image

Nini maana ya protini

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya protini

NINI MAANA YA PROTINI

 

Protini ni chembechembe zinazotokea kwa njia ya asili (bila ya kutengenezwa) na zimetokana na asidi za amono (amino acid) zilizounganishwa kwa kutupia bondi za peptide. Neno protini asili yake ni lugha ya Kigiriki ”proteios” likiwa na maana ya kuwa ni kitu kinachopewa nafasi ya kwanza. Yaani protini ni viinilishe “nutrients” ambazo ni muhimu sana mwilini kuliko viinilishe vingine. Neno hili limeanzaka kutumiwa karne ya 19 mwaka 1838 na Mkemia kutoka Swedih Jöns Jacob Berzelius.

 

Protini huweza kutofautiana namna zilivyo kutoka kiumbe kimoja na chingine, pia protini huweza kutofautiana kutoka kiungo kimoja kwenda kingine. Kwa mfano protini za kwenye macho ni tofauti na zile za kwenye moyo, ini na figo. Kila kiumbe hai kina protini, na pia protini huhusika katika michakato tata kwenye miili ya viumbe hai, kwa mfano protini huhusika katika kutengeneza antibodies ambazo hutengeneza kinga na kupambana na maradhi na wadudu shambulizi kama bakteria na virusi. Protini hutengeneza enxymes ambazo ndizo hutumika katika kumeng’enya chakula. Pia protini hutengeneza homoni (hormones)

 

Baada ya kukila chakula chenye protini chakula kinaanza kumengenywa kinapofika kwenye tumbo na utumbo, kisha hufyonzwa kwenye utumbo mdogo na kuingia kwenye mirija ya damu. Pindi chembechembe za protini zinapoingia kwenye damu, damu huanza kusafirisha protini kwenda maeneo mbalimbali ya mwili yanayohitajia protini. Huko protini zitaingia kwenye seli za mwili. Ndani ya seli mchakato kwa kuvunjwa vunjwa protini ili kutumiwa zaidi hufanyika. Ndani ya seli mchakato huu jhufanyka kwenye sehemu inayotambulika kitaalamu kama ribosomes

 

Miili ya wanyama haina uwezo wa kuhifadhi protini kwa matumizi ya baadaye. Hivyo kama mtu atakula protini nyingi, mwili utaibadili protini kuwa fati na baadaye kutumika kutengeneza nishati ndani ya mwili. Na endapo mtu hataweza kupata protini za kutosha mwili utaanda kuangalia maeneo yenye protini ndingi kama misuli, kisha mwili utaanza kuvunja protini iliyomo mule na kuipeleka maeneo mengine na hapa mtua ataanza kukonda na kupoteza nyama na hatimaye kufariki kama hatapata chakula chenye protini.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2450


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Faida za vyakula vya asili
Posti hii inahusu zaidi faida za matumizi ya vyakula vya asili, kama tunavyojua kwamba mababu na mabibi zetu walitumia vyakula vya asili wakaishi miaka mingi kweli. Soma Zaidi...

Vinywaji vyakula salama kwa mwenye Presha ya kupanda
Je umesha wahi kujiuliza kuwa ni vinywaji vipi mwenye presha ya kupanda anafaha kutumia, Unadhani ni maji, mvinyo wa pombe, chai na kahawa. Bila shaka ungependa kujuwa zaidi kuhusu jambo hili. Makala hii ni kwa ajili yako Soma Zaidi...

magonjwa na lishe
DARASA LA AFYA MAGOJWA YANAYOHUSIANA NA VYAKULA 1. Soma Zaidi...

Fahamu vitamini K na kazi zake, vyakula vya vitamini k na athari za upungufu wake
kuhusu vitamini K, wapi tutavipata, ni zipi athari zake na ni zipi kazi zake mwilini. Soma Zaidi...

Faida za kula kunde, maharage, njegere, mbaazi na njugu mawe
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula kunde, maharage, njegere, mbaazi na njugu mawe Soma Zaidi...

JITIBU KWA TANGAIZI: faida za kiafya za tangaizi
Tangaizi ni katika mimea yenye asili na bara la asia hususan nchi ya China. Soma Zaidi...

Vyakula vya vitamini A na kazi zake
Soma Zaidi...

Vyakula vya protini na kazi zake
Soma Zaidi...

Faida za kula Nazi
Nazi ni katika matunda bora sana kiafya, Soma faida zake kwa afya yako Soma Zaidi...

UPUNGUFU WA VITAMIN NA MAJI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

ijuwe namna ya kufanya ihram na Vazi la ihram
Soma Zaidi...

Faida za tangawizi
Somo Hili linakwenda kukuletea faida za tangawizi Soma Zaidi...