Njia za jumla za kujikinga na magonjwa mbalimbali

Njia za jumla za kujikinga na magonjwa mbalimbali

Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kujikinga na magonjwa, kwa kawaida tunajua wazi kuwa magonjwa yapo na yanasambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na mengine hayasambai yanaweza kumpata mtu mmoja akapona au magonjwa mengine si ya kupona

Njia za kujikinga na magonjwa.

1. Njia ya kwanza ni kufanya usafi wa mazingira,kufanya usafi wa binafsi yaani kuoga, kufua nguo, kukata kucha, kusafisha meno, kunywa maji safi na salama na mambo hayo ya kuhakikisha mwili unakaa kwenye hali ya usafi kwa kufanya hivyo ni vigumu kupata magonjwa,na pia kwa upande wa mazingira, kukata nyasi zilizozunguka makazi , kumchoma takataka,kutunza uchafu sehemu Moja na kutoruhusu kuishi sehemu Moja na wanyama, yaani kuwatengea wanyama sehemu yao kwa kufanya hivyo ni vigumu kupata magonjwa.

 

 

2. Kupata kinga ya mwili.

Kwa upande wa kupata kinga ya mwili ni pamoja na kupata chanjo zote zinazohitajika mwilini hasa hasa kwa watoto kwa kufanya hivyo tunazuia magonjwa ambayo yanaweza kutokea hapo mbeleni,kwa mfano kupata chanjo ya kifua kikuuu, kupata chanjo ya kuzuia kupooza, kupata chanjo ya kuzuia kuharisha kupata chanjo ya pepo punda na chanjo zote za lazima kwa mtoto na kwa mabinti wanaotegemea kubeba mimba kupata chanjo zinazohitajika Ili kuepuka magonjwa mbeleni. Kwa kuweka mwili katika hali ya kinga ni vigumu kupata magonjwa.

 

 

3. Kula mlo kamili.

Kuna msemo usemao kwamba chakula Bora ni dawa, kwa sababu mlo ukiwa kamili na kutosha ni vigumu sana kupata magonjwa, kwa mfano aina zote za vyakula zikiwa sawia ni vigumu kupata magonjwa kwa mfano matumizi mazuri ya vyakula vya wanga, protein, mafuta kidogo na mboga za majani za kutosha na kunywa maji kulingana na uzito wako kwa kufanya hivyo ni vigumu kupata magonjwa, lakini Kuna tabia ambayo watu wanapendelea aina Moja ya vyakula hasa vyakula vya madukani vilivyojaa kemikali na mafuta kwa wingi sukari wakitegemea kupata afya njema kwa kufanya hivyo matokeo yake ni kinenepeana na kuwa na vitambi hatimaye magonjwa ya presha na mengine mengi tu. Kwa hiyo kula mlo kamili ni kujikinga na magonjwa.

 

 

4. Kuangalia afya Yako mara kwa mara.

Kitendo cha kuangalia afya mara kwa mara nayo ni hatua Moja kubwa kwa sababu unaweza kukuta Kuna ugonjwa upo na ujautibu au kwa wakati mwingine ukikutwa na presha labda inaelekea kuwa juu unarekebisha mtindo wa maisha au ukikuta sukari ni kubwa unapunguza kiwango cha sukari kwa kufanya hivyo ni vizuri kabisa kuepuka na magonjwa au kwa vijana ni vizuri kabisa kupima maambukizi na magonjwa ya zinaa ikitokea kuna ugonjwa ni kuanza dawa mapema Ili kuweza kuepukana na matatizo mbalimbali ambayo ni pamoja na ugumba kama Kuna zinnia Kali au kuepuka kinga ya mwili kushuka kama Kuna maambukizi ya virus vya ukimwi.

 

 

5. Elimu kutolewa kila mara.

Kwa kupitia watu mbalimbali kwa lengo la kutoa elimu ni jambo zuri na la busara kwa sababu pengine Kuna mlipuko Fulani wa magonjwa jamii ikijulishwa mapema na kuweza kujikinga na kufuata mashart au tiba kama ipo ni vigumu kupata magonjwa kwa hiyo viongozi wa jamii wawe tayari kutoa elimu kwa waliowazunguka Ili kuzuia kuongezeka kwa magonjwa.

