Nini maana ya ndoa katia uislamu na ni upi umuhimu wake
Hapa utajifunza maana ya ndoa kulingana na uislamu na umuhimu wake katika jamiii
Maana ya Ndoa
Ndoa, kwa ujumla, ni mkataba wa kuishi pamoja kati ya mume na mke kwa kufuata utaratibu uliowekwa na jamii. Kwa mfano, hapa Tanzania mume na mke watatambulika kuwa wameoana kisheria, pale watakapokuwa wamefunga mkataba wa kuishi pamoja mbele ya Mkuu wa wilaya au mbele ya walii na mashahidi wawili (ndoa ya kiislamu)au mbele ya Padri (Kanisani).
Ndoa ya Kiislamu ni mkataba wa hiari kati ya mume na mke wa kuishi pamoja kwa kuzingatia masharti na taratibu zilizowekwa na sheria ya Kiislamu. Ndoa yoyote iliyofungwa kinyume na masharti na taratibu za Kiislamu, haikubaliki kwa Waislamu.
Umuhimu wa Ndoa kwa Mtazamo wa Uislamu
Katika Uislamu ndoa ni jambo lililokokotezwa sana kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:
Katika Hadithi iliyopokelewa na Imamu Bukhari Mtume (s.a.w) amesisitiza kuwa ndoa ni katika sunnah yake na akaongeza kusema: "Yeyote anayekataa sunna yangu sipamoja nami ".
Anas (r.a) amesema kuwa Mtume wa Allah amesema, 'Mtu anapooa huwa amekamilisha nusu ya dini, kisha amche Allah ili akamilishe nusu iliyobakia." (Bukhari).
Ndoa inasisitizwa kutokana na umuhimu wake katika kuijenga na kuiendeleza jamii kwa:
(i)Kuihifadhi jamii na zinaa.
(ii)Kuendeleza kizazi kwa utaratibu mzuri.
(iii)Kujenga mapenzi na huruma katika familia.
(iv)Kukuza uhusiano na Udugu katika jamii.
(v)Kukilea kizazi katika maadili mema.
(vi)Kuwafanya watu wawajibike ipasavyo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 Bongolite - Game zone - Play free game 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Hadhi na Haki za Mwanamke katika jamii mbalimbali hapo zamani
Utangulizi:Uislamu unamuelekeza mwanaadamu namna nzuri ya kuendesha maisha yake katika kila kipengele cha maisha akiwa binafsi, katika familia na katika jamii.
Soma Zaidi...haki ya kutaliki: kuacha na kuachwa katika ndoa ya kiislamu
Haki ya KutalikiKatika jamii nyingi za kjahili haki ya kutoa talaka iko kwa mwanamume tu na mwanamke hana haki yoyote ya kumtaliki mumee.
Soma Zaidi...Nini kifanyike baada ya mazishi ya kiislamu
Huu ni utaratibu unaotakiwa kufanyika baada ya kuzika.
Soma Zaidi...