image

Njia za kukabiliana na presha ya kupanda/hypertension

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kukabiliana na presha ya kupanda

NJIA ZA KUKABILIANA NA PRESHA YA KUPANDA (HYPERTENSION)

1.Fanya mazoezi ya mwili na viungo walau kila siku kwa dakika kama 30 mpaka 60. si lazima uwe unakimbia ama mazoezi magumu ya kutoa jasho, hapana unaweza hata kuamua kutembea kwa miguu kwa mwendo mrefu kwa lisaa limoja na ikawa ni mazoezi tosha.

2.Kula vyakula vilivyo bora kwa afya, ambavyo vinasaidia kupunguza ama kuzuia presha. Kitaalamu mlo huu huitwa DASH yaani Diet Aproaches to Stop Hypertension. Vyakula hivi ni kama:

A.Matunda

B.Mboga za majani

C.Nafaka nzima

D.Samaki, karanga na korosho

E.Wacha kula vyakula vyenye mafuta mengi

3.Punguza ulaji wa chumvi sana. Kuzidi kwa ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi kunaweza kusababisha presha ya kupanda. Kitaalamu ni kuwa ukila chumvi sana mwili unahitaji kupata maji mengi na hali hii itapelekea presha.

4.Punguza uzito uliozidi mwilini. Rafiki mkubwa wa presha ni kuzidi kwa uzito. Na tambuwa kuwa uzito wa mwili unatakiwa uendane na urefu wa mtu na si umri ama unene alio nao. hivyo tambua. Ili kuhakikisha kama uzito wako upo sawa unaeza kujipimia kiuno chako. Kikawaida wanaume wnatakiwa viuno vyao visizidi nchi 40 na wanawake viuno vyao visizidi nchi 35.

5.Punguza matumizi ya sigara ama wacha kabisa. Ndani ya sigara kuna kemikali za nicotine na nyinginezo. Nicotine ni rafiki sana na presha ya kupanda.

6.Punguza unywaji wa pombe ama wacha kabisa. Unywaji wa pombe sio hatari tu wa afya ya moyo lakini pia unaweza kuleta shida nyingine za kiafya kama saratani. Hakikisha kama ni mnywaji unapunguza unywaji ama unawacha kabisa itakuwa ni bora kwako.

7.Hakikisha huna misongo ya mawazo. Misongo ya mawazo inaweza kuwa ni adui mkubwa wa afya ya ubongo. Ni vyema kusamehe wanaokukosea na kuomba msamaha unapo kosea hali zote hizi mbili zitakusaidia kupunguza misongo ya mawazo. Jichanganye na watu na pemba kuwa mbali na fujo.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1145


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Umuhimu wa pua kama mojawapo ya mlango wa fahamu
Post hii inahusu zaidi umuhimu wa pua kama mojawapo ya mlango wa fahamu.pua ni mlango wa fahamu ambao uhusika na kupumua. Soma Zaidi...

Huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi
Posti hii inahusu zaidi huduma ambazo wagonjwa wanaoishi na maambukizi ya virus vya ukimwi wanaweza kupata, huduma hii utolewa hasa kwa wale ambao wamejitokeza kupima afya zao na kujua wazi hali zao na kwa wale wanaofatilia huduma hii wanaweza kuishi vizu Soma Zaidi...

Vifaa vya kutumia wakati wa kusafisha vidonda.
Posti hii inahusu zaidi vifaa vya kutumia wakati wa kusafisha vidonda, ni vifaa muhimu ambavyo mara nyingi kutwa hospitalini. Soma Zaidi...

Nini husababisha kibofu cha mkojo kuuma na baadae kutoka damu
Katika post hii utajifunza sababu zinazowezabkuorlekea kibofu kuuma upande mmoja Soma Zaidi...

Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyezimia
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyezimia Soma Zaidi...

Njia za kupunguza uzito na kitambi
Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kupunguza tatizo la kuwepo kwa uzito mkubwa pamoja na kitambi Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ANAYETOKWA NA DAMU YA PUA
Kama mtu anatokwa na damu za pua, basi juwa kuwa anahitaji huduma ya kwanza. Soma Zaidi...

Huduma ya Kwanza kwa aliyepatwa na presha ya kupanda
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na presha ya kupanda Soma Zaidi...

Ajali ya jicho
Post hii inahusu zaidi ajali ya jicho na visababishi vyake, ajali ya jicho ni pale jicho linavyoingiliwa na uchafu na vitu vingine ambavyo havistahili kuwa kwenye jicho Soma Zaidi...

Njia za kujikinga na UTI
Somo hili linakwenda kukuletea njia za kujikinga na UTI Soma Zaidi...

Maana ya afya
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya afya Soma Zaidi...

Huduma ya Kwanza kwa mwenye kizunguzungu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu mwenye kizunguzungu Soma Zaidi...