image

Ni nini maana ya twahara na kujitwaharisha?

Posti hii inakwendabkukujiulisha maana ya twahara na jinsi ya kujitwaharisha.

Maana ya Twahara:

“Twahara” ni neno la Kiarabu lenye maana ya usafi wa nje ulioambatana na usafi wa ndani ya mtu. Usafi wa nje unahusiana na usafi wa mwili na nguo na usafi wa ndani unahusiana na utakaso wa nafsi. Mwili na nguo hutwaharika kwa kusafisha kwa kufuata maelekezo

 

ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Ama nafsi hutwaharika kwa kumtii Allah na Mtume wake kwa kufuata maamrisho yao na kuacha maovu na machafu waliyotukataza. Watu waliotwaharika kwa mtazamo huu hupendeza mbele ya Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:

 

“...Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu na huwapenda wanaojitakasa (wanaojitwaharisha)” (2:222)

 

“...Humo wamo watu wanaopenda kujitakasa. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wajitakasao”. (9:108)
Kwa ujumla tunaweza kusema twahara kwa mtazamo wa Qur-an ni usafi wa nguo zetu, miili yetu, hisia zetu, mawazo yetu na mwenendo na tabia zetu kwa mujibu wa maelekezo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

 


Pamoja na maana hii ya ujumla, Muislamu aliyetwaharika na kuwa tayari kusimama kwenye swala ni yule aliyeepukana na Najisi na Hadathi. Hivyo tunapojitwaharisha kwa ajili ya swala tunajishughulisha na kuondoa Najisi na Hadath.

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1160


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Zijuwe funga za sunnah na jinsi ya kuzifunga
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu funga za sunnah na jinsi ya kuzigunga. Soma Zaidi...

malezi ya mtoto mchanga baada ya talaka
Soma Zaidi...

Vituo vya kunuia hijjah au umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sheria Katika Uislamu
4. Soma Zaidi...

Maana ya Hija na Umuhimu wa kuhiji
Soma Zaidi...

lengo la kuswali za faradhi na suna
Soma Zaidi...

Haki za kiuchumi za mwanamke katika uislamu
Haki za UchumiKuwa imara kiuchumi ni sababu mojawapo kubwa ya kumpa mtu hadhi katika jamii. Soma Zaidi...

familia
Soma Zaidi...

Hali ya kuzuiliana kurithi katika uislamu
KuzuilianaTumeona kuwa wanaume wenye kurithi ni 15 na wanawake wanaorithi ni 10. Soma Zaidi...

hizi ndio nguzo za swala, swala za faradhi na suna
Soma Zaidi...

Aina ya talaka zisizo rejewa
2. Soma Zaidi...

.Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu
3. Soma Zaidi...