Njia za kumsafisha Mama aliyetoa mimba.

Post hii inahusu njia safi za kumsafisha Mama ambaye ametoa mimba au mtoto amefia tumboni.

Njia  za kumsafisha Mama ambaye ametoa mimba au mtoto amefia tumboni.

1. Kama tulivyoona hapo mwanzoni kwamba njia hii utumika kumsafisha Mama kwa kutumia vyuma kawaida mimba ikiwa chini ya miezi minne au wiki kumi na mbili njia hii I aweza kutumika na pia wanaopaswa kuitumia ni wataalamu wa afya sio wake wanaotoa mimba ki magendo ni dhambi kwa Mungu na taifa pia .

 

2. Kwanza kabisa unapaswa kuandaa vifaa muhimu ambavyo vitaweza kutumika na pia viwe vimepitishwa kwenye usafishwaji wajoto la hali ya juu Ili kuweza kuondoa wadudu ambao wanaweza kuleta madhara baada ya kumsafisha vifaa hivi vinapaswa kutumiwa na wataalamu wa afya tu na sio wale wanaotoa mimba kinyume na utaratibu wa sheria za serikali na ki maadili.

 

3. Pia mwelezee mama kitu kinachopaswa kufanyika kama ni kumsafisha kwa sababu ya mimba inayotaka kutoka au ni kwa sababu ya kutoa mtoto aliyefia tumboni, pia mama naye anapaswa kukupatia ruhusa ya kufanya hivyo na pia familia inapaswa kuelezea kila kitu kinachoendelea na kuweza kushirikiana nawe kwenye kazi hiyo.na pia pakitokea shida yoyote unapaswa kuwaeleza familia na ndugu wa mama na mama mwenyewe.

 

4. Kabla ya kuanza kazi unapaswa kufunua sehemu muhimu ambazo unapaswa kufanyia kazi sio kumfunua mama mzima  hapo unakuwa umekosea maadili ya kazi, pia mama anapaswa kufunikwa vizuri na vitambaa maalum ambavyo kwa kitaalamu huitwa drape, hivi vitambaa Vimo kila kituo cha afya na pia kwenye hospitali kubwa vipo kabisa.pia wakati wa kazi ikitokea vikachafuka ni vizuri kabisa kuviweka sehemu maalumu na kuweza kumwekea mama vitambaa vingine na kazi inaendelea.

 

 

5. Hakikisha kwamba vifaa vyako ambayo unataka kuviweka kwenye uke ili kuweza kutoa kichanga unaviweka vizuri ili kuweza kuepukana na uharibifu kwenye sehemu mbalimbali za via vya uzazi, hakikisha unaviweka sawa pia wakati wa kutoa mimba iliyoharibika ni vizuri kumpiga mama sindano ya ganzi kwa sababu maumivu ni makubwa mno, kwa hiyo namna ya kuweka vifaa inapaswa kuwa sawa ili kuweza kuepukana na uharibifu wowote wa via vya uzazi.

 

 

6. Pia unapaswa kusafisha sehemu zote za via vya uzazi kuanzia kwenye sehemu za uke zote kwa kuua bakteria ambao wakiingia ndani wanaweza kuingiza maambukizi, pia na msafishaji anapaswa kuwa makini kwa kuvaa sterile gloves ambazo zinazuia kuingiza uchafu kwenye mwili wa mama na kuzuia magonjwa ambayo yanaweza kutoka kwa mama kwenda kwa mtoa huduma, magonjwa sugu ambayo yanaweza kusambaa ni homa ya nini pamoja na maambukizi ya Ukimwi.

 

 

7. Baada ya kusafisha na kuweka vyuma kwenye sehemu husika unapaswa kuvuta uchafu wote kutoka kwa Mama na hakikisha uchafu wote unaisha kabisa na kuhakikisha na damu yote inaisha na pia kama mama ana maumivu unapaswa kumpatia dawa ya maumivu ili aweze kutulia.

