image

Nje ya jumba la kifahari la aladini

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu

NJE YA JUMBA LA KIFAHARI JUMBA LA ALADINI

Mauwa yaliyojipanga vyema yalianza kukaribisha watu. Sambamba na mauwa haya yenye rangi za kijivu, nyeupe, nyekundu na njao iliyowiva vyema, kulikuwa pia na miti ya matunda iliyojipanga kwenye mistari miwili minyoofu, pembeni ya njia ya kuingilia. Ilinyoka vyema mistari kama ni kundi la askari wakiwa kwenye graride la kumpokea Kiongozi wa Nchi. Ilikuwa ni matunda ya machungwa, na mikomamanga iliyokuwa na rangi nzuri matunda yake. Wekundu wa mikomamanga na unjano wa machungwa utadhni ni madini yanayometameta yametundikwa juu ya miti hii. Haikuwa hivyo tuu pia yalipatikana baadhi ya matunda ya mwituni, kwa pamoja ilipatikaniwa mistari miwili ya miti ya matunda iliyoziba vyema kwenye njia. Pembbeni ilifatiliwa na miti midogo ya mauwa ya kupendaza.

 

Katikati ya njia hii ya kuingilia kumewekwa vijiwe vya kupendaza, zinatofautiana rangi zake. Hayakuwa ni mawe ya kawaida kwa uzuri wa rangi zake. Si dhahabu wala almasi. Ulifanana ukubwa wa vijiwe hivi kwenye rangi tofauti. Rangi ya dhambarau, kahawiya, kijani mpauko, buluu mpauko na njano ya kuwiva. Pia vilikuwepo vya rangi vyeusi iliyo na madoa meupe kama kunguru. Pia vipo vilivyochangan arangi kama mkia wa tausi wa mfalme wa China. Viriwe vilikuwa vilaini vyenye kuteleza miguuni. Kama utatembea peku utahisi mtekenyo kwa ulaini wa vijiwe hivyo. Havikuwa ni malumalu wala lulu. Hakika alipangilia vyema rangi mjenzi. Sauti nzuri ya kuvutia ilitoka baada ya kukanyaga vijiwe hivyo. Sauti ilitaka kufanana na sauti ya Kasuku wa Mfalme pindi anapokuwa anambembeleza binti Sultani alipokuwa mdogo.

 

Njia nzima iliweza kunukia harufu nzruri. Hukuhitaji pafyumu wala mafuta ya kunukia ukiwa kwenye Jumba hili. Yaani mauwa mazuri na matunda kwa pamoja yaliweza kunukisha vyema maeneo haya. Nyuki wa rangi ya dhahab walikuwa wakizunguka kwa ustadi, utadhani waliambiwa vile. Hawakuwa wenye kutisha yuki hawa. Walikuwepo pia buibui waliotanda vyema kwenye baadhi ya miti ya matunda. Buibui waliweza kutengeneza utando uliofana na na mauwa ya jasmini. Yaani kanakwamba walipangwa kuengeneza. Kila kilichoweza kuonekana kilikuwa na kuvutia zaidi. Aladini hauweza kuaini kila anachokiona kama ni uhalisia ama bado yupo kwenye ndoto ya maono.

 

Mbele ya Jumba la Aladini kulikuwa na uwanja mkubwa wa kuchezea na kupunzikia. Kichaka vidogo vodogo vya miti ya matunda vilivyotengeneza kivuli cha duara vilikuwa vikionekana. Viti vya kupendeza na kung’aa viliwekwa katika kila kichaka. Ndege aina ya tausi wenye mikia inayotaka kufanana na kanga walikuwa wakitembea kwenye uwanja kwa mwendo wa madaha. Hawakuwa tausi tu bali walikuwepo na vinyama vidogo kama sungura waliokuwa wakikimbizana kwenye uwanja huu. Ingelikuwa Aladini ni kama alivyokuwa zamani hapa angelitoka mbio kwenda kukamata sungura. Mazingira ya jumba hili yalikuwa safi sana. Sauti za ndege ziliweza kusikika kutoka katika vijichaka vidogo. Ndege walikuwa wakiimba nyimbo nzuri kwa kupekelezana. Haya yote aliyokuwa akiyaona binti Mfalme alikuwa anahisi yumbo ndotoni. Alikuwa akifikicha macho yake mara kwa mara kuthibitisha kama hayupo ndotoni

