image

Njia za kujitwaharisha, na vitu vinavyotumika kujitwaharisha

Post hii inakwenda kukufundisha njia zinazotumika kujitwaharisha.

Chakujitwah aris hia

Nafsi ya mtu hutwaharika kwa mtu huyo kumuamini Allah (s.w) ipasavyo na kufuata mwongozo wake katika kukiendea kila kipengele cha maisha yake ya kibinafsi na kijamii.
Muislamu atatwaharika kutokana na Najisi na Hadath kwa kutumia maji safi au udongo safi kwa kufuata masharti na maelekezo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

 

Sifa za Maji Safi
Maji safi kwa mtazamo wa twahara ni yale yanayofaa kujitwaharishia yaliyogawanyika katika makundi yafuatayo:

(a)Maji Mutlak (maji asili)
Maji yoyote katika hali yake ya asili ni maji safi yanayofaa kujitwaharishia. Maji asili (natural water) ni maji ya mvua, chem chem, visima, mito, maziwa na maji ya bahari.

 


(b)Maji mengi:

Maji mengi ni maji yaliyokusanywa au yaliyokusanyika pamoja na kuwa na ujazo wa mabirika (qullatain) au ujazo usiopungua madebe 12. Mfano wa maji mengi yaliyokusanywa ni maji ya mapipa yenye ujazo wa lita 240, maji ya mabirika (matangi) maalum yaliyojengwa kuhifadhia maji msikitini na nyumbani. Mfano wa maji mengi yaliyojikusanya ni yale ya madimbwi makubwa yanayojikusanya wakati wa mvua.

 


Maji mengi hayahabiriki upesi. Hayaharibiki kwa kujitwaharishia ndani ya chombo kilichoyakusanya au ndani ya mkusanyiko huo wa maji. Pia maji mengi hayaharibiki kwa kuingiwa na najisi. Bali maji mengi yatakuwa hayafai kujitwaharishia iwapo yatabadilika asili yake katika rangi au utamu (ladha) au harufu.

 


(c)Maji machache:

Maji machache ni yale yaliyokusanywa katika chombo au yaliyojikusanya katika ardhi yakiwa na ujazo chini ya Qullatain* au chini ya ujazo wa pipa lenye ujazo wa madebe 12 au chini ya ujazo wa lita 224. Mfano wa maji machache ni ya ndoo, maji ya mtungi na maji yaliyojikusanya kwenye vidimbwi vidogo vidogo wakati wa mvua.

 


Maji machache hayatafaa kujitwaharishia iwapo

 


(i)yataingiwa na najisi japo kidogo sana.
(ii)Iwapo yatakuwa yametumika katika kujitwaharishia humo humo kwa kuondoa najisi au Hadath.
(iii)Iwapo yatakuwa yametumika kwa kufulia au kuoshea vyombo au kuogea humo humo.
(iv)Iwapo yataingiwa na kitu kikayabadilisha asili yake katika rangi, harufu au tamu(ladha).

 


Kutokana na haya tunajifunza kuwa, tunapokuwa na maji machache hatuna budi kuwa waangalifu wakati wa kuyatumia ili tusiyaharibu. Tusijitwaharishe ndani ya vyombo vilivyohifadhia maji hayo, bali tuyateke na kujitwaharisha mbali nayo. Kwa mfano tunakoga kwa kutumia kata na tunatawadha kwa kutumia kopo au birika.

 


(d)Maji makombo

Maji makombo ni maji yaliyonywewa na binaadamu au mnyama yakabakishwa.Maji makombo yanafaa kujitwaharishia ila yale yaliyonywewa na kubakishwa na mbwa au nguruwe.


 

Udongo safi

Udongo safi ni ule ulioepukana na najisi na ukabakia katika asili yake na kutochanganyika na kitu kama vile unga, majivu au vumbi la mkaa, vumbi la mbao (saw dust) n.k. kwa kawaida udongo wote katika ardhi ni safi.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 868


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Ni mali ipi inatakiwa kutolewa zaka?
Soma Zaidi...

Zijuwe funga za sunnah na jinsi ya kuzifunga
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu funga za sunnah na jinsi ya kuzigunga. Soma Zaidi...

Watu wanaolazimika kufunga mwezi wa Ramadhani
Hapa utajifunza watu ambao wanalazimika kufunga mwezi wa Ramadhani. Soma Zaidi...

Kwanini funga imefaradhishwa mwezi wa ramadhani
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Jinsi ya kutoa zakat al fitiri na umuhimu wa zakat al fitri kwa waislamu
Hapa utajifunza kuhusu zakat al fitiri, kiwango chake, watu wanaostahili kupewa na kutoa, pia umuhimu wake katika jamii. Soma Zaidi...

Hali ya kuzuiliana kurithi katika uislamu
KuzuilianaTumeona kuwa wanaume wenye kurithi ni 15 na wanawake wanaorithi ni 10. Soma Zaidi...

Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za Kirumi hapo zamani
(b) WarumiJamii ya Warumi nayo ni miongoni mwa jamii zinazohesabika kuwa zilianza kustaarabika mapema katika historia ya ulimwengu. Soma Zaidi...

Msisitizo juu ya kutoa zaka na sadaka
Soma Zaidi...

Nini maana ya kusimamisha swala
Post hii inakwenda kukufundisha maana ya kusimamisha swala kama inavyotumika kisheria. Soma Zaidi...

Namna ya kujitwaharisha Najisi ndogo
Soma Zaidi...

Ufumbuzi wa tatizo la riba.
Uislamu ndio dini pekee ambayo inatoa ufumbuzi juu ya suala la riba. Soma Zaidi...

Maana ya mirathi katika uislamu
Post hii itakufundishabkuhusu mirathi ya kiislamu, maana yake. Soma Zaidi...