hii ya tajwid imeanza zamani toka enzi za masahaba na toka mtume yupo hai. Pia alikuwa Mtume akiwaelekeza masahaba kwa watu maalumu ili wapate kujifunza qurani kiufasaha. Imepokewa kuwa Mtume (s.a.w) amesema: ((Mwenye kupenda kuisoma Qur-aan kama vile ilivyoteremshwa basi na asome kwa Qiraa-ah [kisomo] cha ibn Ummi ‘Abd)) (amepokea Ibn Majah na ahmad)
Pia Allah amesema :وَرَتِّلِ ٱلْقُرْءَانَ تَرْتِيلً “na soma Qur-aan kwa tartiylaa (kisomo cha utaratibu upasao” Katika kuonesha maana ya neno tartiyla ‘Aly Ibn Abi Talib ambaye ni khalifa wa nne baada ya kufariki mtume amesema: التَّتيلُ هُوَ تَجيد الحْوفَ ومَ عْ رِفةِ الوقوفِ “Ni kuisoma Qur-aan kwa ujuzi wa kutamka herufi ipasavyo na kuwa na ujuzi wa hukmu za kusimama”
Hukumu ya kujifunza tajwid:
Kusoma qurani bila ya tajwid yaani kuchunga herufi ni katika makosa mbele ya maulamaa wa tajwid. Maulamaa wa elimu hii wanazungumza kuwa kujifunza tajwid ni faradh al-kifaya kwa kauli za walio wengi. Pia wapo wanaosema ni faradh ‘ayn yaani ni faradhi ya lazima kwa kila muislamu.
Hawa waliosema ni faradhi kifaya yaani sio faradhi ya lazima kwa wote ila inatosha kwa wachache wakiwa na elimu hii, kundi hili pia linazungumza kuwa inapasa kwa msomaji asisome kwa kukosea ijapokuwa hajui hukumu za tajwiid. Yaani achunge matamchi kama yalivyoandikwa asije akatamka vinginevyo na kubadilisha maana.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 ai web app 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 web hosting 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Sababu za kushuka surat al Zilzalah
surat Zalzalah ni sura ya 99 katika mpangilio wa Quran, na ina aya 8. Sura hii imeteremshwa Madina ila pia kuna kauli zinathibitisha kuwa ni ya Makkah. Katika hadithi iliyopewa daraja la hassan na Imam Tirmidh Mtume S.A.W amesema kuwa kusoa surat Zilzalah
Soma Zaidi...Hukumu za Idh-har na id-gham katika laam al-maarifa
Laam al- maarifa inaweza kusomwa kwa idgham au idh-har pindibitakapokutana na herufi za shamsiya au qamariya.
Soma Zaidi...Hukumu ya tafkhim na tarqiq katika usomaji wa Quran tajwid
Tarqiq ni kuisoma herufi kwa kuipa wepesi na tqfkhim ni kuisoma herufi kwa kuipa uzito.
Soma Zaidi...Maana ya qalqala na aina zake katika usomaji wa Quran tajwid
Qalqala imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Qalqalatul qubra yaani qalqala kubwa na qalqalat as shughura yaani qalqala ndogo.
Soma Zaidi...