NJIA ANAZOTUMIA MWENYEZI MUNGU (S.W) KUWAFUNDISHA NA KUWASILIANA NA WANAADAMU


image


Njia ambazo Allah hutumia kuwasiliana na wanadamu nakuwafundisha elimu mbalimbali. (Edk form 1 dhana ya Elimu)


 

Njia anazotumia Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu ni:

1. Il-hamu.


-    Ni mtiririko wa habari (ujumbe) unaomjia mwanaadamu bila kufundishwa na mtu yeyote au kuona mfano wake katika mazingira yeyote.

2. Kuongea na Mwenyezi Mungu (s.w) nyuma ya pazia.


-    Ni njia mwanaadamu huongeleshwa na Mwenyezi Mungu (s.w) moja kwa moja kwa sauti ya kawaida bila kumuona.

-    Nabii Musa (a.s) ni miongoni mwa Mitume waliosemeshwa na Allah (s.w) nyuma ya pazia.

    Rejea Qur’an (28:30), (7:143) na (19:23-26).

3. Kutumwa Malaika na kufikisha ujumbe kama alivyotumwa.


-    Ni njia anayoitumia Allah (s.w) kumuelimisha mwanaadamu kwa kupeleka ujumbe kupitia mitume na watu wengine wema.

    Rejea Qur’an (53:1-12), (15:51-66), (19:16-19), (2:102) na (3:41).

4. Ndoto za kweli (ndoto za mitume).


-    Ni kupata ujumbe kupitia ndoto za kweli hasa kwa mitume ambayo huwa ni maagizo ya Allah (s.w) kwa Mitume.

-   Mfano ndoto ya Nabii Ibrahim (a.s) juu ya kumchinja mwanae Nabii Ismail (a.s).

    Rejea Qur’an (37:102), (12:4-5), (12:100) na (48:27).

5. Njia ya Maandishi (mbao zilizoandikwa).


-    Ni njia ya mawasiliano ya Allah (s.w) na waja wake kupitia maandishi yaliyoandikwa tayari.

-    Nabii Musa aliletewa ujumbe kwa maandishi kutoka kwa Allah (s.w).

    Rejea Qur’an (7:145) na (7:154).

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    2 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    3 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    4 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    6 Magonjwa na afya    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Mji wa Makkah na kabila la kiqureish
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Elimu Yenye Manufaa
Kwenye kipengele hiki tutajifunza elimu yenye manufaa kwenye jamii na pia tutajifunza sifa za elimu yenye manufaa. Soma Zaidi...

image Kukusanywa na kuhifadhiwa kwa quran
Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Tofauti kati ya hijjah na umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kuandaliwa kwa Muhammad kabla ya kupewa utume
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Maswali juu ya Mambo anayopaswa kufanyiwa maiti ya muislamu
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kusimamisha swala za faradh katika nyakati za dharura.
Kipengele hichi tutajifunza namna ya kusimamisha swala ukiwa safarini na vitani na nguzo zake. Soma Zaidi...

image Mafunzo yatokanayo na upinzani wa maquraish dhidi ya uislamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Sababu za Quran kuwa mwongozo sahihi wa maisha ya mwanadamu
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Mazingatio kabla ya kuosha maiti
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...