NIMLAUMU NANI part 1
Post hii inahusu hadithi Moja ya kijana maaalufu aliyeitwa Frank, ni kijana aliyekuwa mwaminifu ila amekumbana na wasichana wengi wanamasaliti ukizingatia Frank alikuwa kijana mstaalabu na mwaminifu sana ila anafikia kufanya maamuzi magumu kufuatana na ku
"NIMLAUMU NANI"
1. Ni asubuhi Moja nzuri iliyokuwa na upepo kidogo na jua kuanza kujitokeza huku ndege wakiimba nyimbo nzuri na watu wakijiandaa kwenda makazini, ila kwa sababu Frank siku hiyo hakuwa na picha atatokea wapi kwa sababu yeye kupata kazi kwa siku ilikuwa ni majaliwa ya mwenyezi Mungu kwa sababu alitegemea vibarua Ili mkono uweze kuingia kinywani kwa hiyo siku hiyo alikuwa Hana picha na hata hajapata mtu wa kumwita kumpatia kibarua. Frank aliendelea kuvuta shuka ghafla akasikia simu ikiitia kupokea anasikia maneno makali kutoka kwa mpenzi wake Amina, ni maneno ya kusikitisha yakisema.
2. "Wewe ni mpenzi gani maskini naona huwezi kunitunza kwa hiyo chukua zako hamsini na mimi nichukue zangu hamsini kwa sababu siwezi kuishi na mvulana maskini Kama wewe" maneno haya yalimchoma sana Frank na yalimfanya ahamke kutoka usingizi na kukimbia kwenda dukani kutafuta vocha kwa ajili ya kuongea na mpenzi wake Amina, lakini Amina alimjibu hivi, " yaani wewe maskini hujanielewa sikutaki na usinifatilie na koma kwa sababu mimi sio wa kiwango chako, baada ya Frank kusikia maneno kama hayo aliumia sana na kuwa na uchungu sana kwa sababu alitegemea sana Amina kama faraja kwake, alifikilia sana akajipigapiga kichwa ,akajishauri na akaamua kwenda kwa rafiki yake James kuomba ushauri Ili kumbembeleza Amina kuendelea kuwa karibu na frank.
3 Basi frank aliamua kujiandaa vizuri kwenda kwa rafiki yake James kumwambia yaliyo moyoni, ingawa Frank alikuwa na uchungu aliamua kuwa mkakamavu Ili asiweze kuonyesha uchungu kwa watu aliokutana nao kwa sababu ilimpasa kupanda daladala kwa sababu Kuna mwendo kama saa moja hivi, Frank alikuwa kwenye kituo cha daladala anmesubiri daladala ghafla akaja gari linaendeshwa na msichana mlembo sana yule msichana akamwambia frank aingie kwenye gari ampe lift akihaidi kumfikisha pale anapoenda basi frank akakubali akapanda lile gari na alifurahi kwa sababu na nauli kwake ilikuwa ni shida.
4. Basi frank alipokuwa kwenye gari alikuwa na uzuni, ila yule msichana aliamua kusimamisha gari Ili kujua yaliyompata Frank, basi frank akapaswa kumwambia msichana yaliyompata yule msichana akaumia sana akaamua kumpa Frank moyo na kumpatia frank number za simu Ili waje kuongea baadae basi frank akafikishwa kwa rafiki yake wakaagana na yule msichana wakapeana number za simu basi frank alipofika kwake na James akabisha hodi hakufunguliwa akazunguka nyuma ya nyumba hakuona mtu baadae aliamua kuingia ndani mpaka chumbani kwa James ndipo aliposhutuka kuwakuta James na Amina wako kitandani wamekumbatiana.
Itaendelea.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
NIMLAUM NANI? (Sehemu ya pili)
Post hii ni mwendelezo wa hadithi iliyopita ambapo Frank aliwakuta Amina ambaye ni mpenzi wake ameumbatiana na James ambaye ni rafiki yake ,kwa hiyo tuendelee kusikia yaliyotokea baada ya Amina na James kukutwa na Franki.
Soma Zaidi...Hasara za wivu na kutokuwa wazi ( sehemu ya 2)
Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu na kutokuwa wazi sehemu ya pili, sehemu hii inahusu mama Lisa anaenda kwa mama lina ili kuuliza kinachoendelea kwa mtoto wake , kwa hiyo tuona atapata jibu gani.
Soma Zaidi...Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili, hapa tunaona Jackie anajibu barua ya Julius kwa kusema yafuatayo.
Soma Zaidi...NIMLAUMU NANI ( sehemu ya tano)
Post hii inahusu mwendelezo wa hadithi ya Nimlaumu nani ambapo juma anapanga na madaktari wanaopima DNA ili kuweza kutambua kwamba mtu mimba ni ya kwake na sio ya Frank kwa hiyo tuendelee kusikiliza mpaka tutakapoona mimba itakuwa ya Frank au juma.
Soma Zaidi...USALITI (sehemu ya pili)
Post hii ni mwendelzo wa hadithi ya Usaliti kati ya Rhoda na Moses ambapo Moses anampenda sana Rhoda na wakati wa kuoa umefika ila akagikilia kwamba akimuoa Rhoda inawezekana wasipate watoto kwa sababu ya mimba ambazo Rhoda alikuwa anatoa mara kwa mara.
Soma Zaidi...