NJIA YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA VIRUSI VYA VYA UKIMWI NA ATHARI ZAKE

Posti hii inahusisha maambukizi ya virusi vya ukimwi .pia' tutangalia' njia za kujikinga na' ugonjwa wa UKIMWI

 

        NJia za kujikinga na ugonjwa wa ukimwi.

 1. Kulingana na  ilivyoelezwa apo mwanzo  kwamba  tutangalia njia za maambukizi ya virusi vya ukimwi.hivyo hivyo mtu mwenye virusi vya ukimwi au mtu yoyote hambaye hana ni marufuku kutotumia miswaki mmoja.
 2. Kuacha kabisa kufanya ngono umri mdogo chini ya miaka 18.pia ata hivyo kuna njia nyingi za maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.njia ya ngono ndo njia inayongoza kuwa na maambukizi mengi sana . Pia ukiangalia sahivi watu wanaoishi katika kundi ili wengi ni vijana walio na umri wa miaka hiyo .hivyo ukiacha ngono utakuwa umejiepusha na maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI kwa njia ya ngono.
 3. Kuepuka kishirikiana vifaa vyenye ncha kali kama  wembe, sindano ,mikasi ,na vifaa vya kutobolea masikio,pamoja na vifaa vya kunyolea nywele.
 4. Kuepuka kuchangia nguo za ndani na taulo.Nguo hizi zinaweza kusababisha maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI .
 5. Kutumia glavu unapokuwa unamuhudumia mgonjwa wa virusi kama atakuwa ametokwa na maji au damu
 6. Kuhakikisha kuwa wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi wanapata ushauri wa daktari
 7. Kuhakikisha kuwa wenye maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya ukimwi wanapata matibabu sahii.
 8. Mama mjamzito na mume wake kuhudhuria kiliniki mapema ili wachunguzwe kama wana maambukizi ya virusi vya ukimwi wakigundulika wapate tiba sahii .pia  mama lazima apate dawa ya kuzuia maambukizi kwa mtoto aliyetumboni mwake.

9.Mama mjamzito anashauriwa kujifungulia hospitalini ili kama mtoto ameathirika apate matibabu ya haraka iwezekanavyo.   

    

        Athari za maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.

 1. KUtokana na hivyo tulivyoeleza kuhusu maambukizi ya  mgonjwa anashauriwa kuwahi hospitalini ili kuangalia hali yake
 2. Athari nyingine unafhoofika kwa mwili na kupungua kwa kinga ya mwili .pia huweza kusababisha magonjwa nyemelezi na hatimaye kifo.
 3. Kuharisha mara kwa mara.hii ni mojawapo ya athari ya virusi vya ukimwi.mtu kuharisha inatokana na virusi vya ukimwi kuwa vina nguvu nyingi kwenye mwili.
 4. Kukosa nguvu na kuchoka
 5. Kupata magonjwa ya ngozi kama chunusi sugu na mabakamabaka.
 6. Kupata homa mara kwa mara

        7.kukohoa mara kwa mara.

 

                Kulingana hayo kuna mambo pia ya kuzingatia kwa mtu anayeishi na virusi vya ukimwi.

1.usafi.mtu anayeishi na virusi vya ukimwi na ukimwi anatakiwa kuzingatia usafi wa mwili,nguo na mazingira yanayomzunguka.Anatakiwa kuoza na kuvaaa nguo safi.mgonjwa wa UKIMWI anaweza kushindwa kufanya usafi binafsi na sehemu za kulala.hivyo ni muhimu kumsaidia kufanya usafi wa mwili kama vile kukata kucha ,nywele na kumwogesha .nguo za kuvaaa zinapaswa kuwa safi mda wowote .pia ni muhimu kumfulia nguo zake za kuvaaa na matandikio .Ni vizuri kuchukua tahadhari wakati wa kumhudumia mgonjwa ili kuepuka kuambukizwa virusi.

 

2.lishe bora,.tumeangalia apo mwanzo kwamba virusi vya ukimwi husababisha kupungua kwa kinga mwilini.lishe bora huongeza kinga ya mwili .watu wanaoishi na virusi vya ukimwi huitaji lishe bora ili kiongozi kinga ya mwilini.

 

3.usalama wa lishe,.watu wanaoishi na virusi vya ukimwi wako katika hatari ya kuambukizwa maradhi mengine kwa urahisi .hii inatokana na kupungua kwa kinga mwilini.chakula kinaweza kuwa miongoni mwa chanzo cha maambukizi ya virusi vya ukimwi kama hakitandaliwa kwa kuzingatia usafi.ili chakula kiwe safi na salama ni muhimu kuzingatia usafi wa mara kwa mara wakati wa kuandaa chakula.unatakiwa uzumie vyombo safi wakati wa kuandaa kula chakula vyombo vinatakiwa kuishiwa vizuri kwa sabuni na maji safi na salama.vyombo lazima vianikwe au vipanguswe na kitambaa safi. 

