Zifuatazo ni njia nyingi za kumjua Mwenyezi Mungu (EDK form 2:dhana ya elimu katika uislamu)
NJIA ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU (S.W).
Njia za Kumtambua Mwenyezi Mungu (s.w).
Nafasi ya Fitrah (maumbile).
- Kila Mwanaadamu amepandikizwa hisia za kimaumbile zinazomtambua Mungu kupitia ujuzi wa kutambua mema na maovu.
- Mwanaadamu akipatwa na raha au misukosuko na huzuni hukiri uwepo wa Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Quran (17:67), (30:30) na (91:7-8).
Vipaji vya Binaadamu.
- Vipaji vya akili na milango ya fahamu na fani zingine za elimu ni nyenzo pekee zikitumiwa vilivyo humuwezesha mtu kumjua Mola wake.
Rejea Quran (3:190-191), (35:28).
Nafsi ya mwanaadamu.
- Mfumo mzima wa mwili wa mwanaadamu na utendaji wake wa kazi wa ajabu wa viunge mbali mbali vya mwili kama kuyeyusha chakula tumboni, msukumo wa damu mwilini, n.k. ni ishara tosha juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Quran (51:20-21)
Mazingira.
- Utegemezi na uhusiano wa kimahitaji ya kutumia rasilimali ya kuishi kati ya mimea, wanyama na binaadamu (ecological balance).
- Maumbile mengine kama mbingu, ardhi na yote yanayoonekana na yasiyooneka katika mazingira yanayotunguka.
Rejea Quran (3:190).
Wahyi (Ufunuo).
- Wahyi ndio nyenzo kuu ya kumwezesha mwanaadamu kumtambua Mwenyezi Mungu (s.w) kwa usahihi unaotakikana.
- Elimu, vipaji na ujuzi au sayansi pekee haviwezi kumwezesha mwanaadamu kumtambua Mungu kwa baadhi ya maeneo, mfano nguzo za imani, n.k.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Elimu inaweza kugawanyika katika makundibmrngine mawili ambayo ni elimu yenye manufaa na elimubisiyi na manufaa
Soma Zaidi...Nguzo za Imani (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Allah anatutaka kuchunguza umbile na mbingu na ardhi ili kupata mazingatio.
Soma Zaidi...Mahusiano kati ya elimu ya mwongizo na elimu ya mazingira katika uislamu.
Soma Zaidi...Je ni kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila ya kuwa na dini?. Vipawa alivyopewa na Allahni jibu tosha juu ya swali jilo
Soma Zaidi...Huwaoni wale wanaodai kwamba wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako?
Soma Zaidi...