Njia za kupunguza tatizo la kutanuka kwa tezi dume.

Posti hii inahusu zaidi njia ambazo tunaweza kutumia ili kuweza kupunguza tatizo hili la kutanuka kwa tezi dume, kwa hiyo tunaweza kutumia njia zifuatazo ili kuweza kupunguza tatizo hili kwenye jamii kama ifuatavyo.

Njia za kupunguza tatizo la kuvimba kwa tezi dume.

1.Kwanza kabisa tunajua kubwa Ugonjwa huu umeweza kusambaa kwa kiasi kikubwa na kusababisha madhara kwa hiyo tunaweza kutumia njia zifuatazo ili kuweza kupunguza tatizo hili

 

2. Tunapaswa kula vizuri.

Kula vizuri kwa maana ya kula mchanganyiko wa vyakula sio kula chakula kimoja hata kama una uwezo wa kawaida unaweza leo kula viazi kesho ugali, siku nyingine wali na pia kutumia mboga za majani na matunda hata sio lazima kuwa na mafuta ili utumie mboga za majani au kama una uwezo kula chakula kadri ya uwezo wako maana katika vyakula tunaweza kutibu mambo mengi bila kujua.

 

3. Jaribu kupunguza sumu mwilini.

Kwa wakati huu tunakula sana vyakula vyenye sumu kama vile mafuta mengi kwenye chakula, vyakula vya Makopo, chips, baga na vyakula vingine vya namna hiyo na pia kuna unywaji wa pombe kali kupita kiasi na pia kutumia dawa bila ushauri wa kitaalamu , mambo hayo yote uongeza sumu mwilini kwa hiyo tunapaswa kuepuka vyakula hivyo kuvila kwa muda mrefu badala yake punnguza matumizi ya mafuta na kunywa sana maziwa.

 

4. Daima epukana na ngono zembe.

Kwa wakati huu kuna mlipuko wa magonjwa ya zinaa kila wakati kama vile kaswende, kisonono na mengine mengi kwa hiyo tunapaswa kutumia kondomu wakati wa kujamiiana au kutibu maambukizi ili kuweza na kuendelea kuwepo kwa kuvimba kwa tezi dume.

 

5. Pia wanaume wanapaswa kufanya mazoezi.

Kwa kufanya mazoezi tunaweza kuna vitu vingi tunapata kwa sababu pale mtu akitoa jasho uchafu mwingi utoka na mwili huwa huru na kutokana na mazoezi tunaweza kuepusha Magonjwa mengi tusiyotafahamu.

 

6. Kuepuka Matumizi ya pombe kali na sigara.

Kwa matumizi ya pombe kali na sigara usababisha viungo mbalimbali vya mwili kulegea na kutofanya kazi vizuri hali hii inaweza kusababisha maambukizi sehemu mbalimbali za mwili na mwili kuwa dhaifu hatimaye Magonjwa mengi yanaweza kutokea hata kuvimba tezi dume.

 

7. Kuepuka na msongo wa mawazo.

Siku hizi kuna tatizo hili la kuwa na msingi wa mawazo kwa walio wengi hali ambayo uwafanya eatu kubwa na matatizo mengi ya kiafya. Kama kuna shida yoyote shirikisha rafiki, angalia mpira, au kitu chochote unachokipenda ili mradi kupunguza mawazo.

 

8.Katika maisha yetu tuwe na tabia ya kuchukua vipimo kwa ajili ya kuangalia afya zetu na tabia ya kuwahi hospitali unapohisi kubwa  kuna kitu ambacho hakipo sawa kwa sababu, Ugonjwa wowote kama hata hauna tiba ukiwahi hospitalini madhara yanakuwa madogo kuliko pale ukienda umechelewa,

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/03/09/Wednesday - 10:58:13 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 863

Post zifazofanana:-

Chemsha bongo na bongoclass
Jipime uwezo wako wa kufikiri pamoja nasi. Soma Zaidi...

Je vvu inaweza sababisha mate kujaa mdomoni
Je kujaa kwa mate mdomoni ni dalili ya kuwa na VVU, na je ni zipi dalili za Virusi Vya Ukimwi (VVU) mdomoni? Soma Zaidi...

Kazi kuu tatu za vitamini C mwilini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kazi kuu tatu za vitamini C Soma Zaidi...

Mafunzo yatokanayo na vita vya uhudi
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Fahamu tiba ya lishe ya ugonjwa wa kisukari
Post hii inahusu zaidi tiba ya lishe ya ugonjwa wa kisukari ni tiba ambayo utumiwa sana na wagonjwa wa kisukari na walio wengi na wamefanikiwa kupona Soma Zaidi...

Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume Soma Zaidi...

Sanda ya mwanamke na namna ya kumkafini
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi hadithi ya Binti mfalme ni hadithi ya kusisimua, kuhusu hadithi hii ni kwamba mfalme alihitaji mtoto wa kiume ila wanawake wote hawakumpata ila alitokea mke mdogo mmoja wa mfalme akajifungua watoto wawili mapacha mmoja wa kiume na Soma Zaidi...

Dalili za uchovu wa joto mwilini.
Uchovu wa joto ni hali ambayo dalili zake zinaweza kujumuisha kutokwa na jasho kubwa na mapigo ya haraka, ambayo ni matokeo ya joto la mwili wako. Ni mojawapo ya magonjwa matatu yanayohusiana na joto, huku tumbo la joto likiwa kali zaidi na Kihar Soma Zaidi...

Ukuaji wa mmea
Je wajua kwa nini mmea kama nyasi na miti hukua? Posti hii inahusu' zaidi ukuaji wa mimea katika mazingira yetu kwa sababu watu hawatambui kwamba mimea .ni chanzo cha mahitaji kwa binadamu. Soma Zaidi...

Huduma kwa mama mwenye mimba Inayotishia kutoka.
Post hii inahusu zaidi huduma ambayo Mama anapaswa kutolewa pindi mimba inapotishia kutoka huduma hii utolewa kulingana na Dalili tulizoziona zinazohusiana na mimba kutishia kutoka. Soma Zaidi...

Ndani ya jumba la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...