Ni kipi chanzo cha Elimu, na ni kwa namna gani Allah hufundisha Elimu kwa wanadamu?
Kama tunavyojifunza katika surat ‘Alaq (96:4-5), chanzo cha elimu au mkufunzi wa binadamu ni Allah (s.w). Allah (s.w) huwasiliana na binadamu na kuwaelimisha kwa kutumia mojawapo ya njia zifuatazo zilizoainishwa katika aya ifuatayo:
Na haikuwa kwa mtu kwamba Mwenyezi Mungu anasema naye ila kwa il-hamu (anayetiwa moyoni mwake) au kwa nyuma ya pazia au humtuma mjumbe (Malaika) naye humfunulia kiasi anachotaka kwa idhini yake (Allah), bila shaka yeye ndiye aliye juu mwenye hekima.” (42:51). Aya hii inatufahamisha kuwa binaadamu hupata habari kutoka kwa Allah (s.w) kwa njia tatu zifuatazo:
(a) Il-hamu(Intution).
(b) Nyuma ya pazia.
(c) Kutumwa Malaika na kufikisha ujumbe kama alivyotumwa. Pia katika Qur-an tunafahamishwa njia mbili nyingine anazozitumia Allah (s.w) katika kumfikishia binaadamu ujumbe kutoka kwake:
(d) Ndoto za kweli (ndoto za Mitume).
(e) Maandishi (mbao zilizoandikwa tayari).
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowNguzo za Imani (EDK form 2:. Dhana ya elimu ya uislamu
Soma Zaidi...Hii ni njia ambayo mwanaadamu huongeleshwa moja kwa moja na Allah (s.
Soma Zaidi...Faradhi kwa maiti ya muislamu (edk form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...