 

Aladini sasa ameanza kukaribishwa na ngazi za kuingilia ndani, ngazi iliyomfanya mtu kukanyaga barazani. Loo! Aladini hakuweza kuamini macho yake. Hakujuwa ni nini kulitandikwa pale kwenye balaza, maana hakikuwa ni kioo kwani palikuwa panabonyea kama godoro la Hariri lililotandikwa kwenye kiti cha mfalme. Kilichomshangaza Aladini ni kuwa palifanan sana na kioo, kwani ungeweza kujiona sura yako. Chini hapakuwa Alaini kama kioo wala mtelezo. Kuliweza kumpa uhuru mtembeaji. Baraza yote ilijawa na vitu vya kupendeza, ikiwemo viti vizuri, mauwa ya makopo yaliyopangiliwa kwa ustadi. Lakini kitu kizuri zaidi ni kasuku wawili waliokuwa wakipokezana kukaribisha wageni. Zilipendeza mno sauti na sura za kasuku hawa. Mambo yote haya hayakumshangaza Aladini tu bali watu wote waliofuatana nae waliwachwa midomo wazi.

 

Kuta za jumba la Aladini zilinyooka vyema na kuonyesha rangi iliyowekwa kwa ufasaha. Kuta zilijengwa kwa mawe yaliyopangiliwa vyema. Malumalu za kuvutia machoni ziliwekwa juu ya kuta hizo. Madirisha yalikuwa ni kama almazi iliyopakwa, yaani yaliweza kumeremeta sana. Hukuweza kumuona aliye ndani kupitia nje. Michirizi ya rangi za kuvutia ilipakwa pembeni ya madirisha. Zinafanana rangi hizi na dhahabu nyekundu, lakini haikuwa ni dhahabu. Vioo ngamba viliyosafi vilizidi kuboresha uzuri wa jumba hili. Taa za karabai mbili zilikuwa zimewekwa kwenye pembe mbili za kuta za jumba hili. Karabai zilizungukwa na matovu ya almasi na kutengeneza kitundu kizuri. Aladini alitamani usiku uingie aone uzuri wa mwangaza wa karabai hizo.

 

Aladini aliliendea dirisha bovu, dirisha ambalo halikuweza kumaliziwa. Akaanza kulishika kama vile fundi mbao anavyoshika mbao baada ya kuipiga msasa kuangalia kama msasa umekaa vyema. Binti mfalme mke wa Aladini naye akarudia kama alivyofanya mume wake kisha akasema “Mume wangu kipenzi, nyumba yetu nzuri sana, kasoro hapa tu…, ivi ni makosa tu, ama umekusudia” “….. hahaaa nimekusudia, na nina maana kufanya hivi” yalikuwa ni majibu ya Aladini. Madirisha yote yaliwekwa papi za dhahabu lakini dirisha hii halikuwa na papi hata moja yaani lilikuwa tupu kabisa. Dirisha hili lilikuwa limeelekea kwenye chumba cha stoo. Haikujulikana nini kipo humu ndani ila harufu nzuri ilikuwa ikitoka kwenye chumba hiko. Pia mwangaza mlaini wenye rangi tatu za kuchanganyika, nyeupe, njani na buluu, mwangaza ulitokea kwenye chumba hiko.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 838


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

HADITHI YA KAKA WA TANO WA KINYOZI
Soma Zaidi...

MSHENGA WA ALADINI MBELE YA MFALME
Soma Zaidi...

JARIBU LA PILI LA ALADINI
Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa nne wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi kaa wa tatu
Soma Zaidi...

Hadithi iliyosimuliwa na tabibu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Historia ya zamani
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Siri ya wageni wale
SIRI YA WAGENI WALE INAFICHUKA Tambua ewe kijana changu, mimi na baba yako tulikutana zamani sana. Soma Zaidi...

Hatma ya kinyozi maishani mwangu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

UJUMBE WA SIRI KWENYE KITABU CHA AJABU
Soma Zaidi...

Upendo uliotafsiriwa kwa michoro
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

NDANI YA JUMBA LA ALADINI
Soma Zaidi...