 

 

6. Kutibu magonjwa kama yapo.

Njia nyingine ya kupunguza magonjwa ni pamoja na tiba kama Kuna ugonjwa Fulani kwenye jamii ni vizuri kutibu ugonjwa huo Ili kuepuka kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa sababu Kuna watu wenye kinga ya hali ya juu ana ugonjwa ila haoneshi dalili ni vizuri kutoa ushauri na kuhakikisha kuwa ugonjwa unatibika kwa watu wenye hali ya hivyo.

 

 

7. Kutumia dawa endapo Kuna maambukizi.

Ni vizuri kabisa na jambo zuri kutumia dawa ikiwa umefanya vipimo na kugundulika una maambukizi kwa mfano watu wenye maambukizi ya virus vya ukimwi ni vizuri kabisa kutumia dawa na wasione aibu kabisa kwa sababu wasipotumia dawa wanaweza kuwa na magonjwa nyemelezi yanayosababisha afya zao kuyumba.

 

 

8. Kwa hiyo kuzuia kupatwa na magonjwa ni kazi inayoweza kufanikiwa zaidi kwa kuhakikisha mazalia ya wadudu wanaosambaza magonjwa kuharibiwa kwa mfano kujaribu mazalia ya mbu, nzi na wadudu wote ambao tnajua kazi zao ni kusambaza magonjwa tunaweza kutumia njia zozote pamoja na kutumia dawa za madukani za kuua wadudu.

 

 

9. Kwa hiyo kwa kufanya hayo yaliyojadiliwa magonjwa yanaweza kupungua au yasiwepo kabisa kwa sababu magonjwa yanakuwepo kwenye jamii kwa sababu ya kutozingatia tuliyoyajadili ambayo ni kutokula mlo kamili, tabia ya kutoangalia afya zetu, kushindwa kutumia dawa baada ya vipimo,kutofanya usafi kwenye mazingira yetu,kuishi na wadudu wanaosababisha ugonjwa na mambo mengine kama hayo, kwa hiyo ni vizuri kabisa kuziangatia hayo Ili tuwe mbali na magonjwa.

 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views: 2762

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 web hosting     👉6 ai web app    

Post zinazofanana:

vidonda vya tumbo

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...
NJIA YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA VIRUSI VYA VYA UKIMWI NA ATHARI ZAKE

Posti hii inahusisha maambukizi ya virusi vya ukimwi .pia  tutangalia  njia za kujikinga na  ugonjwa wa UKIMWI

Soma Zaidi...
Dawa za kutibu fangasi sugu za ukeni (Vaginal Candidiasis).

Fangasi wa ukeni (Vaginal Candidiasis) husababishwa na kuzaliana kupita kiasi kwa fangasi aina ya Candida. Ingawa mara nyingi hutibika kwa dozi moja, baadhi ya wanawake hukumbwa na fangasi sugu (recurrent candidiasis)—hali inayojitokeza mara nne au zaidi kwa mwaka. Hii si hali ya kawaida na inahitaji mbinu madhubuti za kitabibu badala ya kutegemea dawa za dukani pekee. Makala haya yanakupa mwongozo wa tiba na hatua za kudumu za kuondoa kero hii.

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu Ugonjwa wa ukoma

Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa ukoma, ni Ugonjwa unaosababishwa na mdudu anayeitwa mycobacterium leprae, mdudu huyu kwa kawaida uathiri sana sehemu za ngozi na sehemu za Neva mbalimbali za mwili

Soma Zaidi...
Chakula kinachosaidia kupunguza gesi tumboni.

​Gesi tumboni (bloating au flatulence) ni tatizo la kawaida linaloweza kusababisha usumbufu mkubwa na kupoteza kujiamini. Makala haya yanachunguza kwa kina vyakula bora vinavyosaidia kupunguza uzalishaji wa gesi, kuelezea sayansi nyuma ya usagaji chakula, na kutoa mikakati ya lishe kwa maisha yenye afya na utulivu wa tumbo.

Soma Zaidi...
​Dalili za UKIMWI Huchukua Muda Gani Kuonekana?

Watu wengi hujiuliza ni muda gani huchukua kwa mtu aliyeambukizwa virusi vya HIV kuanza kuonyesha dalili za UKIMWI. Makala hii inafafanua hatua tatu za maambukizi ya HIV, muda unaochukua kwa dalili kujitokeza, na kwa nini kupima ndiyo njia pekee ya uhakika ya kujua afya yako.

Soma Zaidi...