   

Mtu anayeishi na virusi vya ukimwi anapaswa kula mlo kamili kila siku.chakula kinatakiwa kiwe safi na salama .chakula kifunikwe kwa kutumia mfuniko safi ili kuzuia vumbi na wadudu.mtu anayeishi na virusi vya ukimwi anatakiwa kula chakula cha moto .matunda na mboga mboga hasa zile zinazoliwa bila kupikwa zioshwe kwa maji safi na salama.

 

Pia mtu anayeishi na virusi vya ukimwi anatakiwa kuepuka vyakula viliyosindikwa .vyakula hivi mara nyingi husindikwa kwa kemikali ambazo zinaweza kuleta madhara kwa mgonjwa.vilevile ,haishauriwi kula chakula kilichokaa zaidi ya saa mbili bahada ya kupikwa kinatakiwa kipashwe moto mpaka kichemke kabla ya kula.

Kama ilivyo kwa watu wengine ,mtu anayeishi na virusi anatakiwa kunywa maji safi na salama ,maji ya kunywa yatunzwe katika chombo safi chenye mfuniko na kuweka mahali safi.

 

 

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/08/06/Saturday - 07:50:51 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2717


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Dalili za Kufunga kwa ulimi (tongue tie)
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za Kufunga kwa ulimi (Tongue-tie) kuanzia Mtoto anavyo zalia mpaka navyokua ni hali inayotokea wakati wa kuzaliwa ambayo kitaalamu hujulikana kama ankyloglossia. Soma Zaidi...

Nini kinasababisha kizunguzungu?
Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili za kizunguzungu zinazotekea katika mwili wa binadamu Soma Zaidi...

Je inakuaje kama umempiga denda mtu mweny ukimwi ambaye anatumia daw za ARVs na una michubuko midogo mdomon ya kuungua na chai
Bila shaka umeshawahi kujiuliza kuwa je mate yanaambukiza HIV ama laa. Na kama hayaambukizi ni kwa sababu gani. Sio mate tu pia kuhusu jasho kama pia linaweza kuambukiza ukimwi ama HIV. Wapo pia wanajiuliza kuhusu mkojo kama unaweza kuambukizwa HIV. Kar Soma Zaidi...

Je unazijuwa dalili za Ukimwi na HIV?
Huwenda ukawa ni moja kati ya watu wanaotaka kujuwa juu ya dalili za ukimwi. Kama wewe ni katika watu hawa tambuwa kuwa kuna dalili za VVU (hiv) na dalili za ukimwi. Makala hii itakwenda kukuletea dalili kuu za mwanzo za VVU na HIV kuanzia wiki tatu za mw Soma Zaidi...

Halow samahan dokta nmekuwa nikiumwa tumbo muda mwingi takriban wiki ya 3 halipon naharisha kuna muda nikila chakula hata kama kdogo tu maumivu makali,je nifanyaje msaada
Mvurugiko katika mfumo wa chakula mwilinivunaweza kusababisha maumivu ya tumbo, kuharisha, kutapika na kuchoka pia. Lakini zipo sababu nyingine kama kuwana ujauzito. Nini ufanye endapo unasumbuliwana hali hii Soma Zaidi...

Ujuwe ugonjwa wa ebola, dalili zake na jinsi unavyoweza kusambazwa.
Posti hii inahusu sana kuhusu ugonjwa wa ebora. Ugonjwa huu usababishwa na virusi.Virusi hivyo husababisha kutokwa na damu nyingi mwilini kutokana na kupasuka kwa mishipa ya damu Soma Zaidi...

Typhoid husabisha mwili kuchoka na maumivu ya kichwa pamoja na joint za miguu kuchoka
Dalili za typhid zinapasa kuangaliwa kwa umakini. Bila vipimo mtu asitumie dawa za tyohod, kwanu dalili za tyohid hufanana na daliki za maradhi mengi. Soma Zaidi...

Undetectable viral load ni nini?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya undetectable viral load Soma Zaidi...

Dalili za saratani ya mapafu
Saratani ya Mapafu ni aina ya Kansa inayoanzia kwenye mapafu. Mapafu yako ni viungo viwili vya sponji kwenye kifua chako ambavyo huchukua oksijeni unapovuta na kutoa kaboni dioksidi unapotoa nje. Soma Zaidi...

Dalili za kuaribika kwa mfumo wa kupeleka taarifa kwenye ubongo
Posti hii inahusu zaidi Dalili zinazoweza kujitokeza baada ya sehemu ya kupeleka taarifa kwenye ubongo imearibika, kwa hiyo mambo yafuatayo yakijitokeza utajua wazi kuwa kuna matatizo kwenye mfumo wa kupeleka taarifa kwenye ubongo. Soma Zaidi...

Mbinu za kuzuia na kuepukana na maradhi ya uti wa mgongo
Posti hii inahusu zaidi njia au mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuepukana na tatizo la ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo. Soma Zaidi...

Dalilili za homa ya matumbo (typhoid fever)
Post hii Ina onyesha DALILI za Homa ya matumbo (typhoid fever) huenea kupitia chakula na maji machafu au kwa kuwasiliana kwa karibu na mtu aliyeambukizwa. Dalili na ishara kwa kawaida hujumuisha Homa kali, maumivu ya kichwa, maumi Soma Zaidi...