 

 

8. Baada ya hapo unapaswa kumshauri Mama na kumwambia mda mzuri wa kubeba mimba ili kuweza kuepukana na matatizo ya mimba kutoka mara kwa mara na kama mimba imetoka zaidi ya mara moja ni vizuri kabisa kutafuta sababu ya kutoka kwa mimba.

 

 

9. Pia ndugu jamaa na marafiki wote wanapaswa kuwa pamoja na mama ili kuweza kumtunza mama katika kipindi chote mpaka atakapofikia wakati wa kubeba mimba nyingine, na pia jamii inapaswa kuacha mila mbaya na desturi za kuona kwamba kutoa mimba ni mkosi kwa jamii.

 

 

10. Kwa hiyo mama baada ya kutoka kwa mimba anapaswa kwenda hospitali ikiwa amepata shida yoyote ya kiafya hata kama hana mtoto kwa sababu changamoto anazozipata Mama baada ya kujifungua na aliyetoa mimba anaweza kupata hizo hizo.

 

 

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/11/13/Sunday - 10:07:52 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1014

Post zifazofanana:-

Mwenendo wa mwenye kunuia hijjah na umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Hadithi ya tabibu wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Namna ya kumlisha Mgonjwa ambaye hawezi kujilisha mwenyewe ni
Posti hii inahusu njia za kumlisha Mgonjwa ambaye hawezi kujilisha wenyewe, hali hii uwa inawapata wagonjwa wale ambao hawawezi kujilisha wenyewe tunaweza kuwalisha kwa njia zifuatazo. Soma Zaidi...

Niharisha siku ya pili baada ya tendo. Jana hadi leo sijapata choo inawezakua nimeshika ujauzito?
Hivi unadhani kuharisha ni katika dalili za mimba, vipi kuhusu kutopata choo pia inaweza kuwa ni ujauzito? Soma Zaidi...

Dawa ya chango na maumivu ya hedhi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa ya chango na dawa ya maumivu ya hedhi Soma Zaidi...

Mabadiliko kwa wavulana wakati wa kubarehe
Post hii inahusu zaidi mabadiliko kwa wavulana wakati wa kubarehe, ni kipindi ambacho ni kutoka utotoni kwendea ujana. Soma Zaidi...

Namna ya kumfanyia usafi Mgonjwa kwa mwili mzima.
Posti hii inahusu namna ya kumfanyia mgonjwa usafi mwili mzima, ni njia ambazo utumika kumfanyia mgonjwa usafi mwili mzima au kumwosha Mgonjwa hasa wale walio mahututi na hawawezi kuamka kitandani. Soma Zaidi...

Dalili za ugonjwa wa Saratani.
Saratani inahusu ugonjwa wowote kati ya idadi kubwa ya magonjwa ambayo yanaonyeshwa na ukuaji wa seli zisizo za kawaida ambazo hugawanyika bila kudhibitiwa na kuwa na uwezo wa kupenya na kuharibu tishu za kawaida za mwili. Saratani mara nyingi ina uwezo Soma Zaidi...

Zijue hatua za kufata ili kuepuka maradhi ya tumbo
Posti hii inaelezea kuhusiana na hatua za kufata ili kujikinga au kuepuka maradhi ya tumbo.kuna vitu vikikosekana husababisha maumivu ya tumbo. Soma Zaidi...

Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya nne)
Post hii inahusu zaidi watoto Hawa wawili wakiwa kwenye kituo cha mapumziko ambapo mtoto wa tajiri anabugia soda aliyopewa na yule mwalimu pia tumbo linaanza tena na anaanza kuendesha Soma Zaidi...

SAFARI YA MUUJIZA ( SEHEMU YA PILI)
Post hii ni mwendelezo wa hadithi ya safari yenye muujiza ,ni pale mtoto ya Mungu mengi anafika kwenye kituo Cha ntonga na kuona yake mazingira na kufahamu njia ya kwenda kule. Soma Zaidi...

Faida za karoti
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za karoti na umuhimu wake kiafya Soma Zaidi...