Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kupunguza tatizo la kuwepo kwa uzito mkubwa pamoja na kitambi
1. Tunapaswa kufahamu kwamba mara nyingi tatizo la kuwepo kwa uzito mkubwa na kitambi ni mtindo wa maisha ambapo kwa walio wengi ujiachiaa kabisa katika maisha na vyakula, kwa mfano unaweza kuona mtu anatoka nyumbani kwenda kazini kwa kutumia gari na akifika kazini ni kukaa tu na jioni akitoka kazini ni kupiga bia na nyama yoyote ile na pengine anaongezea chips akitoka hapo anafika nyumbani ni kuangalia movies na kusubiria chakula, watu wanaishi hivyo hata bila ya mazoezi hatimaye kuota kitambi na unene kupita kiasi.
2. Kwa hiyo watu wanapaswa kubadilika na kufuata yafuatayo ili kuweza kuepuka na tatizo la kuwepo kwa vitambi kwa kubadilisha mtindo wa maisha kwa kupiga mazoezi mara kwa mara walau mara tatu kwa wiki pamoja na kutumia maji ya uvuguvugu ili kupunguza vitambi na unene uliopitiliza.
3. Epuka matumizi ya vyakula vya wanga.
Kwa kawaida kitu kikubwa ambacho kipo kwenye vyakula vya wanga ni starch na ndiyo inayosababisha kuwepo kwa unene uliopitiliza.
4. Epuka matumizi ya vyakula vyenye sukari nyingi.
Kwa kawaida tunajua kazi ya sukari ikiwa nyingi mwilini usababisha kuwepo kwa mwongezeko wa mwili pamoja na uzito kwa hiyo ni vizuri kutumia sukari kidogo kwenye vinywaji.
5. Kufunga ili kuweza kuchoma calories ambazo zimo mwilini ambazo utokana na ulaji wa vyakula vyenye wanga na sukari.
6. Tumia vyakula vyenye wingi wa protini na gari kwa kiasi kidogo na pia tumia uchache wa unga na sukari.
7. Katika kupunguza uzito ni vizuri kabisa kufahamu kwamba matumizi ya vyakula vya wanga mara kwa mara hata kama unafanya mazoezi sio rahisi kupunguza tatizo kwa hiyo punguza matumizi ya vyakula vyenye wanga.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Kuzimia ni hali ya kupoteza fahamu ambako kunaendana na kutokuhema.
Soma Zaidi...Kifafa hakiambukizi na ugonjwa wa ubongo lakini kifafa pia hakiathiri akili au ubongo Ila kikiwa kifafa Cha kudumu na Cha nguvu ndio huweza kuadhiri. Pia Kuna kifafa Cha mimba na kifafa Cha kawaida.kifafa Cha mimba ndio kinahatari Sana kuliko Cha Kawaid
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya roghage
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa aliyeungua na Moto.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu magonjwa ya vidonda vya tumbo, ni hatari inayotokea kwa mtu ambaye haujatibiwa vidonda vya tumbo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyuko
Soma Zaidi...Posti hii inahusu njia mbalimbali ambazo utumika kupitisha chanjo, njia hizo utegemea na kazi ya chanjo kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi malengo ya kusafisha vidonda, kwa sababu Kuna watu wengine huwa wanajiuliza kwa nini nisafishe kidonda hospitalini au kwenye kituo chochote Cha afya, yafuatayo ni majibu ya kwa Nini nisafishe kidonda.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mgawanyo wa matibabu ya kifua kikuu, tunajua kubwa kifua kikuu ni Ugonjwa ambao utumia mda mrefu kidogo katika matibabu kwa hiyo mgawanyiko wake uko kwenye sehemu mbili muhimu kama tutajavyoona
Soma Zaidi...