Njia za kuongeza uwezo wa kuzaa au kuzalisha.

Njia za kuongeza uwezo wa kuzaa au kuzalisha.

Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuongeza uwezo wa kuzaa au kuzalisha kwa sababu kuna familia nyingi zinakosa watoto sio kwa sababu ni tasa ila kuna njia mbalimbali za kuongeza uwezo wa kuzaa kama ifuatavyo.

Njia za kuongeza uwezo wa kuzaa.

1.kuwa na uzito unaofaa.

Kwa kawaida uzito unapaswa kuwa sawia kwa sababu uzito ukiwa mkubwa unaleta shida na ukiwa mdogo zaidi na lenyewe ni shida kwa hiyo uzito wa wazazi wote wawili unapaswa kuwa sawa ili kuweza kusababisha uzalishaji nzuri kabisa.

 

2. Kuweka mbegu za kiume katika hali nzuri.

Kwa kawaida mbegu za kiume zinapaswa kuwa katika hali ya ubora kwa hiyo baba anapaswa kula mlo kamili ili kuweza kutingisha Mimba.

 

3. Kuepuka matumizi ya tumbaku na kudhibiti matumizi ya pombe kwa sababu usababisha Mama na baba kushindwa kuzalisha vizuri.

 

4. Pia wazazi wote wanapaswa kujikinga na magonjwa mbalimbali kama vile magonjwa ya zinaa, na magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kusababisha uzalishaji kuwa mbaya.

 

5. Kufanya tendo la ndoa mara kwa mara hasa wakati wa siku za kubebea mimba, fanya mapenzi kabla ya siku tano wakati wa kurutubishwa kwa yai na fanya mapenzi siku mbili baada ya yai kuchevushwa.

 

6. Kunywa pombe kistaarabu.

Yaani pombe zisizidi kiasi kwa mfano bia moja kwa siku au  kiasi kidogo kwa siku, ila zisizidi kipimo. Kwa sababu unywaji wa pombe kupita kiasi usababisha kupungua kwa hormone ya testerone .

 

7. Punguza matumizi ya kahawa.

Kwa kawaida kwenye kahawa kuna kafein ambayo inaleta shida kwenye uzalishaji hasa hasa kwenye homoni.

 

8 epuka matumizi ya tumbaku,

Kwa kawaida  matumizi ya tumbaku usababisha matatizo kwenye DNA tunajua kabisa kwenye DNA ndicho chimbuko cha mwanadamu.

 

9. Epuka mazoezi magumu.

Kwa kawaida mazoezi  na kwa mda mrefu ukandamiza ovulation na kuaribu homoni ya  projestoren, kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwa na mazoezi madogo madogo.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views: 3516

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Bongolite - Game zone - Play free game     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 ai web app     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Habari nilitaka kujua kuhusu ugonjwa wa fungusi kwenye uume

Je na wewe unasumbuliwa na fangasi wenye uume. Post hii ni kwa ajili yako.

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu mapacha wanaofanana

Post hii inahusu zaidi watoto mapacha wanaofanana,ni watoto wanaozaliwa wakiwa wanaofanana kwa sura na hata group la damu huwa ni Moja.

Soma Zaidi...
SIKU HATARI ZA KUPATA UJAUZITO KWA MWENYE MZUNGURUKO WA SIKU KIDONGO AU NYUNGI

SIKU YA KUPATA UJAUZITO Kawaida wanawake walio wengi mzunguruko wa siku zao ni siku 28 lakini wapo ambao ni zaidi ya hapo na wapo ambao ni chini ya hapo.

Soma Zaidi...
Maumivu ya mgongo kwa wajawazito: Chanzo chake.

Maumivu ya mgongo ni mojawapo ya changamoto za kawaida zinazowakumba wanawake wengi wakati wa ujauzito. Ingawa mara nyingi ni hali ya kawaida inayotokana na mabadiliko ya mwili, inaweza kuleta usumbufu mkubwa katika maisha ya kila siku. Makala hii inaangazia vyanzo vya maumivu haya na jinsi unavyoweza kuyapunguza ili kupata kipindi cha ujauzito kilicho na utulivu.

Soma Zaidi...
Dalili za kuharibika kwa mimba

Katika post hii utajifunza ishara na dalili ninazoonyesha kuwa mimba ipo hatarini kutoka ama inaweza kuwa imeshatoka.

Soma Zaidi...
Dali za udhaifu wa mbegu za kiume.

Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo zinaweza kujitokeza na zikaonesha kwamba mbegu za kiume ni dhaifu au ni chache.

Soma Zaidi...